in

Huyu Jamaa Ni Mbumbumbu wa Mwisho: VICHEKESHO.

Tazama Matokeo Hapa

Download Mitihani

Huyu Jamaa ni Mbumbumbu wa Mwisho Kweli. Vichekesho Vunja mbavu lazima uta Cheka tu. Kwani jamaa Mwenyewe anasemaje..? Hebu tumsikilize.

Usisahau kuni Follow @japhary kwa Vichekesho na Mada Mbalimbali za Kuvutia. 😊

VICHEKESHO - HUYU JAMAA NI MBUMBUMBU

VICHEKESHO – HUYU JAMAA NI MBUMBUMBU

Unataka kujua alicho kifanya huyu jamaa..? Soma mpaka Mwisho.

RAJABU: Vipi mbona leo huna uchangamfu.
JUMA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje kunamambo atakuficha tu.
RAJABU: Nini tena ndugu yangu..? Mbona shemeji mtu fresh sana.
JUMA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri ananificha.
RAJABU: Nini tena..?
JUMA: Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia.
RAJABU: Kitimoto..! We umejuaje..?
JUMA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kutoka kitandani, simu ya Wife siikaita, nikaamua kuipokea. kabla hata sijajibu Chochote, nikasikia sauti ya Msela mmoja akiuliza, “Huyo nguruwe amesha Ondoka..?”
Hebu we fikiria, kumbe Wife Anasafirisha Nguruwe Kisirisiri Hata Kuniambia. mambo gani haya Rajabu. Baada ya Kusikiliza icho kisa, Rajabu kamuambia “Ndugu Fanya Namna Umuongezee Mtaji.”

Huo Ushauri Wa Rajabu kwa jamaa yake unafaa..? Au Ndo Bure Kabisa. maana Sio Kwa Utopolo Huo…

Nawatakia Siku njema 😊😊. Na Kwa wale tunao lala kesho nawatakia “Usiku Mwema“.

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

MCHUNGAJI NA MLEVI KIMEUMANA - VICHEKESHO

MCHUNGAJI NA MLEVI KIMEUMANA: CHEKA TU

KICHEKESHO - HII KITAALAMU TUNAITAJE

HII KITAALAMU TUNAITAJE?: Maana Nimebaki Sielewi 🤨.