in

Biashara ya Duka: Jinsi ya Kuanzisha na Kupata Faida Nzuri (2022)

Tazama Matokeo Hapa

Download Mitihani

Jinsi ya Kuanzisha Biashara ya Duka na Kupata Faida Nzuri (2022). Katika Biashara ya Dukani Kuna Mambo mengi ya Kuzingatia ili Uweze Kupata faida Nzuri ya Kueleweka na Maisha Kusonga.Hakikisha Hauruki Kipengele chochote Katika Ukuraha Huu. Maelezo yote yamebeba Point za Msingi za Kukuwezesha Wewe Kuanzisha Bishara hii ya Duka, au Kama Umesha Anzisha Kuiboresha iweze Kuwa na Faida Zaidi.

Biashara ya Duka

MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA KATIKA BIASHARA YA DUKANI.

Baada ya Kuandaa Mtaji wako wa Kuanzisha Biashara ya Duka Unapaswa Kuzingatia Mambo ya Fuatayo. Kuhusu Mtaji Unaweza Kuanza na 1,000,000 Tsh au Zaidi Kulingana na Uwezo wako.

 • Kauli.
 • Location.
 • Usimamizi.
 • Timing.
 • Kumbukumbu.

Kauli.

Katika Biashara yoyote Kauli ni Kitu cha Msingi Kuliko Vyote. Kama Kauli yako ni mbovu kwa Wateja Utaambulia Kufukunza Inzi tu, Maana Hakuna anaependa Kujibiwa Vibaya.

Ila Ukiwakaribisha Wateja wako kwa Kauli za Kiungwana na Uchangamfu Kulingana na Mood Aliyo Kuwanayo Mteja wako Basi Ume Win. Lazima Wateja Watakupenda.

Location.

Angalia sehemu utaweka hiyo biashara yako kuna watu wa aina gani. Hii itakusaidia hata kujua ni bidhaa za aina gani uweke dukani. Pia ni Bidhaa gani Usiweke Kulingana na Mahitaji yao.

Usimamizi.

Hapa inategemea kama Utamuajiri Mtu. Au Kama Upo Mwenyewe usimamizi Utakua ni juu Yako. Ila Kwa Wale wanao Ajiri watu Hakikisha Unamsimamia Katika Namna Ambayo. Unaemsimamia Hatakuona Wewe ni Kero.

Pia, Usipokuwa makini na Usimamizi utashangaa binti/kijana wa dukani anabadili Simu, Viatu na vitu vingi kwa kukuibia. kama hufanyi Usimamizi kwa kubanwa na muda, funga  CCTV Camera hata mbili tu, zinawaogopeshaga kuiba.

Timing.

Kawaida ya biashara hizi zinahitaji Muda Mwingi Uwepo Eneo la Kazi. hivyo UKICHELEWA kufunga na UKIWAHI kufungua una nafasi kubwa ya kufanikiwa. Timing vile vile inahusiana na ununuzi wa baadhi ya bidhaa ambazo ni za msimu Ukiziwahi waweza hata kuzinunua kwa Nusu Bei. Ukapiga Pesa yako Nzuri.

Kumbukumbu.

Waswahili Husema Mali Bila Daftari Huisha Bila Habari”Wahenga Hawa Hawakukosea Hata Kidogo. Unapaswa Kuzingatia Uwekaji wa Kumbukumbu zako Kila Mara. Unapaswa Kuwa na Daftari lako ikiwezekana Chukua ata Couter Book Uandike Taarifa Zote Muhimu za Dukani ikiwemo.

 • Mauzo.
 • Manunuzi.
 • Gharama za uendeshaji.
 • Bank
 • TRA
 • Mikataba/Mengineyo.

Zingatia kufanya hivi ili Biashara ya Duka Iweze Kukulipa Zaidi.

• Hakikisha unanunua bidhaa kidogokidogo kwa kila item.
• Weka bidhaa ambazo hazitakusumbua sana kuuza kwa eneo lako, mfano. Juice, Maji, Unga, mafuta Kula, sabuni etc, bidhaa ambazo ni mahitaji ya lazima.
• Weka vocha kwa huvutia wateja. Pia Jiongeze uwe ni Wakala wa Mitandao. Biashara hii inalipa sana kama utajituma na kuwa na nidhamu ya matumizi.
• Kama Bidhaa inayo uliziwa Sana dukani haipo, hakikisha unaandika Kisha uinunue.
• Survey maduka ya jirani Kujua bei na baadhi ya bidhaa ambazo hawana we uziweke japo kidogo.

Namna bora ya kufanya hesabu dukani.

Unahitaji vitabu (nunua hata counter books) vya kumbukumbu za hesabu kama vile:

 • KITABU CHA MATUMIZI
 • KITAB CHA MANUNUZI, KITABU CHA MAUZO
 • KITABU CHA MADENI – kwa unaowadai na wanaokudai
 • KITAB CHA MALI YA BIASHARA, KITABU CHA STOCK.

Vilevile unahitaji kununua mafaili ya kutunzia stakabadhi za manunuzi, malipo, bank slips, mikataba, na nyinginezo ktk mpangilio kila moja na faili lake.

Pia unatakiwa kuwa na diary au note book kubwa kuandika bidhaa ambazo hautakuwa nazo wateja ambazo wateja wamehitaji (missing items) ili kukupa kumbukumbu za kuzinunua. Kitu kingine panga vitu ktk mpangilio mzuri usifanye duka ili mradi duka, panga vitu vinavyofanana kwa pamoja na usijaze items nyingi katik display kwa pamoja.

Kauli nzuri kwa wateja, uharaka, uhakika, ubora na hali ya kujali wateja ndo uchawi wako ktk biashara hii. Usisahau kufuga paka mdogo kufukuza panya. JINGINE MUHIMU, hakikisha kila siku asubuhi unapeleka mauzo ya jana yake benki kabla ya kuyatumia, pia usajili biashara yako na uifungulie akaunti ambayo itakuwa na jina la hiyo biashara (mfano JAPHARY RETAIL SHOP).

Biashara ya duka la Rejareja siyo ya kudharau hata kidogo.

Inatunza familia kabisa na kusaidia kugharamia baadhi ya matumizi kwenye familia. Watu wengi waliotanguliaga kuifanya hii biashara wako mbali saaana. wengine wamejenga na kumudu hadi Kujenga nyumba kwa Biashara Hii Hii ya Duka.

USIACHIE FURSA. Kamwe usiuze ‘HAKUNA’
Kitu kikubwa katika maduka ya Rejareja ni kuhudmia hitaji la kila mmoja kadri uwezavyo. Kamwe usiuze hakuna ikiwa inawezekana icho kitu/bidhaa inaweza kuuzika katika duka lako. Hata kama mhitaji ni mmoja, mletee anachotaka. Ili mradi kile anachohitaji kipo kwenye uwezo wako na unaridhia kuuzika kwako.

Biashara ya Pombe na sigara.

Siagara, Angalia eneo lako la biashara kama kuna watu wanahitaji sigara wawekee.(ikiwa umeridhia na hufungwi na imani yako pia) Beer unaweza weka bia katika miundo miwili, kuuza take awa y(wanaenda kunywa nyumbani), au kama eneo linaruhusu, kukawa na kasehemu wakawa wanakunywa kwa ndani/bandani (duka-grocery). NB usieke pombe ya banana kama eneo lako ni la wastaarabu).

Pombe za kupima kwa shot.

Pima K-Vant, Valuu, Konyagi n.k kuendana na eneo shot 500/1000. Weka vipombe vichupa vidogo: Azura/Rivella/Zed/Diamond/Konyagi ndogo/KVant ndogo. ukinunua kwa caton utapata faida kubwa zaidi, ukinunua kwa maduka ya jumla pia utapata pia.

Mfano kwa maduka ya jumla Azura/Rivella n.k

Vitu vya kupima pima

Kuna mchangiaji ameshaeleza kuhusu Prestige za kupima kwenye kurasa zilipita. Labda niongezee
Maziwa: Kuna maziwa ya kupima, ya fresh/chai na ya mtindi, itategemea zaidi na eneo ulipo sababu ya usafi/usalama kwa wateja wako.

Maziwa bei ya kununua na kuuzia itategemea na maziwa unayapata kwa bei gani. Kuna vitu vingine dukani vinatembea fasta pia, kama unga wa lishe, unaochanganya mwenyewe pia. Ila kwa lengo la kuzungusha hela na kueka ubora unaeza nunua kwa watu na kisha ukaweka marhin kidogo ukauza dukani kwako.

Vitu kama sembe, Dona kama unaeza saga mwenyewe, margin inakuwa kubwa zaidi kuliko kununua.

NB: Hakikisha unatoa bidhaa bora inayofanana na hizi unga za special, wateja wengine hawaangalii brand, wanaangalia ubora/ladha basi.

Changamoto:

Changamoto za serikali anzia za kata (Bwana Afya). Manispaa (Ushuru) na TRA -Kodi havikwepeki, kutana nao utajua jinsi ya kudili nao. Kikubwa Hakikisha Unalipa Kwa Wakati Kulingana na Kipato Chao.

Natumai Utakuwa Umejifunza Kitu Kuhusu Biashara ya Duka. Nijulishe Hapo Chini Kwenye Comment Unamaoni Gani au Unahitaji Ushauri gani Kuhusu Bishara ya Dukani na Mimi nitakujibu Kwa Ufasaha. Kadiri niwezavyo.

Written by Teacher Pizo

My Name is Teacher Pinael Zakaria Olais. Wengi wamezoea Kuniita Teacher Pizo. Nipo Hapa Kuwasaidia wanafunzi katika Masomo yao. Niandikie Swali lako Hapo Kwenye Comment nami Nitakujibu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scholarship Opportunities Worldwide

Scholarship Opportunities Worldwide: Fully Funded (2022)

African Culture

AFRICAN CULTURE: Tribes and Traditions Found in Africa