in

HADITHI YA BWANA TAJIRI NA MASIKINI – SIMULIZI ZA KALE

Tazama Matokeo Hapa

Download Mitihani

Hadithi ya Bwana Tajiri na Masikini imehadithiwa na mzee Ngwali Mashaka. Soma hadi mwisho simulizi hii, nakuhakikishia hutojutia lazima itakufundisha kitu.

Hadithi - Bwana Tajiri na Masikini Africona

SIMULIZI ZA KALE: BWANA TAJIRI NA MASIKINI.

Hapo zamani za kale alikuwepo bwana mmoja aliyekuwa akiitwa Hassan Saira. Bwana huyo alikuwa ni tajiri sana kwa wakati wake.
Vile vile alikuwapo mtu mmoja katika kijiji hicho ambae ni masikini sana bwana huyo alikuwa akiitwa Bwana Vuai Pandu.
Bwana Hassan ni mtu mmoja wapo aliye Barikiwa uwezo mzuri na Mwenyezi Mungu. Bwana huyo alioa na akapata mtoto mmoja wa kiume aliyeitwa Maulid.

Mtoto wake huyo alikuwa ni mgonjwa, lakini moyo wake ulipenda amuozeshe na huenda ikawa bahati nzuri akapoa na kupata mtoto ambaye aliweza kumfaa babu yake. Bwana Hassan alikwenda kwa jirani yake Bwana Vuai Pandu ambaye alikuwa na watoto wengi wake na waume.

Bwana Hassan alikwenda kuposa katika nchi moja wapo ya kifalme na kumwambia mzee Vuai kuwa mtoto wangu nimemposea, lakini ni mgonjwa haifai kuonekana. Lakini nimekuja kwako unipe mtoto wako mmoja aitwae Yunus. Bwana Vuai alisema na kumwambia Bwana Hassan mimi mtoto wangu ni masikini jee atawezaji kufika kutoka nchi hizo za kifalme na akaonekane kuwa ni mtu?

Hassan alijibu kuwa ataonekana kuwa ni mtu, usijali. Bwana Vuai alimuelezea mkewe Bibi Khadija kadhia hiyo. Bi.Khadija alimwambia mumewe jee haitakuwa taabu baada ya kwishakuoana, kwa sababu kila mmoja atakuwa anampenda mwenziwe.?

Mzee Vuai alisema si tatizo nitamnasihi sana baada ya kurudi hapa tu kuwa amwache. Hapo alimwambia asili ya kukwambia hayo sisi hapa ni masikini tusipokubali anaweza hata kutufukuza, tutafanya nini.? Kwa hiyo ni bora tukubali.

Baada ya maneno hayo Bi Khadija aliridhika na Bwana Vuai alipeleka jawabu kwa Bwana Hassan Saira kuwa ameridhika kumpa mtoto wake. Na hapo ilifanywa safari, akasafi ri kwa meli, huku mtoto wa Bwana Vuai akapambwa na kuonekana ni mtoto wa mfalme. Pia askari walichukuliwa wakaenda kwenye harusi.

Mizinga ilisikika siku ile ya kupokewa bwana harusi na kukaribishwa wapite ndani ya kasri ya Mfalme. Gari nyingi za watu zilikuja katika sherehe hiyo na mtoto wa mfalme akachukuliwa na kufanyiwa kama ilivyo ada ya harusi na wafalme wote waliohudhuria walifurahi sana kwa kupata mchumba mzuri wa kifalme.

Baada ya hapo ilifanyika safari ya kurudi nyumbani ambapo alikabidhiwa watumishi mbali mbali, wa kike na wanaume. Mizinga ya harusi ya kurudi ilisikika na watu wote walikuja kumpokea harusi.
Shangwe na vigelegele vilizagaa mtaani kwa Bwana Hassan Saira. Na walipofi ka maharusi nyumbani kwao watu walikaa na kushereheka usiku wa kucha.

Ilipofi ka siku ya pili Bwana Vuai alikwenda kuomba kuonana na mwanawe Yunus. Yunus hakupinga amri ya mzee wake na hapo Yunus akamuaga mkewe kuwa anakwenda kuangalia bustani zake na alitoka nje kwa muda mchache na hatimayae mtoto wa mfalme akaletewa mume mwengine na kuambiwa huyu ndie mumeo.

Bi harusi alisema huyu siye mume wangu niletewe mume wangu na hapo alilia kwa muda mrefu na kilio kilizagaa katika nyumba mpaka watu wote wakatetemeka. Aliitwa Bwana Hassan na kuelezwa kuwa Bi harusi hataki lolote na anataka kurudi kwao au aletewe mume wake kwani aliyeletewa siye mumewe halisi.

Bwana Hassan alipofika mabibi wa nyumbani walimwambia utuletee mume wetu kwa haraka. Si hivyo tunakwenda zetu. Ikabidi Bwana Hassan kusema kuwa huyu ndiye mume wako lakini bibi harusi akasema aitwe baba yake mzazi. Bwana Hassan alipeleka barua ya ugonjwa ili kumrudisha kwao kwa sababu tu hataki kukaa na mume aliyekuwa siye aliyeozeshwa.

Mfalme alipopata barua na kufika kule nyumbani aliletewa mwanawe. Baada ya kuzungumza na watu wa nyumbani alihisi kuwa hana sifa ya ugonjwa. Hivyo bwana mfalme aliandika barua ya kumshitaki Bwana Hassan kwa kitendo alichokifanya ambacho si cha ukweli.

Bwana Hassan alishitakiwa na kutakiwa kulipa fidia kwa kitendo alichokifanya cha kuozeshwa mtu mgonjwa. Bwana Hassan alikubali na kulipa fedha pamoja na masharti yote aliyopewa.
Baada ya hapo mtoto wa mfalme alimwambia mzee wake kuwa alifanya hadaa tu kumletea mtu mzima na baadae kupewa mgonjwa, kwa hivyo mimi ninamtaka yule niliyeozeshwa mwanzo. Nina hakika bado kijana yule hajafa katika nchi ile, hivyo nikaozeshwe yule yule na niletewe mwenyewe.

Kwa kweli mfalme alisononeka sana kwa kitendo hicho kwa sababu mtoto wake alikuwa hali wala halali. Mfalme alitoa askari na kwenda kwa Bwana Hassan Saira na kumtaka apewe yule kijana aliyekuja kumuozesha mwanawe na wampeleke kule aliko mwana wa mfalme. Hapo Bwana Hassan alikwenda kwa Bwana Vuai na kumwambia kuwa mfalme amekuja na anamtaka yule kijana wako tumpelekee.

Lakini Bwana Vuai alimwambia Bwana Hassan kuwa mwambie mfalme aje mwenyewe na asitume askari. Baada ya hayo askari walipeleka ujumbe na mfalme akaja kutokana na shida ya mwanawe.

Mfalme baada ya kufika kwa Bwana Hassan, akapelekwa kwa Bwana Vuai Pandu. Bwana Vuai alitakiwa kumwita mtoto wake ili waende pamoja. Walipofika alisema; „nasikia umetuma ujumbe kuwa nije mwenyewe nisitumize mtu yeyote, kwa hivyo tayari nimekwishafika.”

Hapo Bwana Vuai alisema huyu ndie mtoto wangu alichukuliwa kwa hadaa ili kuozeshwa mtoto wako. “Jee wewe ukiangalia anastahiki kuchukuliwa kuja huko?” Unakuja kuchukua mtoto wangu, kutokana na umasikini tulio nao hebu twende ukaangalie nyumba yetu ilivyo tunavyoishi,” alisema.

Mfalme alikubali hayo yote na baada ya kufika aliona nyumba yao na alimwambia warudi tena kwa Bwana Hassan. Na baada ya kufika aliamrisha aletewe yule mtoto aliyekuwa mgonjwa, kwa kweli mfalme alisikitika sana baada ya kuona hali yake. Baadae mfalme alizungumza na Bwana Vuai juu ya shida iliyompata kutokana na mtoto wake,.

hivyo ninakiri umasikini wako na kwamba nitakujengea nyumba yako na nitakusaidia kama ipasavyo lakini mtoto wako amuoe mtoto wangu, kwa sababu ninaridhika vya kutosha. Na hapo Bwana Vuai alikubaliana na mfalme na wakaandikiana mkataba kuhusu hayo waliyoyazungumza.

Ilipofika siku ya sita mfalme alifika na zana zote, na kuanza shughuli za ujenzi. Na baada ya siku kidogo nyumba ilimalizika na kwenda kufunga ndoa. Hapo tena baada ya ndoa mtoto wa mfalme alipoa matatizo yake na hatimae mtoto wa Bwana Vuai alipewa mali nyingi sana na mfalme. unyonge pamoja na umasikini waliokuwa nao awali ukaondoka na akawa wakati wowote anaruhusiwa kwenda kuwaona wakwe zake.

MWISHO

Funzo la Msingi katika Hadithi Hii ni Kwamba Usimsaliti mtu aliyekusaidia, Pia tukumbuke fadhila.

Kwa upande wako umepata funzo gani katika Hadithi Hii? Niandikie hapo chini kwenye comment.

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

swahili Love Stories

SWAHILI LOVE STORIES: Simulizi za Kusisimua na Kuelimisha

SAMAKI MKUBWA - HADITHI

HADITHI YA SAMAKI MKUBWA : HADITHI ZA KUSISIMUA NA ELIMISHA