in

AMKA MAMA: SIMULIZI YA KUSISIMUA NA KUHUZUNISHA

*********

Veronica mwanangu. Njoo mwanangu, Njoo karibu. Nimeamka mama yako. Mama yule aliongea kwa sauti ya chini huku akiunyoosha mkono wake kumuelekea mwanaye ambaye alikuwa akisitasita kwenda.

Tafadhali njoo mwanangu. Hujafanya chochote kibaya. Usiogope. Mama yule alikuwa kamaameusoma moyo wa Vero hivyo Veronica alisogea alipkuwa kalala mama yake na kumkumbatia kwa nguvu ikifatiwa na sauti ya kilio iyotawala kwa muda kiasi kabla ya Doktari kuingilia kati na kuwasihi wasifanye vile kwa manufaa ya mgonjwa ambaye alikuwa hajapona kabisa kutoka katika hali yake.

Umeamka mama yangu. Asante sana MUNGU kwa kumrudisha mtu nimpendaye katika maisha yangu. Asante sana MUNGU. Veronica aliongea hayo huku akiangalia angani akiwa na imani kuwa MUNGU alikuwepo huko.

Nimerudi kukupooza mwanangu. Nisingevumilia hali uliyokuwa nayo baada ya mimi kuondoka. Nimepigana ili kuinusuru roho yangu kuondoka bila kuwaona wajukuu zangu na ndoa yako. Nakupenda sana Vero. Mama yule aliongea huku akiwa kaweka tabasamu hafifu lakini lenye matumaini.

Dokta. Veronica alimuita Daktari ambaye alkuwa kasimama pembeni huku tabasamu la haja likiwa limetawala usoni mwake.
“Naam binti yangu. Daktari aliitika.

“Mama karudi. Veronica aliongea kwa furaha kisha akamfata Daktari na kumrukia huku pia akimpa kumbate ambalo Daktari alishindwa cha kufanya zaidi ya yeye pia kumkumbatia. Hujanimalizia hadithi yako lakini. Ulifanikiwa kupata pesa za kumtibia mama yako? Daktari aliuliza baada ya kumaliza kukumbatiana na Veronica.

Vero alimuangalia mama yake kama mwenye kumuuliza amuhadithie au asimuhadithie ile hadithi huyu Daktari. Na mama yake aling’amua lile swali la macho,bila hiyana alimpa ruhusa ya kuimalizia ile hadithi.

Vero alizidi kumuangalia mama yake kwa macho ya huruma,na kisha kwa upendo mkubwa, alikaa pembeni yake na kuanza kuongea tena.

Shida na mateso uliyoyapitia ukiwa nami, nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisiposema asante na MUNGU akupe mwanga zaidi katika maisha yako.

*********

Mama, asante pia kwa kuniwezesha kuaminika na watu japo elimu yangu yenyewe siyo kubwa ya kuweza kufanya haya ninayofanya sasa hivi. Hakuna kama wewe mama, na ninakupenda sana mama yangu, hilo siwezi kulificha kwa MUNGU hata kwa yeyote yule ambaye atataka kujua kiasi gani nampenda mama yangu. Alimshukuru mama yake na kisha akamgeukia Daktari.

Dokta, ni miaka sita sasa imepita tangu lile tukio la mama kuumwa litokee. Nasema ukweli kuwa sikuamini siku ile nilipoondoka na kutokomea kusipojulikana kisha baada ya siku tatu nikarudi kuja kushuhudia kitakacho kutokea, kwa sababu sikupata ile fedha niliyoagizwa na hospitali.

Mwili wangu ulichezewa lakini haukuweza kufanya fedha ya mama kutibiwa ipatikane. Lakini MUNGU anamaajabu yake, na MUNGU si Athumani Dokta. Nilishikwa na butwaa pale nilipofika hospitali na kumkuta njemama yangu anaota jua la jioni, na aliponiona, alinyanyuka na kunikimbilia kana kwamba hakuwa kitandani wiki bila kujitambua.

Hata pale aliponikumbatia, nilihisi ni ndoto bado kama hii ndoto nayoiona sasa hivi. Lakini joto na sauti yake ya msisitizo ndivyo vilivyoamsha hisia zangu na kurudisha furaha yangu tena.

Watu walitutazama jinsi mama alivyokuwa amenidandia mwanae na huku mwana naye kakushikilia vizuri ili msidondoke, najisikia faraja sana mama yangu kwa lile tendo.”Hapo tena alimgeukia mama yake na kumkuta kapambwa na tabasamu mwanana usoni pake. Akamgeukia Daktari tena na kuendelea kusimulia.

Lakini siri ya kupona kwako mama, ni nini? Ni kwa sababu ya wema uliyonifundisha kuutenda tangu utotoni kwangu. Wema wangu niliyoutenda miaka kumi na kitu iliyopita kwa wale wazungu, siku ile uligeuka kuwa dawa yako mama yangu.

Sikuamini kuwa yule kaka aliyelipa zile fedha za matibabu kuwa ndiye yule aliyenipa chokoleti kipindi kile cha nyuma.

*********

Mtu ambaye alinifanya nijigambe kwa watoto wenzangu pale kijijini kwa sababu ya chokoleti aliyonipa. Leo hii ni mvulana mkubwa na mwenye akili zake za kufanya mambo yake binafsi,na siyo yule wa kulilia tena vitu kwa wazazi wake. Kweli hii ndio dunia bwana.

Kalipa wema wake kwetu japo sikuwahi kumfanyia jambo kubwa zaidi ya kuwazungusha yeye na wazazi wake mbuga za wanyama. Sijajua alilipata taarifa wapi kuwa tupo Dar es Salaam, ila nachojua alitusaidia hadi mama akawa mzima lakini ugonjwa wake umerudi tena mwaka huu. Na umekuja kwa kasi ya kutaka kumchukua kabisa.

Nakushukuru Daktari na jopo lako la wauguzi kwa uangalizi wenu kwa mama yangu. Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa MUNGU awazidishie kila mtakachomuomba.”Veronica alimaliza kumsimulia Dokta na kugeuka tena kwa mama yake.

Tumepata watoto mapacha mama na mume wangu mtarajiwa. Nimekuja nao sema nimewaacha nyumbani,utawaona wajukuu wako. Veronica alimpa taarifa mama yake ambaye alizidi kutabasamu baada ya kusikia hayo.

Daktari. Yule mzungu aliyenipa chokoleti na kumlipia mama gharama za matibabu,ndiye mume wangu mtarajiwa,nilikuwa naishi naye Uholanzi. Mimba niliyokuwa nayo,nikashauriwa nisisafiri umbali mrefu kwa sababu ya afya yangu.Maisha ndivyo yalivyo Daktari. Huwezi jua wema wa leo utaleta fadhila lini. Tenda wema,fadhila zitakuja pale usipopategemea.”Vero alimaliza kwa ushauri mdogo kwenda kwa Daktari aliyemtibu mama yake.

Alimuangalia mama yake na wote wakajikuta wanacheka cheko ya pamoja ambayo Daktari alishindwa kuitafsiri bali alisubiri vicheko vile viishe ndio aulize. Lakini haikuwa hivyo,mtu na mwanaye walipomaliza kucheka, mara moja wakampa jibu Daktari juu ya vicheko vyao.

Na wewe unajidai umekuwa mtu wa ushauri eeh, embu lione kwanza. Mama Vero aliongea hayo akimtania mwanaye.

Wewe ndiye uliyenifundisha tabia hiyo. Nimekuiga sasa. Vero alijibu na kuongezea kicheko kirefu huku Daktari akiondoka na kuwaacha mule wodini wakiendelea kutaniana.

BAADA YA MIEZI MITATU.

Hali ya Mama Vero ilikuwa imetengamaa na sasa alikuwa mbele ya umati wa watu akitoa wasaha wake kwenda kwa mwanaye mpendwa Vero, baada ya mwana huyo kufunga pingu za maisha na mtu aliyemuita muokozi wa maisha yake.

Mwanangu Vero, endelea kupigania nafsi za wengine kama nilivyopigania mimi. Nimekulea katika malezi hayo na ndio maana leo hii umenipigania mimi. Sina cha kukulipa na wala sihitaji malipo yako,umelipa mengi sana ambayo hapo mwanzo sikufahamu kama uliwahi kufanya hivyo.

Mama Vero aliongea na kisha aliangalia sehemu fulani iliyopo mle ukimbini, na moja kwa moja alimuona Daktari aliyemtibia hadi siku ile amesimama pale.

Namshukuru sana Daktari wangu aliyekuwa ananiangalia hadi leo hii nimesimama hapa mbele yenu. Nilikuwa wa kufa lakini Daktari hakukata tamaa licha ya miezi mitano niliyokaa kitandani bila kujitambua. Nakushukuru sana Daktari Zubery Mavugo. MUNGU akujaze roho hiyohiyo. Mama Vero aliongea mengi sana usiku ule lakini mengi yalikuwa ni ushauri pamoja na mahaso.

Taarifa ya Daktari kuhusu ugonjwa wa mama yule, ilisema kuwa Mama Vero alikuwa anasumu ya tetenasi ambayo haikupona kipindi kile cha nyuma, hiyo ndio ilimlaza mama yule kwa miezi mitano. Lakini aliwatoa hofu baada ya kuwaambia kuwa hali hiyo haitotokea tena kutokana na tiba alizompa mama yule.

Jina halisi la Mama Veronica ni Sarafina Sauti huku mwanaye akiitwa Veronica Tambo na watoto wake mapacha waliitwa Elizabeth na Michael. Baba Yao aliitwa John Drake, Raia wa Holland.

MWISHO.

Huo Ndio mwisho wa Simulizi hii ya Amka Mama, Natumaini Kuna Jambo Umejifunza. Kwa Simulizi nyingine Kama Hizi Tembelea Hapa Hapa Africona. Simulizi Zote ni Bure Hutoi Hata Sumni. Kikubwa ni Bando Lako tu.

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Akufukuzaye Akwambii Toka

AKUFUKUZAYE AKWAMBII TOKA: ASHURA NA BATULI

Sarafina Simulizi

SARAFINA: MOJA KATI YA SIMULUIZI PENDWA MNO