Tazama Matokeo Hapa
Download Mitihani
Shukurani za dhati ziende kwa bibi Zubeda Abdalla Omar, kwa kutusimulia hadithi ya WIZI MBAYA. Soma mpaka Mwisho utafahamu jinsi mke alivyo ponzwa na wizi wake, Pia kuna wimbo apo lazima utaupenda.
SIMULIZI ZA KALE: HADITHI YA WIZI MBAYA.
Hapo zamani za kale alikuwepo bwana mmoja, aliekuwa na wake watatu mmoja alikuwa mwizi. Yule bwana alikuwa anafuga mbuzi, siku moja kati ya wale wake zake mmoja aliiba mbuzi na kumchinja na kumpika bila ya yeye kujua. Aliporudi safari yake aliuliza nani alimchinja mbuzi? Wote walikataa.
Yule bwana akasema basi mimi nitafanya dawa. Wakajibu sawa, yule bwana akafanya mambo yake kisha akawapeleka mtoni. Walipofika aliwambia mmoja mmoja aanze kuingia mtoni na huku akiimba. Aliingia wa kwanza huku akiimba nyimbo:
Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Mani nenga Kachiri
Depala dipolo kachiri
Dipolo dabambo kachiriri
Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Alipomaliza kuimba akaibuka, kwani yeye hakuwa mwizi. Akafuata wa pili huku akiimba:
Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Mani nenga Kachiri
Depala dipolo kachiri
Dipolo dabambo kachiriri
Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Yeye pia akaibuka na kukaa pembeni. Akafuata yule wa tatu akaingia huku akiimba:
Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Mani nenga Kachiri
Depala dipolo kachiri
Dipolo dabambo kachiriri
Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Lakini yeye alizama.
Kuona vile yule bwana akajua kwamba yule mke wa tatu ndie mwizi. Hapo akafanya dawa zake na yule bibi akaibuka, alimuomba radhi mumewe na kuahidi kuwa hatorudia tena kosa lake. Na yule bwana alikubali na wakaendelea kuishi kwa raha mustarehe.
MWISHO
Kwenye Hadithi hii umejifunza kitu gani? mimi binafsi nimejifunza tusiwe waongo na pia tusiwe Wadokozi (Wizi ni Mbaya).
Pia nimejifunza wimbo “Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Bill nenga Kachiri
Depala dipolo kachiri
Dipolo dabambo kachiriri
Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.” 😉😂,, Nipo serious ila sio kila wakati…
Niandikie hapo chini kwenye comment, kitu chochote ulicho jifunza kwenye Hadithi hii.
Pia sio vibaya kama uta share simulizi hii kwa wengine nao wapate kujifunza na furahi.
- 211shares
- Facebook128
- Twitter83
- Gmail
- Copy Link