in

BIBI MILELE NITAKULAUMU: SIMULIZI ZA KUSISIMUA

Bibi Milele Nitakulaumu Simulizi ya Kusisimua. Soma Mpaka Mwisho Simulizi Hii Fupi ya Kusisimua na kufundisha Utafahamu Mambo Mengi ya Maisha yenye Kukupa Mafunzo Mengi. Kufahamu Sababu ya Kijana Huyu Kumlaumu Bibi yake Ungana nami @aisha-mapepe

Bibi Milele Nitakulaumu

SIMULIZI FUPI YA KUSISIMUA: BIBI MILELE NITAKULAUMU

Jamani mume wangu mbona nilikupenda sana, nilikuthamini sana. Nilikupokea vyema katika nafsi yangu, niliruhusu moyo wangu ukupokee na kukutunza vyema. Mume wangu nilikuheshimu nilifanya kila ulichotaka ili tu nisivunje kiapo cha ndoa yetu.

Nilijitahidi kukuandalia chakula kizuri na hata pale uliponikosea basi Mimi nilijishusha na kukuomba msamaha ili tu maisha yaendelee. Upendo wote huo uligeuka uchungu wa milele na kilio kisichokoma, shida haina hodi niliamini kwamba mapenzi ni majani popote penye mbolea huotea.

Jamani mume wangu sikupenda kukuona ukiwa mpweke wala mwenye huzuni na ndio maana hata ulipofukuzwa kazi. Na kulia kumbuka nililia pamoja nawe na kipindi Kile ulipougua takribani miaka mitatu hakuna ndugu wala Rafiki aliyekuja kukujulia hali ila ni Mimi mke wako niliyekuwa nawe katika mateso yote hayo mpaka pale ulipopona na kuendelea na shuguli zako.

*********

Mume wangu kumbuka siku ile nilipopika samaki ulisema huwezi kula mpaka niweke limao. Tena ulinilazimisha nipande mwenyewe juu ya mti, Jamani mume wangu kipindi naanza kupanda ulinisindikiza kwa teke Kali sana lililotuwa vyema katika mgongo wangu, kwa jinsi nilivyokupenda sikutaka kukukwaza kabisa ikabidi nipande katika mti huo mrefu kidogo wa mlimao ulioko pale nyumbani nilifanikiwa mpaka nikafika juu, ila Ghafla shina nililokuwa nimekanyanga lilikatika yaani masikini ya Mungu nilidondoka chini kama Mzigo.

Nilipopelekwa hospitali nikaambiwa nilikuwa na mimba ya miezi miwili ivyo imetoka. Kisha Daktari akasema pingili za uti wa mgongo zimeharibika vibaya sana ivyo ikapelekea mwili mzima kupooza nikawa wakulala tu, yaani sikuweza kukaa, kusimama wala kutembea nilikuwa wa kulala tu.

Jamani nilivyorudi nyumbani mume wangu alinikataa alisema hawezi tena kuishi na mlemavu. Nililia sana uku maneno yakinitoka, “Jamani mume wangu nilikupenda sana tazama navyoteseka nimeumia kwa ajili yako Leo unanikana hunitaki tena mbona Mimi ulivyougua mpaka unatoa harufu nilivumilia mpaka ukapona,

Jamani Mume Wangu basi njoo unimalizie kabisa ili nikapumzike mbinguni kwa Baba. Yaani pamoja na kupooza huku ila bado umekuwa ukinifata nilipolala na kuanza kunitandika viboko toka asubuhi mpaka mchana uku ukisema nikupishe katika nyumba yako, hapana mume wangu unajua siwezi kutembea kabisa Mimi ni wakulala tu mpaka siku ntakayofariki, mume wangu nakusihi sumu mpe paka mbuzi utamdhulu. Kwani maumivu yote niliyoyapata bado tu unaendelea kuniadhibu, Upendo wangu kwako ndio umenifanya hivyi.

*********

Ndio sikatai unaleta wanawake ndani uku ukiwaambia achaneni na huyo. Mlemavu ni wakufa tu, jamani mume wangu hata kama unasema Mimi ni wakufa tu kumbuka wote njia yetu ni moja nashukuru sana umekuwa ukininyima chakula mpaka wiki moja na umenifungia ndani watu wasijue, asante mume wangu Mimi nilikupaka wanja ila Leo wewe wanipaka pili pili.

Namlaumu sana Bibi yangu kwa kumkeketa Mama mpaka ikapelekea. Mama kutokwa na Damu nyingi Siku ya kujifungua ivyo Mama yangu alifariki. Baada tu ya kujifungua mtoto ambaye ni mimi, bibi akanilea mpaka siku nilipokutana na mwanaume katili kama Wewe.

Mateso ni makali mpaka nakitamani kifo. Mume wangu Leo unasema Mimi mchafu ninanuka mithili ya mzoga, unaniita Mimi Malaya wa kutupwa! Jamani mume wangu Muogope Mungu wako, mateso nayoyapata hapa kitandani pasipo kuamka ndio umalaya au? nashukuru sana mume wangu,

Nimelalia upande mmoja tu wa ubavu wangu takribani mwaka mmoja hadi wadudu wadogo aina ya funza. Wameanza kutoka katika ubavu huo, yaani mume wangu Hata kunigeuza tu hutaki. Kwa kheri Mume wangu nakupenda sana ila ipo siku tutaonana utanieleza kwa nini uliamua kunitenda hivi. Nasema kwa heri Dunia acheni nikapumzike mbinguni kwa Baba pasipo na mateso kama Haya.

MWISHO.

Simulizi yetu Hii ya Bibi Milele Nitakulaumu Haina la Ziada Kwa Simulizi Nyingine Nzuri za Kuvutia na Kukufundisha Maisha Tembelea Africona.

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Barua Kwa Mpenzi

BARUA KWA MPENZI: SIMULIZI FUPI ZA MAPENZI

BINADAMU HATUNA UTU: SIMULIZI ZA MAISHA