in

AKUFUKUZAYE AKWAMBII TOKA: ASHURA NA BATULI

Akufukuzaye Akwambii Toka ni Simulizi ya Maisha inayo Wahusu Marafiki Wawili Ashura na Batuli. Utafahamu Kilicho Jiri Mpaka Marafiki hawa Wakafikia ku Kwaruzana, Soma Mpaka Mwisho Kufahamu. Mwandishi wako ni @aisha-mapepe

Akufukuzaye Akwambii Toka

SIMULIZI ZENYE MAFUNZO: AKUFUKUZAYE AKWAMBII TOKA

Simulizi yetu inaanzia Katika Nyumba Moja Wanayoishi Marafiki Wawili Ashura Pamoja na Batuli. Walikuwa Wakizungumza, Ashura Akaanza Kumuambia Batuli.

“Mbona umepauka sana, au haujapaka mafuta, mmmh halafu unanenepa sana siku hizi” Nilimtizama Ashura na kusema “Mbona mimi najiona nipo kawaida Alafu nimepaka mafuta.” Huku akicheka kwa dharau Ashura aliingia ndani na Kumuacha Batuli Akiwa Amekaa kibarazani. Batuli Alijiuliza maswali mengi kwanini Ashura anamcheka alijitizama huku akihisi labda ana kasoro yoyote katika mwili wake lakini hakuiona. Basi Alimpuuza na kuendelea na safari yake.

Batuli ni mzaliwa wa Morogoro katika Familia ya watoto watatu, Baada ya kumaliza kidato cha sita nilipata nafasi ya kuendelea na Elimu ya chuo kikuu Jijini Dar es salaam. Kutokana na hali halisi ya maisha ya nyumbani nilipotokea wazazi wangu walikuwa hawana uwezo, hivyo ilinibidi nimuombe rafiki yangu Ashura anisaidie hifadhi katika chumba alichokuwa amepanga karibu na maeneo ya chuo. Ashura alinikubalia na hivyo nilipata sehemu ya kuishi bila ya kutumia Gharama yoyote.

Maisha yetu yalikuwa mazuri kwani tulipendana sana mimi na Ashura, kiasi kwamba pale shuleni watu walikuwa wakituita mapacha. Mara nyingi tulikuwa tukiongozana kama kumbikumbi. Kwa kiasi kikubwa Ashura alikuwa akinisaidia sana, kwani ni msichana aliyetokea katika familia ya kitajiri. Kwa Upande Wangu Mimi nilikuwa naishi maisha ya kujinyima sana kutokana na hali halisi ya Familia yangu.

*********

Baada ya mwaka Mmoja kupita tukiwa tunaendelea kuishi pamoja, Ashura alipata mchumba ambaye alikuwa akija kumtembelea mara kwa mara. Siku moja nikiwa Nimekaa kitandani nikijisomea Ashura alikuja na kusema “Batuli, leo mchumba wangu atakuja kulala hapa, sasa sijui itakuwaje”. Nilimtizama Ashura kwa dakika chache bila ya kuzungumza chochote halafu nikamwambia.
“Mh, lakini ni bora ungeniambia mapema sasa hivi ni saa tatu za usiku, nitaenda kulala wapi”

Alikuwa amesimama mlangoni huku akiguna na kusema “Sasa sijui itakuwaje, lakini mimi namwambia aje, tutajua la kufanya”. Moyoni mwangu nilikuwa nawaza “Hivi Ashura anawezaje kumwambia mpenzi wake aje kulala wakati chumba ni kimoja na kitanda ni kimoja sasa akija mimi nitaenda wapi”. Nilikosa amani kabisa lakini sikuwa na Namna. Haukupita muda mrefu yule mchumba wake alikuja na walikubaliana kuwa watalala kitandani na mimi nitalala kwenye kochi.

Siku hiyo nililala kwa tabu sana, lakini ilinibidi nivumilie na kufikiri kuwa ilikuwa ni siku hiyo moja tu, lakini hali ile iliendelea mara kwa mara. na mimi nilikuwa nikilala kwenye kochi. Siku moja nilirudi nikiwa nimechelewa nakukuta mlango umefungwa. nilibisha hodi bila ya mafanikio. Ilinibidi niondoke na kwenda kuomba kulala kwa jirani. Kesho yake nilipomuuliza Ashura kwanini hakunifungulia mlango akasema kuwa alikuwa amepitiwa na usingizi.

Mambo yaliendelea kuwa magumu, kwani Ashura aliendelea kunifanyia visa vya hapa na pale wakati mwingine alikuwa akinizungumzia vibaya kwa watu. kuwa mimi namtaka mpenzi wake halafu mimi ni masikini na sina uwezo kila kitu namtegemea yeye. Nilikuwa navumilia sana.

*********

Siku nyingine alikuwa akija anaimbia nyimbo za mafumbo 🎵”kodi nimelipa mie, kulala ulale wewe, chakula nimenunua mie kula unakula wewe” Majanga mbona Majanga”🎵 huku akicheka na kuondoka. Kutokana na hali halisi ya maisha yalivyokuwa yakiendelea niliamua kumuomba rafiki yangu mwingine anisaidie hifadhi kwa muda huku nikiwa naendelea kutafuta pesa ya kupangisha chumba pale chuoni.

Siku hiyo nilipokuwa nakusanya vitu vyangu Ashura alikuja na kuniuliza “Hee Batuli, mbona unondoka jamani, mmh! Ghafla Ghafla hivi”. Nilimtizama na kusema “Akufukuzaye akwambii toka hata siku moja vitendo tu utaviona kuwa huyu mtu hapendi uendelee kuishi naye, mimi nimeamua kuondoka. samahani sana kama kuna jambo lolote nilikukosea, na pia asante sana kwa kunisaidia kwa kipindi chote tulipokuwa pamoja”.

Baada ya miezi sita kupita Ashura alikuwa ametengana na mpenzi wake. na kwa kipindi chote hicho alikuwa Hazungumzi na mimi, siku moja aliamua kunifuata na kuniomba msamaha kwa yote aliyonikosea. “Naomba unisamehe Batuli mimi ni binadamu sijakamilika, nisamehe rafiki yangu najua nilikukosea sana”. Kwasababu mimi nilikuwa sina kinyongo tena bila hiana nilimsamehe Ashura na tuliendelea kuwa marafiki kama kawaida.

MWISHO.

Katika Simulizi ya Kufundisha Kama Hii ya Marafiki Hawa Wawili Ashura na Batuli. Walio Kua Wameshibana Hapo Mwanzo, Na Baadae Waka Kwaruzana. Je, Katika Maisha yako Ulisha Kutana na Mkasa wa Akufukuzaye Akwambii toka. Niandikie Hapo chini Jambo lako japo kwa Kifupi Itakuwa Vyema.

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Abunuasi na Hukumu ya kijana

ABUNUASI NA HUKUMU YA KIJANA: Simulizi Fupi

Amka Mama

AMKA MAMA: SIMULIZI YA KUSISIMUA NA KUHUZUNISHA