in

HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE: SIMULIZI ZA KALE AFRICONA

Tazama Matokeo Hapa

Download Mitihani

Hadithi ya Mfalme na Waziri wake imehadithiwa na Mzee Ali Rehani Ali, Soma hadi mwisho simulizi hii, huto amini alicho kifanya waziri huyu…

MFALME-NA-WAZIRI-WAKE-HADITHI

 

HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE

Hapo zamani za kale alikuwepo mfalme na waziri wake ambao walikuwa na tabia ya kwenda kusaka porini, siku tatu kwa kila mwezi. Siku moja waziri huyo wa mfalme alisafi ri na kwenda nchi za nje. Alipofika huko aliona upanga ambao unamfaa mfalme wake, kwani mpini wake ulikuwa wa dhahabu hivyo alimnunulia na aliporudi nchini kwake alimpa upanga ule mfalme wake kuwa ni zawadi.

Mfalme aliupokea na akawa anacheza na ule upanga, lakini upanga ule ulimkata kidole kimoja cha mkono wa kushoto hivyo mfalme alikasirika sana na alitwaa ule upanga na kumfunga gerezani waziri wake kwa mwaka moja.

Baada ya kupita kipindi fulani, mfalme ilimjia hamu ya kwenda kusaka na siku ile alikwenda peke yake kwani waziri wake alikuwa bado anatumikia kifungo gerezani. Alipofi ka porini alianza kusaka, lakini kule porini kulikuwa na watu wa mizimu, na watu hao waliambiwa na shetani wa mzimu ule kuwa, anataka mtu wa muhanga.

Kwa bahati mbaya miongoni mwa watu walikuwepo pale mzimuni wote walikuwa na ulemavu, yaani wana upungufu wa viungo katika miili yao. Hivyo punde wale watu waliokuwepo mzimuni walimkuta mtu mmoja walimvamia. Kumbe yule mtu alikuwa ni mfalme, walimfunga mikono na miguu ili awe ni muhanga kama walivyoagizwa mzimuni kwao.

Kabla hawajamuathiri mmoja wa watu wale waliomvamia mfalme yule, aliwakataza wenzake na kuwaambia; „Huyu hatufai kwani hana kidole chake kimoja cha kushoto.” Hivyo walimfungua, na kumpiga makofi kidogo kwa vile ameyafeli mambo ya watu na baadae walimwachia aende zake kwa vile ni
mlemavu wa kidole.

Mfalme alirudi nyumbani kwake na kuwaamuru askari wake, wamchukue yule waziri waliyemfunga gerezani na wamlete nyumbani kwake. Baada ya waziri kukutana na mfalme. Mfalme alimwambia waziri wake „Ah! Umeniokoa kweli kweli kwa kuniletea ule upanga mkali ulionikata kidole, la si hivyo, ningelikuwa nishakufa“.
Na waziri alimjibu mfalme wake kuwa „na mimi umenihifadhi kwani safari hiyo ilikuwa twende sote kusaka, na mimi mwili wangu hauna ulemavu wowote hivyo ningeuliwa“.

MWISHO

Kwenye Hadithi hii ya “MFALME NA WAZIRI WAKE” umejifunza kitu gani? ningependa kusikia kutoka kwako ya kwamba kunafunzo lolote umelipata hapa…

Niandikie hapo chini kwenye comment, nami nitakujibu. pia sio vibaya kama uta share simulizi hii kwa wengine nao wapate kujifunza na furahi…☺

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

HADITHI SUNGURA NA FISI - NANI ALIYE KULA MAZAO

HADITHI ZA SUNGURA NA FISI : “NANI ALIYE KULA MAZAO ?”

JOKA LENYE VICHWA SABA - HADITHI ZA KALE

JOKA LENYE VICHWA SABA: SIMULIZI YA KALE YA KUSISIMUA