in

Hadithi ya Subiri ni sali: Simulizi za Kale Zenye Mafunzo

SUBIRI NI SALI - HADITHI

Tazama Matokeo Hapa

Download Mitihani

Hadithi yetu hii ya kusisimua (Subiri ni sali) imehadithiwa na mzee Khalfan Mwita, Soma hadi mwisho simulizi hii nakuhakikishia huto jutia, lazima itakufundisha kitu.

SUBIRI NI SALI - HADITHI

SIMULIZI ZA KALE: HADITHI YA SUBIRI NI SALI.

Hapo zamani za kale alikuwepo mfanyabiashara ambaye aliheshimika kama mfalme wa mji. Alikuwa na wafanyakazi wa kila aina.

Siku moja alipokuwa akijiandaa kwenda nchi za ng’ambo kwa ajili ya shughuli za biashara aliwaita watoto wake saba na kuwaambia; „wanangu mimi ninasafiri nakwenda katika shughuli za kibiashara, lakini ninachotaka kwenu ninyi ni kuwa na tabia nzuri ambayo haitawaudhi watu wengine, muwe na heshima na kupendana.”

Hivyo kila mmoja alimpa kioo cha kujionea ambapo atakayekwenda kinyume na mambo aliyoyasema baba yao kioo chake kitafifia na hakitaonesha kitu.
Hapo mfanyabiashara yule alifunga safari na kuwaacha watoto wake pamoja na mama yao. Kawaida mfanyabiashara huyo anaposafiri huondoka na wafanyakazi wengine pamoja na makuhani yaani waganga wa kienyeji.

Lakini wale watoto walisahau, na wakaanza kwenda kinyume na mambo waliyoambiwa na baba yao. Kulikuwepo na watoto sita watundu na hawasikii wanayokatazwa na wakubwa zao, isipokuwa mdogo wao wa mwisho tu ndiye ambaye alikuwa mtiifu na alisikiliza na kufuata yale waliyoambiwa na baba yao. Kadiri siku zilivyoenda wale watoto wengine walizidi kuwa wakorofi na hatimae vioo vyao vilianza kufifia na vikawa havitoi taswira yoyote isipokuwa kile kioo cha mtoto wa mwisho ambaye yeye alikuwa mtiifu.

Baada ya muda kupita ililetwa taarifa kuwa baba yao anategemea kurudi. Walipopata taarifa zile watoto sita waliokuwa wakorofi waliingia hofu kwani waliambiwa atakaporudi baba yao atakaeonekana na kioo kilichofififa atakatwa kichwa. Hivyo walivyosikia habari za kurudi kwa baba yao waliogopa sana na wakawa wanamuonea kijicho mdogo wao, walimtenga, wakawa hawampendi na walimchukia sana.

Oh, siku ya kurudi kwa mfanyabiashara huyo iliwadia, na kama kawaida anaporudi hupigiwa mizinga kwa kumpa heshima na baada ya kupokea heshima hiyo alielekea kwenye vyumba vya watoto wake kuangalia vioo.

Hapo watoto wake sita walikuwa wanaogopa sana na mwisho walipanga mpango wa kukichukua kioo cha mdogo wao. Mipango yao ilifanikiwa kwa kukibadilisha na kumuekea kioo kilichoharibika.
Mara baba yao alianza kuvikagua vioo kwa kupitia katika kila chumba.

Alianza chumba cha mtoto wake wa kwanza na alipokiona kioo alifurahi sana na kumpongeza kwa tabia nzuri aliyo nayo. Alipokua akitoka walikirudisha kioo na kukiingiza katika chumba chengine alipoingia mfanyabiashara kwa mtoto mwengine naye alipongezwa kama alivyopongezwa yule wa mwanzo.

Walifanya tendo la kubadilisha kioo hadi chumba cha mtoto wa sita na mzee alifurahishwa sana kwa jinsi alivyoviona vioo vya watoto wake. Mambo yalibadilika alipoingia chumba cha saba ambacho ndio cha mwisho, kioo kilikuwa kimebanduka sana na mfanyabiashara alikasirika sana.

Ndipo alipowaita wafanyakazi na akawaamrisha wamchukue mtoto yule wampeleke msituni wakamchinje na baadae watie damu kwenye kifuu wamleletee kama ni ushahidi.
Wafanyakazi walitii amri ya mkuu wao na wakamchukua mtoto na kwenda naye msituni, lakini walipofika msituni walimuonea huruma kwa kuwa walimuona yule mtoto alikuwa mtiifu sana.

Hivyo walitafuta paa na kumchinja na kuchukua damu yake kwenye kifuu ili kumuonesha mfanyabiashara huyo na baadae walimtafutia chakula yule mtoto na kumjengea kibanda cha kujihifadhi. Hapo ndipo wakarudi na kumuonesha mfanyabiashara damu ndani ya kifuu na mfanya biashara aliridhika.

Mara alifunga safari nyengine na aliwaita watoto wake na kuwataka kila mmoja aagize zawadi anayoipenda. Kama kawaida alisafiri kwa kutumia meli na meli ile ilipofika katikati ya bahari ilikwama na ikawa haiwezi kwenda mbele wala kurudi nyuma. Na mfanyabiashara aliwaita makuhani ili wapige ramli.

Makuhani walipiga ramli na wakasema: „Wewe una watoto saba, lakini watoto sita umewaambia waagizie zawadi, mtoto mmoja hukumwambia, hivyo unatakiwa urudi ukamuulize ili safari yako iweze kuendelea.”

Mfanyabiashara alikasirika sana, lakini ilibidi arudi na akawauliza wafanyakazi kwa nini hawakumuua yule mtoto? Na ndipo akawaambia wafuatane na mkewe wakamuulize nini anataka haraka sana maana anachelewa safari yake.

Mama yule alifunga safari pamoja na wafanya kazi mpaka alipofi ka sehemu ambayo mtoto alikuwa anakaa, kwa bahati yule mtoto alikuwa anataka kusali akamwambia „Subiri ni Sali.” Mama alifahamu mwanawe anataka zawadi ya „subiri ni sali” na mama akarudi nyumbani na kumuelezea zawadi anayoitaka.

Mzee alisafi ri na baadae alinunua zawadi za watoto wake na kurejea nyumbani lakini alipokuwa katikati ya bahari meli ilikwama tena na wakaitwa makuhani ili kutabiri. Makuhani walisema: “wewe una watoto saba lakini umenunua zawadi za watoto sita na mmoja umemsahau, hivyo hutaweza kuendelea na safari yako mpaka uipate zawadi ya huyo mtoto.”

Mzee alianza kuhangaika kutafuta zawadi kila duka aliulizia „subiri ni sali” lakini hakuipata na alikuwa amechoka sana hadi siku moja alikuwa anapita chini ya nyumba moja akipiga kelele „subiri ni sali“. alitokea msichana mmoja na akampa ubawa na akamwambia auchome baada ya kusali na atapata „subiri ni sali”.

Mzee alichukua ubawa ule na akarudi nchini kwake na alipofi ka akamuagizia mkewe ampelekee zawadi yake na akamwambia achome kidogo tu atapata “subiri ni sali”. Mama akapeleka ubawa ule kwa mtoto na akamwambia afanye alichoagizwa, mtoto alishangaa.

Kwani yeye alimtaka mama asubiri amalize kusali. Lakini mtoto aliupokea ubawa ule na mama yake akarudi nyumbani.
Hivyo ilipofi ka jioni baada ya kumaliza kusali alichoma sehemu ndogo ya ubawa ule. Alitokea msichana mzuri ambae alikuwa wa ajabu. Oh! Alikuwa mzuri mno wa umbo na sura utatamani umuangalie jinsi alivyoumbika, matiti kama ncha ya msumari.

Msichana alimuuliza yule kijana; „kwa nini unakaa msituni peke yako?” Na yule mtoto alimuelezea mkasa uliompata mpaka akawa anaishi msituni. Baadae wakawa marafi ki, na kila jioni alichoma ubawa na yule msichana mzuri alitokea. Waliendelea hivyo hivyo mpaka wale ndugu zake sita walipajua alipokuwa
anakaa ndugu yao.

Siku moja walimuona yule msichana na walimuonea wivu na wakapanga njama za kutaka kumuua yule msichana. Hivyo walipokutana na mdogo wao walimwambia amuulize yule msichana; „akitaka kuuliwa kwa haraka afanye nini?” Yule mtoto alimuuliza na yule msichana alikasirika sana lakini kwa kuwa alikuwa anampenda sana alimwambia; „ukitaka kuniua kwa haraka nikikanyage kigae; mimi nitakufa kwa haraka.”

Siku ya pili yule mtoto aliwasimulia kaka zake. Siku moja alipokuwa akirudi katika shughuli zake alikuta vigae chini ya mlango, na yule mtoto alivikusanya na kuvitupa. Kumbe kilibakia kipande kidogo cha kigae chini ya mlango na alipokuja yule msichana akakikanyaga kigae kile na kikamkata.

Kwa huzuni yule msichana akamtaka achome ubawa ili apate kurudi nyumbani kwao. Masikini msichana mzuri alitoweka kwa huzuni na maumivu makali
aliyokuwa nayo.

Sasa yule mtoto kila akichoma ubawa, yule msichana akawa hatokei. Alichukuwa kipindi kirefu sana. Na mara alipata habari kuwa baba yake amefariki. Baada ya siku nyingi kupita, siku moja alifunga safari ya kwenda kumtafuta „subiri nisali”. Alichukua chakula na maji kwani alisafi ri kwa miguu na kuwa muda mrefu.

Baada ya machofu ya muda mrefu, alipofi ka mahali pamoja akaona mti na aliamua kwenda kupumzika kwa ajili ya kupata chakula na mara usingizi mzito ulimchukua. Alipozindukana alisikia sauti za ndege wa ajabu wanaongea. „Mtoto wa mfalme anaumwa lakini ukichukua majani ya mti huu, ukimpulizia atapona haraka sana.”

Hivyo kijana aliposikia vile aliinuka haraka sana na akatoa chakula chake chote na akatia majani. Alipofi ka mtaani aliona mabango yanasema binti mfalme anaumwa lakini atakaemtibu atamuoa na kama atashindwa atakatwa kichwa.

Yule mtoto alikwenda hadi kwenye kasri la mfalme na akajitangaza yeye anaweza kumtibu binti wa mfalme. Wafanyakazi walimuonesha vichwa vya watu waliokatwa, lakini yule mtoto alisema ataweza kumtibu.

Hivyo alichukuliwa hadi ndani ya nyumba ya mfalme na akafi kishwa kwa mfalme. Mfalme alimuita yaya ili ampeleke katika chumba cha „subiri nisali”.

Alipofi ka akatoa dawa yake akampulizia, mara „Subiri nisali” aliinuka kitandani alipolala na alipona na kila mmoja alishangaa kumuona „Subiri nisali” amepona.
Hapo „Subiri nisali” alifuatana na yule kijana hadi kwa baba yake. Mfalme alishangaa na alifurahi sana na akasema huyu ndie atakaekuoa. „Subiri nisali” alimwambia baba yake kuwa maradhi aliyoyapata yalisababishwa na huyo mtoto.

Mfalme alikasirika na akaamrisha auliwe lakini yule kijana alisema sio mimi niliyefanya kitendo hicho, ndugu zangu ndio waliofanya hivyo. Mfalme alitaka apelekwe waliko watoto hao na alipofi ka aliwakata vichwa wote sita na baadae ilifanywa arusi na mwisho akatawazwa kuwa mfalme. Wakaishi kwa raha mustarehe.

MWISHO

Umejifunza kitugani katika Hadithi ya Subiri ni Sali?, Kila wakati napenda kuuliza hivi kwa kuwa Lengo kubwa la hadithi ni kufundisha. Hivyo kama huja jifunza utakua umeburudika natumaini hivyo…

Niandikie hapo chini kwenye comment, nami nitakujibu.

Sio vibaya kama uta share simulizi hii kwa wengine nao wapate kujifunza na kufurahi…☺

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

NISAMEHE MWANANGU: SIMULIZI MPYA OCTOBER (2022)

NISAMEHE MWANANGU: SIMULIZI MPYA OCTOBER (2022)

Top 15 Richest People in Tanzania

Top 15 Richest Peoples in Tanzania: Matajiri wakubwa (2022)