in

HADITHI ZA KALE: MUME WA AJABU – SIMULIZI YA KUSISIMUA

Tazama Matokeo Hapa

Download Mitihani

Hadithi hii Fupi ya Kale Mume wa Ajabu, imesimuliwa na mzee Farasha Saidi Kombo, Soma hadi mwisho simulizi hii hadi mwisho utajionea maajabu ya kimbunga. Pia ukimaliza Hadidhi Hii Kuna Hadithi za Kale Nyingine nyingi Katika Website Hii Usikose.

MUME WA AJABU - HADITHI

HADITHI ZA KALE: MUME WA AJABU.

Hapo zamani za kale alikuwepo mzee Subira na mzee Pandu, wote walikuwa marafiki na walikuwa majirani. Mzee Pandu alikuwa anakawaida ya kusikitika. Siku moja mzee Pandu alioteshwa aende porini yeye na rafiki yake Mzee Subira wakachukuwe mapesa.

Kwa bahati Mzee Subira alikuwa na punda, mzee Pandu alienda kumchukua yule punda na kumvalisha
soji bila ya yeye mwenyewe kumwambia. Alimchukua punda yule wakaenda porini kule alikofahamishwa. Alipofika huko aliyakuta mapesa mengi na mali za kila aina.

Alizipakia mali zote zile alizozikuta na kumbebesha yule punda. Kwa bahati mbaya ukavuma upepo, ukamchukua mzee Pandu. Punda alipoona vile alifuata njia na kuelekea kwao, alifuata njia mpaka kafika kwao, alifika kwao pamoja na ule mzigo aliobebeshwa, alipofika akaanza kulia kwa kelele kubwa; Gha!
Gha! Gha! Gha! Gha! Gha! mpaka mzee Subira akaamka, na alipotoka nje alimuona punda kaja na mzigo wa mapesa.

Mzee huyo alishangaa kuona punda kavalishwa soji na kubebeshwa mzigo. Aliuchukua ule mzigo na kuutia ndani na punda akamuweka pahala pake pa kawaida. Ilipofika asubuhi akaenda kumuamsha jirani
yake ambaye hakuwemo ndani ya nyumba.

Hayumo!!! alishangaa sana kuona asubuhi ile mzee Pandu hayumo ndani mwake. Akaanza kujiuliza huyu bwana kaenda wapi? Kuona hivyo, aliwaelezea wenzake kwamba mzee Pandu haonekani, alianza kufanya ramli na dawa za miti shamba pamoja na majini ili ajuwe aliko.

Mwisho wake alijua kwamba alichukuliwa na upepo mkubwa baada ya kufanya dawa .

MWISHO

Kwenye Hadithi hii umejifunza kitu gani? ningependa kusikia kutoka kwako ya kwamba kunafunzo lolote umelipata katika Simulizi hii. Hadithi za kale

Niandikie hapo chini kwenye comment, nami nitakujibu. pia sio vibaya kama uta share simulizi hii kwa wengine nao wapate kujifunza na furahi na Hizi Hadithi za Kale…☺

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

JOKA LENYE VICHWA SABA - HADITHI ZA KALE

JOKA LENYE VICHWA SABA: SIMULIZI YA KALE YA KUSISIMUA

MTOTO WA MAKAME WA MAKAME - HADITHI

MTOTO WA MAKAME WA MAKAME: SIMULIZI ZA KALE ZA KUSISIMUA.