in

HADITHI YA SAMAKI MKUBWA : HADITHI ZA KUSISIMUA NA ELIMISHA

Katika Hadithi yetu hii ya leo inayoitwa SAMAKI MKUBWA , imesimuliwa na mzee wetu kutoka Tanga anaye fahamika kwa jina la Akama Pandu Saleh, soma hadi mwisho kuna ujumbe mzuri sana. Katika Haadithi yetu Hii utafahamu ni kivipi mfalme alivyo kosa utajiri na Samaki Mkubwa.

SAMAKI MKUBWA - HADITHI

HADITHI YA SAMAKI MKUBWA

Hapo zamani za kale walikuwepo watu ambao walikuwa wanaishi karibu na pwani. Kazi yao ilikuwa kuvua, na siku zote walikuwa wanavua samaki wadogo wadogo. Siku moja alitokezea bwana mmoja akaenda baharini akabahatika kuvua samaki mkubwa sana.

Yeye mwenyewe akaanza kushangaa kumuona yule samaki mkubwa, na akaanza kusema ningempata samaki kama huyu ningetajirika. Kila siku tunakuja pwani tunapata samaki wadogo wadogo, hapo akajiuliza samaki huyu nimfanye nini?
Akaenda kumwita baba yake na baba mtu alipofika akaanza kushangaa na kusema samaki huyu mkubwa sijawahi kumuona, sasa wakaanza kushauriana.

Baba mtu akasema bora tukawaite jamaa waje kumtizama, wakaenda kuitwa wale jamaa walipofika na wao wakaanza kushangaa na kusema; „Samaki mkubwa, samaki kama huyu hatujawahi kumvua maisha yetu.” Na wao wakasema; „twendeni tukamwite sheha.” Na sheha alipokuja alishangaa na akasema; „Bora tukawamwite Mfalme aje kumuona.”

Alipokuja Mfalme na yeye alishangaa na kusema; „Bora tukamwite mzungu aje kumpiga picha.” Hapo waliondoka wakaenda kumchukua mzungu, na mzungu alipofika akasema; „Mngelimuweka kwa kule nikampiga picha lakini hapa anazunguuka nitampiga vipi?” Wale watu wakajibu mpige hivyo hivyo, na huku maji yanajaa na yule samaki akachukuliwa na maji, na kuenda zake baharini wakakosa utajiri pamoja na samaki.

MWISHO

Na huo ndio mwisho wa Hadithi ya samaki mkubwa, Natumai kunajambo utakua umejifunza kupitia Simulizi Hii ya kale yenye kusisimua na kuelimusha. hivyo usisite kutuandikia katika comment hapo chini ya kwamba umejifunza nini…?

Pia sio vibaya kama uta share Hadithi hii kwa wengine nao wapate kujifunza na kufurahi…

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Hadithi - Bwana Tajiri na Masikini Africona

HADITHI YA BWANA TAJIRI NA MASIKINI – SIMULIZI ZA KALE

WIZI MBAYA HADITHI FUPI

HADITHI YA WIZI MBAYA : HADITHI ZA KUSISIMUA NA KUFUNDISHA.