in

HII KITAALAMU TUNAITAJE?: Maana Nimebaki Sielewi 🤨.

Tazama Matokeo Hapa

Download Mitihani

Hii Kitaalamu Tunaitaje, maana Nimebaki Sielewi. Wajumbe Wenzangu embu tuthaidiane Kwenye hili. Soma Mpaka mwisho.

Usisahau kuni Follow @japhary kwa Vichekesho na Mada Mbalimbali za Kuvutia. 😊

KICHEKESHO - HII KITAALAMU TUNAITAJE

KICHEKESHO: HII KITAALAMU TUNAITAJE..?

Kisa Chutu Kinaanzia Maeneo ya Ofisini. Bosi mmoja Alikuwa anazungumza na Mfanyakazi Wake. Soma Mpaka Mwisho…

BOSI: Wiki hii tutaenda wote Serena Hotel kwenye mkutano fanya mipango yote. Secretary anaitikia na Kuamua kumpigia Simu Mume Wake.

SEKRETARI: Mume Wangu Tunaenda na bosi Serena hotel kwenye mkutano for 1 week.

MUME: (anampigia Mchepuko Wake). Mambo safi, wife anaenda kikazi Serena, jitayarishe tujipe raha for 1 week.

MCHEPUKO: (Anamwambia mwanafunzi wake wa tution) wiki hii nina kazi fulani hakuna tution mpaka week ijayo.

MWANAFUNZI: (anampigia simu sugar daddy wake) ambaye ndo (BOSI). Dear hakuna tution wiki hii nakuja kwako…

BOSI: (anamwambia sekretari wake) Siendi Serena tena coz mjukuu wangu atanitembelea.

SEKRETARI: Mume wangu hatuendi Serena tena Bosi amepata Dharura.

MUME: (anampigia Mchepuko) dah..! mpenzi, huyu mke wangu haendi tena. Shit..! So hadi next time please.

MCHEPUKO: (anampigia mwanafunzi) Darasa kama kawaida, sorry for the earlier message.

MWANAFUNZI: (Mwanafunzi anampigia Sugar Dady) Darling Tution inaendelea kumbe, so nakuja wiki ijayo.!

BOSI: Sekretari sorry jitayarishe ile safari ya Serena iko palepale…


Mimi kiukweli nimebaki Njia Panda hapa Kwenye Hichi kisa. Yaani naona Kabisa Hapa Kimeumana tena Sio kidogo. Nawaza hapa Secretary nae atamshtua Mumewe, mume na ata mshtua mchepuko, mchepuko atatoa tena ruhusa kwa Mwanafunza, Hahaha 😂.

Niandikie Hapo Chini Kwenye Comment Kuhusu ichi kisa. Hii Kitaalamu Tunaitaje maana hii ni “Loop” Tena Infinity.

(Loop ni Kitu Kinacho Jirudia Rudia, Infinity Loop ni Kitu kinacho jirudia Pasipo kuwa na Mwisho.)

Nijulishe Hapo Chini Kwenye Comment ungependa Vituko kama Hivi, au Kwenye Hivi Vichekesho tuongeze Kipi Tu Punguze Kipi. Nawatakia Tabasamu lenye furaha 😊😊.

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

VICHEKESHO - HUYU JAMAA NI MBUMBUMBU

Huyu Jamaa Ni Mbumbumbu wa Mwisho: VICHEKESHO.

VITUKO - HAYA MATAMBO TUACHE

LITAKUJA KUFA JITU: Haya Matambo Ifike Mahali Tuache