in

I Will Be Back: Simulizi za Kusisimua na Kufundisha

Tazama Matokeo Hapa

Download Mitihani

Aisha mapepe Ndani ya Ubora Wangu nimerudi tena Kwenye Chama la Wana Africona Kukupa Burudani ya Simulizi. Leo Simulizi yetu Imekaa kishua ila Hakuna Kilicho Aribika Karibuni. I Will Be Back Simulizi za Kusisimua na Kufundisha.

I Will Be Back

SIMULIZI ZA KUSISIMUA NA KUFUNDISHA: I WILL BE BACK

Sehemu Ya Kwanza (1).

Ilikua ni afrajili tulivu sana ya siku ya Jumatatu, wakati mawingu mazito yalipoonekana kutanda karibu kila sehemu huku mvua za rasha rasha zilizokua zikisindikizwa na baridi kali zikimfanya kila mtu aliyekuwepo eneo lile awe ndani ya koti zito.

Makoti, kofia pamoja na skafu nzito vinaonekana kuifaidi miili ya watu wengi waliokuwepo eneo lile huku uwingi wa miamvuli iliyokua imetapakaa karibu mkononi kwa kila mtu ikionekana kuongeza giza la afrajili ile.

Ngurumo za radi zilizokua zikisikika kutoka kila sehemu zilioonekana kuzimeza sauti za watembea kwa miguu huku sauti za honi na ngurumo za magari vikionekana kusikika kwa mbali sana.
Licha ya hali ya hewa kuonekana kuwa mbaya lakini uwimgi wa watu nchini China uliifanya barabara kuu ya mji wa Chang chun uliokua kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Beijing ionekane kuelemewa na uwingi wa watu ambao kwa asilimia kubwa walikua wakitegemea usafiri wa treni ziendazo kasi kwa kutumia umeme.

Ilikua ni saa 10 afrajili kwa saa za china wakati ambao na mimi nilionekana kuwa miongoni mwa wale watembea kwa miguu waliokua wakitegemea sana usafiri wa treni ziendazo kasi kwa kutumia umeme.

Ilikua ni Wuhan sehemu ilipokuwepo station kubwa ya treni ziendazo kasi kwa kutumia umeme katika mji ule wa Chang chun uliokua kaskazini ya Beijing mji mkuu wa China

Hali ya hewa ya mvua na ubaridi ilimfanya kila mtu aliyekuwepo pale Wuhan alisubirie treni lililokua limeenda mji wa Harbin uliokua karibu na mpaka wa nchi ya China na Urusi kwa hamu kubwa sana huku wengi wao wakionekana kuifunua mikono yao na kuzitazama saa zao mara kwa mara.

Umbali wa kutaka mji wa Chang chun na Harbin ulikua ni karibu saa 1 na robo kwa usafiri wa zile treni ziendazo kasi imaana kwa waliokua wakitumia usafiri tofauti na treni zile ziendazo kasi walikua wakitumia zaidi ya masaa matano mpaka sita kufika Harbin.

Hivyo ilinibidi na mimi nisubiri treni pale Wuhan sehemu nilipoianza safari yangu ndefu ya kurudi nyumbani nchini Tanzania mara tu baada ya kua nimemaliza masomo yangu ya biashara niliyoyasoma kwa muda wa miaka minne katika chuo cha Chang Jiang kilichopo katikati ya mji wa Chang chun mji uliokua na zaidi ya wakazi wapatao milioni mbili.

Wakati niliokua nikilisubiria treni masikioni kwangu spika za hearphone zilionekana kudunda sana huku wimbo P diddy I’m coming home ukionekana kuniburudisha sana kiasi cha kufanya fikra zangu zote zirejee nchini Tanzania huku picha na kumbukumbu za matukio mbalimbali yaliyotukia nchini Tanzania yakianza kukatiza kichwani kwangu.

Nilijikuta nikiurudia rudia wimbo huu mara kwa mara huku nikiwakumbuka ndugu pamoja na mke wangu Tressy kiukweli kila nilipozidi kuwaza jinsi mke wangu atakavyokuja pamoja na wazazi wangu kunipokea uwanja wa ndege nilizidi kupata mshawasha kiasi cha kufanya nione kama treni lililokua mji wa Harbin likichelewa kuja.

Nilijikuta nikiitazama saa yangu ilikua ni saa 11 kasorobo afrajili kwa saa za China kiukweli niliuona muda kana kwamba ulikua hauendi niliutazama mshale wa dakika na kuona kana kwamba ulikua ukizunguka kurudi nyuma nilitamani niusogeze walau dakika tano mbele lakini niligundua kua ningekua najidanganya mwenyewe.

Kiukweli hakuna kitu kilichokua kikijirudia kichwani kwangu mara kwa mara kama taswira ya mke wangu nilijikuta nikiona kana kwamba sura ya mke wangu Tressy ilikua ikikatisha mbele ya macho yangu huku nikiona kama sauti ya mtoto wetu niliemuacha akiwa na umri wa miezi sita ikiniita baba nadhani kama isingekua sauti za watu kuanza kujisogeza mbele kuelekea sehemu linaposimama treni basi ningechanganyikiwa kwa kumuwaza mke wangu pamoja na mtoto wetu niliyemuacha angali bado kichanga.

Basi baada ya kuacha kumuwaza Tressy niliitazama saa yangu ya mkononi huku na mimi nikijisogeza karibu na sehemu linaposimama treni ilikua ni saa kumi na 11 na dakika 5 kwa muda wa nchini China hii iliashiria kuwa muda si mrefu treni lingeingia kutokea kule mji wa Harbin kwani kikawaida mara nyingi treni lilikua likifika kati ya 11 na dakika 20 afrajili kwa muda wa kule nchini China.

Baada ya kusogea karibu na sehemu linaposimama treni nilihakikisha kama mizigo yangu pamoja na kila nilichonacho kama kipo sawa na baada ya kuridhika kua hakukuwa na tatizo lolote yaani kila kitu kilikua sawa nilikaa kwenye benchi la chuma lililokua limepakwa rangi nyeusi huku likionekana kupambwa kwa kuzungushiwa bustani za maua ya kila aina na kuanza kuzisuburia izo dakika chache zilizokua zimebaki ili treni liwasili.

Saa kumi na 11 na dakika 20 ilifika bila treni kuwasili wala kuwa na dalili yoyote ya treni kuwasili wote tuliokua pale station ya Wuhan tulionekana kushangazwa sana kwani haikua kawaida kabisa treni kutowasili ndani ya wakati nilimuona karibu kila mtu akiitazama saa yake na kuanza kuongea maneno ambayo mengine niliyaelewa na mengine sikua nikiyaelewa lakini hakukua na jinsi zaidi ya kuendelea kusubiri.

Turisubiri sana mwishowe wale waliokua wamesogea mbele zaidi ya sehemu linaposimama treni walianza kurudi nyuma huku mivuke kama moshi iliyosababishwa na baridi ikionekana kutoka midomoni mwao kwa sababu ya kuongea kwao kwa hasira.

Kuchelewa kwa treni kulifanya nigundue kua huenda ningechelewa kufika Beijing mji mkuu wa China na hivyo huenda ningekosa tiketi ya ndege zilizokua zikiondoka usiku wa siku hiyo ya Jumatatu hivyo huenda ingenilazimu nitafute hoteli ya kulala pale Beijing mpaka siku ya jumanne ili nitafute tiketi ya kuondoka usiku huo wa Jumanne.

kadiri nilivozidi kugundua ukweli huo wa kuumiza kam huenda ungetokea nilizidi kuumia na kuona kana kwamba nachelewa kurudi nyumbani kuwaona ndugu na mke wangu Tressy pamoja na kitoto chetu kichanga nilichokiacha kikiwa na umri wa miezi sita.

Kadri muda ulivyozidi kwenda pasipo ya treni kuwasili ndipo hofu yangu ya kukosa tiketi ya ndege ilivyozidi kuongezeka nilijikuta nikiitazama saa yangu mara kwa mara huku nikijaribu kuyazuia machozi yaliyokua yameanza kunitoka kwa sababu ya ukweli wa kuumiza niliokua nimeugundua kuwa sasa kwa zaidi ya asilimia hamsini nilikua nimekwisha chelewa tiketi za ndege za kurudi nyumbani usiku huo wa Jumatatu.

Ghaflaa!! Nikiwa mawazoni nilishtuka kusikia sauti ya breki ya treni ziendazo kasi ikisikika mita chache mbele yangu kutoka nilipokua nimekaa.

Kiukweli sikuyaamini macho yangu kama kweli lilichosimama mbele yangu lilikua ni treni nakumbuka ilikua ni saa 12 ya afrajili kwa saa za China ndio muda ambao treni liliwasili tena bila kuchelewa watu wote tuliokuwapo hapo Wuhan tukaanza kuingia ndani kwa ajili ya kuianza safari yetu kwenda katika jiji la Beijing.

Wakati watu wote tuliokua pale station ya Wuhan tukianza kuingia ndani ya treni sauti ya kike iliyokua ikiongea kwa lugha ya kingereza ilianza kusikika kutoka kwenye spika kubwa za plastic zilizokua ndani ya treni hilo treni lililoonekana kuwa safi kupita kawaida huku kila kitu kikionekana kupangwa katika mpangilio mzuri wa kuvutia sana.

‘’Sorry for coming late it was out of our control the weather was too bad in Harbin’’
(Samahani kwa kuchelewa ilikua nje ya uwezo wetu hali ya hewa ilikua mbaya sana Harbin)

Sauti ile ilizidi kusikika huku ikirudia kuongea mara mbili mbili na kisha ikanyamaza.
Basi mara baada ya kila mtu kua ameingia ndani ya treni na ile sauti kunyamaza safari yetu ya kuelekea jijini Beijing ilianza huku nikiwa sina matumaini yoyote ya kwenda kupata tiketi za ndege zinazoondoka usiku huo.

Ilikua ni saa 12 na dakika 10 afrajili wakati tulipokua tunaianza safari yetu ndefu ya kuelekea jijini Beijing mji mkuu wa nchi hiyo ya China
Ilikua ni safari ndefu sana ya zaidi ya masaa 9 mpaka kufika Beijing kutokea ule mji wa Chang chun uliokuwepo upande wa kaskazini ya mji mkuu wa china ambao ni Beijing.

Muda wote ambao safari ilikua imeanza nilikua nimekiinamisha kichwa changu kwenye kioo cha dirisha huku nikitazama upande wa nje jinsi miti, majumba pamoja na watu walivyoonekana kurudi nyuma haraka haraka kwa sababu ya mwendo kasi wa treni.

Kwaheri China!! Nilijikuta nikijisemea huku nikiukumbuka wema wa watu wa China taswira na picha za baadhi ya rafiki zangu wa China niliosoma nao chuo zikaanza kujirudia rudia kichwani kwangu Ghaflaa nikaanza kuzikumbuka baadhi ya nyakati za furaha nilizokua nazo mimi pamoja na rafiki zangu wa kichina nilikutana nao pale chuoni Chang Jian

Nilijikuta nikiwakumbuka rafiki zangu vipenzi Chang ging, Guiyang, Xi’an yuan, pamoja na Lee chun lee chong ambao mara kwa mara walikua wakinifundisha na kufanya nianze kuupenda mchezo wa mapigano maarufu kama Kung Fu.

Kwaheri Chang ging, kwaheri Guiyang kwaheri Xi’an yuan pamoja Lee chun lee chong nilijikuta nikisema huku nikitengeneza tabasamu bandia usoni mwangu kw ajili ya kuizuia huzuni iliyokua imeanza kuzishambulia fikra zangu.

Kwa heri rafiki zangu kwa heri China hakika milele mtakua moyoni mwangu nilisema huku nikipitisha leso machoni kwangu na kuyafuta machozi ya huzuni yaliyokua yakinitoka.

Safari iliendelea huku ukimya mkubwa ukionekana kutawala mle ndani ya treni niliyaangaza macho yangu huku na kule nikaona karibu kila mtu alikua amesinzia isipokua baadhi ya watu wachache ambao walionekana kua bize wakijisomea vitabu vyao.

Tulikua bado ndani ya mji wa Chan chun wakati na mimi nilipopitiwa na usingizi kama baadhi ya watu wengine wengi waliokua wakisinzia.

Nilijikuta nikisinzia huku ndoto za vihelehele. Zikipokezana kutoka na kuingia kichwani kwangu
Nilijikuta nikimuota mke wangu Tressy huku nikiuona uzuri wake ulioonekana kuongezeka mara mbili zaidi ya nilivyokua nimemuacha

Nilijikuta nikiuona uso mwembamba wa Tressy uliokua umepambwa na ngozi laini nyeupe ukizidi kuvutia huku macho yake makubwa meupe mazuri ya duara yakizidi kung’aa sana na kufanya yawe ya kupendeza

Pua zake nyembamba zilionekana kuupamba sana uso wake huku midomo yake mizuri miekundu ikionekana kua kivutio kikubwa sana usoni mwake wakati nywele zake ndefu nyeusi alizozilaza kwa nyuma zikimfanya Tressy afanane sana na mwanadada mashuhuri kutoka nchi za Columbia aitwaye maarufu kama Maria clara.

Nilijikuta nikiendelea kusinzia huku ndoto zangu za vihelehele pamoja na mawazo yangu yote yakiwa juu ya mke wangu Tressy pamoja na kitoto chetu nilichokiacha na umri wa miezi sita ambao sikua nimeonana nao kwa takribani miaka minne iliyopita.

Ilikua ni saa 2 na nusu asubuhi kwa saa za China wakati treni iliposimama katika mji wa Shenyang na kufanya watu wote tuliokua tumesinzia tuamke.

Shenyang ulikua ni mji wa kwanza kuingia mara baada ya kutoka mji wa Chang chun na ulikua na wakazi wapatao milioni 1 na nusu mji huu ulikua mdogo kuliko mji wa Chang chun.
Basi baada ya watu wa pale Shenyang kuingia ndani ya treni safari yetu ilianza tena huku yikiwa yamebaki masaa kama 7 ili kuimaliza safari yetu ya kuelekea jijini Beijing.

Tulikua Shenyang hivyo tulibakiza miji minne ndipo tufike jijini Beijing tulikua tumebakiza mji wa Tianjin, Shijiazhuang, Lanzhou na Talyuan ndipo tuweze kuwasili ndani ya jiji la Beijing.
Safari iliendelea huku ukimya ukizidi kutawala tena kama ilivyokua hapo awali lakini safari hii ulionekana kuzidi zaidi kwani hata baadhi ya watu wachache waliokua wakijisomea vitabu vyao nao walionekana wakianza kusinzia.

Namimi nilikua miongoni mwa watu wengi waliosinzia kwa mara nyingine tena huku ndoto za asubuhi asubuhi zikionekana kukifaidi kichwa changu sikuelewa tena ni kitu gani kilichokua kikiendelea mpaka nilipokuja kushtuka kutoka usingizini wakati tulipofika katika mji wa Tianjin ambapo treni ilisimama.

Ilikuwa ni karibu saa 5 na nusu kwa asubuhi ambapo baadhi ya watu wachache wakionekana kuaga rafiki zao walioketi nao siti moja na kuteremka huku wengine wakipanda kwa ajili ya kuinza safari yao ya kueleke miji ya mbele.

Hivyo ndivyo ilivyokua kila tulipofika kituo treni ilikua ikisimama huku watu wengine wakishuka na wengine wakipanda na kisha safari kuendelea tena

Ukimya ulionekana kutawala sana kila mara wakati ambapo treni lilikua likiianza kuondoka namimi kwa mara nyingine tena nilionekana kuunga mkono ukimya ule kwani kila mara wakati treni likiondoka nilikua napitiwa na usingizi na kuzinduka pindi ambapo treni limesimama.

Tulifika mji Shijazhuang tukitokea mji wa Tianjin ilikua ni saa 7 mchana wakati treni iliposimama huku baahi ya watu wakishuka na wengine wakiingia kisha safari ikaendelea kama kawaida ukimya ukatawala tena huku na mimi mwenyewe.

Nikasinzia nikaja kushtuka tena pindi treni iliposimama katika mji wa Lanzhou na kufanya tubakize mji mmoja wa Talyuan ndipo tufike jiji la Beijing.
Safari iliendelea tena huku karibu kila mtu akiwa anasinzia akuna aliekua anajua nini kinachoendelea mpaka pale tulipokuja kughutuka tena kutoka usingizini

Ilikua ni saa 9 kasorobo wakati watu wengi tulipoghutuka kutoka usingizini mara tu baada ya treni kusimama hakuna aliyeamini kwani tayari tulikua ndani ya mji wa Talyuan na hivyo kufanya tubakize muda wa kama dakika 45 ama 50 ili tufike ndani ya jiji la Beijing.

Safari iliendelea kama kawaida huku wakati huu hakuna mtu aliyeonekana kulala ama kusinzia tena kwani muda uliokua umebaki haukuonekana kua mrefu machoni kwa watu wengi.

Sauti za maongezi zilianza kusikika ndani ya treni huku baadhi ya watu nikiwemo na mimi tukizivaa hearphone zetu masikioni na kuanza kusikiliza muziki kutoka kwenye simu zetu nilikua nikisikiliza wimbo uitwao Read all about it wa mwanadada mashuhuri aitwae. Emilie Sande niliusikiliza kwa makini huku nikimuomba Mungu anisaidie niweze kupata tiketi ya ndege yoyote abayo ilikua ikiondoka usiku huo.

Kama ilivyotegemewa kufika jijini Beijing ndani ya dakika 45 ama 50 ndivyo ilivyokua imetokea kwani tulitumia zaidi ya dakika 47 mpaka kufika jiji la Beijing ndipo treni liliposimama ndani ya moja ya station maarufu na mashuhuri sana duniani ilikua ni station ya Nanchang moja kati ya station maarufu sana nchini China nadhani ndio iliyokua ikiongoza kwa ubora na uzuri kuliko station zote za nchini humo.

Basi baada ya treni kusimama katika ile station ya Nanchang kila mtu alishuka na baadhi ya abiria wakionekana kupokelewa kwa furaha na ndugu zao huku uwingi wa watu ukionekana kulijaza na kulielemea sana jiji hilo la Beijing.

Watu walikua ni wengi sana katika lile jiji la Beijing pengine kuliko katika miji yoyote ya hapo China uwingi wa watu huo ulionekana kuleta joto sana joto lililofanya asilimia kubwa ya watu waonekana kuvaa vinguo vyepesi vyepesi.

Basi baada ya kushuka kwenye treni sikutaka kupoteza muda niliibeba mizigo yangu kisha nikajipenyeza katikati ya ule uwingi wa watu na kuanza kuisogelea barabara kubwa ya lami iliyokua imejengwa kwa ustadi mkubwa sana kiukweli ilikua ni barabara nzuri sana ya kuvutia ambayo sijawahi kuiona katika mji wowote nchini mwetu Tanzania.

Baada ya kuifikia ile barabara nilikwenda moja kwa moja mpaka kwenye kijibustani kizuri cha maua ya kila aina kilichokua kimezungushiwa viti vizuri vya chuma vulivyopigwa nakshi kwa rangi ya dhahabu.

Ilikua ni kituo cha mabasi pamoja na tax basi mara baada ya kufika pale bustanini niliketi kwenye moja ya vile viti vizuri vyenye rangi ya dhahabu na nikaanza kusubiria tax
Haikupita hata dakika 5 tax yenye rangi ya njano ikasimama mita chache mbele yangu niliisogelea kisha nikapakiza mizigo yangu na kuingia ndani

“Hii old man, please drive me to Beijing airport’’
(Habari mzee naomba nipeleke airport ya Beijing)
Nilimwambia yule dereva mzee mara tu baada ya kuingia ya lile tax.
“Ok son, its 50 dollars only”
(Sawa,mwanangu ni dollar 50 tu, dollar 50 ni karibu na sh. elfu 80 za Tz)

Yule mzee aliniambia huku akiawasha gari na kuanza kuondoka
Tulikua tunaelekea mtaa wa Nanning uliopo katikati ya jiji la Beijing huko ndipo sehemu ilipokuwepo airport ya jiji la Beijing
Ulikua ni kama mwendo wa dakika 20 ama nusu saa inategemea na uwingi wa watumiaji wa barabara kwa siku hiyo.

Uwingi wa watu ulimfanya dereva aendeshe polepole na kwa umakini sana na mimi niliutumia muda huo kuliangalia jiji la Beijing kwa mara ya mwisho huku nikiwatazama wakazi wake niliwatazama wazee walioonekana kubarikiwa kuishi miaka mingi huku mvi zikionekana kuzitawala nywele zao, kisha niliwatazama wanaume jinsi walivyobarikiwa nguvu.

Ubabe wa kung fu pamoja na akili na maarifa ya kujenga barabara na madaraja alafu macho yangu yakatua juu ya wanawake wao yakaufaidi uzuri wa sura zao zilizobarikiwa kwa macho madogo lakini meupe mazuri ya kuvutia pamoja na ngozi zao laini za rangi nyeupe.

Baada ya kuwatazama wanawake hao wazuri wa kichina macho yangu yalitua tena juu ya majengo makubwa mazuri ya kupendeza yaliyoonekana kuipamba sana Beijing.

Niliikuta nikijisemea tena kimoyomoyo kwa heri China kwa heri Chang chun pia kwa heri Beijing hakika sitowsahau kila mara mtakua moyoni mwangu nilijikuta nikizidi kusema kana kwamba ile miji ilikua ikinisikia na kunielewa.

Basi katika kuendelea kulishangaa kwa mara ya mwisho jiji la Beijing na wakazi wake ghafla nilishtuka kuona yule dereva mzee amesimamisha gari
Ooh kumbe tayari tulikua tumesha fika pale Nanning ilipokua Airport ya jiji la Beijing
Bila kuchelewa nilishuka nikashusha mizigo yangu na kumkabidhi yule dereva mzee hela yake.

“Thanks old man have a goodluck’’
(Asante mzee kila la heri) nilimwambia yule dereva mzee huku nikihesabu
noti za dollar 50 na kumkabidhi .
“Thanks too son,have a nice journey and welcome again China”
(Asante pia mwanangu,uwe na safari njema na karibu tena China)

Yule dereva mzee aliniambia huku akizipokea zile noti za dollar 50 na kuondoka zake.
Na mara baada ya kuagana na yule dereva mzee nilibeba mizigo yangu kisha nikaelekea katika
moja ya hotel zilizokuwepo pale karibu na airport.

Ilikua ni hotel ya Zhanjang ambapo nililipa karibu dollar 90 sawa na sh.laki 1 na elfu 44 kwa pesa za nchini mwetu Tanzania.

Na baada ya kulipia niliweka mizigo yangu bila hata kula wala kupumzika nikaenda moja kwa moja mpaka airport ambapo nilianzia katika ofisi ya shirika la ndege la serikali ya Ethiopia na kukuta tiketi zote zimekwisha uzwa pasipo kusalia hata tiketi moja.

Baaada ya kukosa tiketi katika shirika lile la ndege la Ethiopia nilipoteza matumaini kabisa huku nikibakiza matumaini yangu katika mashirika mawili yaliyokua yamebaki moja ilikua ni katika shirika la ndege la Misri na lingine katika shirika la ndege la Afrika kusini.

Basi baada ya kutoka katika shirika la ndege la serikali ya Ethiopia nilienda moja kwa moja katika shirika la ndege la Afrika kusini na kukuta hakuna utofauti na shirika la ndege la Ethiopia nako mambo yalikua vilevile hakuna hata tiketi moja iliyokua imesalia tiketi zote zilionekana kuisha toka majira ya saa saba wakati treni letu lilipokua katika mji wa Shijiazhuang.

Kitendo cha kukosa tena tiketi tena katika shirika la ndege la Afrika kusini kilinikatisha tama kabisa lakini sikua na jinsi zaidi ya kukubali majibu na hivyo kwenda kujaribu bahati yangu ya mwisho katika shirika moja la ndege lililokua limebaki lilikua ni shirika la ndege la Misri ambapo nako nilikuta hamna kitu napo tiketi zote zilikua zimeisha kiukweli nilijihisi kuchoka sana kwa hiyo ilinilazimu nilale hapo Nanning na kisha niondoke kwa ndege za kesho yake usiku.

Baada ya kukosa tiketi katika mashirika yote hayo matatu nilirudi tena katika shirika la ndege la Ethiopia na kukata tiketi ya ndege zinazoondoka kesho usiku wa saa 8 na mara baada ya kukata iyo tiketi iliyonigharimu karibu dollar 1300 zaidi ya million 2 na elfu 80 za Tanzania nilirudi tena hotelini huku nikiwa nimeyaamini maneno ya wahenga yasemayoo kuwa nyota njema huonekana toka asubuhi.

Na mara baada ya kufika hotelini nilichukua simu yangu kwa ajili ya kumpigia mke wangu Tressy na kumfahamisha kwamba ningeondoka nchini China siku ya jumanne saa 8 usiku na ndege ya shirika la serikali ya Ethiopia hivyo ningefika nchini Tanzania siku ya Jumatano muda wa saa 7 au saa 8 mchana.

Nilipiga namba za mke wangu karibu mara tatu lakini simu ilikua inaita tu bila ya kupokelewa nilijipa moyo labda huenda atakua amelala ama kuna kazi atakua anaifanya

Basi baada ya kuona mke wangu Tressy hapokei simu yangu nilikwenda kuoga kisha nikaagiza chakula nikala alafu nikaanza kuifaidi ela yangu niliyolipia hapo hotelini kwa kuanza kuitumia huduma ya internet iliyokuwepo humo chumbani.

Niliperuzi mitandao mbalimbali ya kijamii kisha nikaingia katika ukurasa wa facebook na kulifungua profile la mke wangu Tressy.

Mungu wangu!!!! Nilijikuta nikisema kwa sauti kubwa bila hata kujizuia huku mvua kubwa ya machozi ikianza kunyesha machoni kwangu mara tu baada ya kulifungua profile la mke wangu Tressy katika ukurasa wa facebook.

Haikua rahisi kabisa kuamini kama mtu aliyetakiwa kunifuta machozi ndiye aliyesababisha mimi nitokwe na machozi nilijikuta nikilia sana kwani mambo niliyokua nimeyaona katika profile la mke wangu haikuitaji hata kuambiwa kama tayari nilikua nimeshasalitiwa kwani picha pamoja na status alizokua amezipost mke wangu Tressy zilionekana kujieleza wazi kabisa.

Tressy alikua anaolewa tena na mwanaume mwingine hivyo ndivyo ilivyokua ingawa iliniwia vigumu kuamini lakini picha alizokua amezikweka zilikua zikijieleza wazi.

Kwani aliweka picha nyingi sana zilizojaa uchafu na anasa ambazo kwa mwanamke aliyeolewa asingeweza kufanya vile picha nyingi zilimuonyesha Tressy akiwa amekumbatiwa na mwanaume huku wakiwa wanapigana mabusu.

Kama haitoshi aliweka picha za huyo mwanaume pamoja na mtoto mwenye umri wa kama miaka 4 ama 5 huku akiwa ameandika dady and son

Kiukweli niliumia sana hasa pale nilipogundua kua huenda hata yule mtoto mchanga niliyemuacha akiwa na umri wa miezi 6 wakati nikija masomoni nchini China hakua mwanangu kiukweli nilijihisi kuchanganyakiwa sana, niliuhisi mwili wote ukiishiwa nguvu kiasi cha kuanza kuona kana kwamba ile kompyuta niliyokua naitumia ilikua ikinikejeli.

Lakini hayo yote tisa kumi kama haitoshi Tressy aliamua kuolewa tena kwani picha aliyokua ameiweka kama profile picha yake akiwa na huyo mwanaume katika duka la nguo za maharusi ilionekana kuelezea na kuweka kila kitu wazi.

Nilijikuta nikizidi kuchanganyikiwa huku nikiamini kua ningekufa muda si mrefu kwani mapigo yangu ya moyo yalionekana kupiga haraka haraka sana huku mzunguko wangu wa damu nao ukionekana kuzunguka haraka zaidi ya isivyokua kawaida.

Mvua kubwa ya machozi ilionekana kuyafumba macho yangu kiasi cha kuyafanya yaanze kuvimba na kunifanya nianze kuuona ukungu mzito ukianza kutanda mbele yangu.

Nilijikuta nikianza kuichukia safari yangu ya kurejea nyumbani nchini Tanzania nikatamani niendelee kuishi tena nchini China furaha yangu yote ya kurejea kurudi nyumbani ikageuka na kuwa huzuni nikajiona kama nilikua mjinga kulisuburia treni kwa hamu liwahi kufika wakati tukiwa Chang chun nilipokua nikianza safari yangu ya kuanza kurejea nyumbani.

Nilianza kujichukia sana nikajiona kana kwamba nilikua kinyago labda ndio sababu Tressy aliamua kuniacha na kuamua kuolewa na mwanaume mwingine.
yaani kama isingekua wazazi pamoja na ndugu zangu sidhani kama ningetamani kurudi tena nyumbani nchini Tanzania.

Niliendelea kulia huku nikijutia kwanini niliruhusu uzuri wa mke wangu Tressy uyadanganye macho yangu nikaanza kujiona kua nilikua mjinga sana kumuachia mke wangu Tressy mali zangu nyumba magari kampuni zangu mbili za usafirishaji pamoja na akaunti za benk

Nilijilaumu sana huku nikijiona kua nilikua mjinga sana pengine kuliko wajinga wote wa duniani kiasi cha kufanya nione kwamba watu wote wa China walikua wakinidharau na kunizomea kwa sababu ya ujinga wangu niliokua nimeufanya.

Ilikua ni saa 2 usiku kwa saa za China wakati machozi yalipoonekana kuyafumba macho yangu zaidi kiasi cha kufanya nishindwe hata kuiona mishale ya saa kubwa iliyokua imetundikwa ukutani karibu sana na ile kopmyuta niliyokua nikiitumia.

Ukungu wote ulioonekana kutanda mbele yangu hapo awali uligeuka na kua giza kubwa huku akili yangu ikionekana kutoelewa ni kitu gani kilichokua kinaendelea.

Nililia mpaka nikapitiwa na usingizi mzito sana nililala bila kujielewa huku Israel akionekana kutocheza mbali na roho yangu kwani nilikua kama mtu aliezimia na kukaribia kufa kwa kiu mara baada ya kua amekosa maji jangwani.
usingizi ule mzito ulionekana kuzichukua fahamu zangu zote kwani sikuelewa ni kitu gani kilichokua kinaendelea.

Ilikua ni siku ya Jumanne wakati kengele iliposikika kutoka katika mlango wa chumba nilichokua nimelala pale hotelini Zhanjang.

Na kufanya nishtuke kutoka usingizini ilikua ni majira ya saa 4 asubuhi kwa mujibu wa ile saa kubwa iliyokua imetundikwa pale ukutani karibu kabisa na ile kompyuta niliyokua nikiitumia jana majira ya usiku.

Mara baada ya kushtuka kutoka usingizini hata kabla sijashuka kutoka kitandani ile kengele ilisikika ikigonga tena pale mlangoni
“ Sorry sir breakfast please”
(samahani mh.mlo wa asubuhi tafadhali)

Ilikua ni sauti kike ya mhudumu wa pale hotelini Zhanjang ndiyo iliyonifanya nishuke
kitandani na kuusogelea ule mlango uliokua umepakwa rangi nyeupe.
“Thank you very much”
(asante sana) nilisema mara tu baada ya kuufungua ule mlango na kukipokea kile
Chakula kilichokua kimebebwa juu ya kijitoroli kidogo cha chuma kilichotengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu na kufanya kionekane kupendeza sana.

Basi mara baada ya kupokea chakula kutoka kwa yule muhudumu nilikwenda kuoga kwa ajili ya kuweka mwili safi na kutoa uchovu wote niliolala nao jana usiku
Picha na matukio yote yaliyotokea jana yalionekana kuanza kujirudia kichwani kwangu lakini nilijikaza kiume nikajitahidi kula kile chakula mpaka nikakimaliza kwa sababu ya njaa niliyolala nayo jana usiku.

Na mara baada ya kumaliza kula nilipanga mizigo yangu na kuiandaa vizuri kwa sababu ya safari yangu ndefu ya kurejea nyumbani nchini Tanzania ambayo itaanza saa 8 ya usiku wa siku hio kisha mara baada ya kupanga mizigo yangu na kuhakikisha kuwa kila kitu kipo sawa nilizichukua picha za mke wangu Tressy zilizokuwepo kwenye albamu yangu iliyokua ndani ya begi langu la nguo kisha nikaziweka ndani ya bahasha na kuondoka nazo.

Niliamua kwenda kupunguza mawazo katika fukwe za bahari wakati nikiusubiria muda wa safari
Nilichukua tax nikaenda mpaka katika fukwe za Guangzhou moja kati ya fukwe maarufu sana jijini Beijing nilikaa huko kwa muda wa zaidi ya masaa 8 huku chakula cha mchana nikikila katika fukwe hizo hizo za Guangzhou.

Na kabla sijaondoka katika fukwe hizo nilizuchukua picha za mke wangu Tressy zilizokua kwenye bahasha nikazitupia kwenye bahari ya fukwe hizo kiukweli nilifanya hivyo ili nisizidi kuumia pindi nizionapo picha hizo za mke wangu ambae alikua ameamua kunisaliti na kuniacha bila ya mimi kuwa na kosa lolote nililomtendea.

Basi baada ya kutoka kule ufukweni nilikwenda moja kwa moja mpaka hotelini nikajipumzisha mpaka ilipofika majira ya saa 6 za usiku ndipo nilipoamka nikaenda kuoga kisha nikajiandaa na kukipanga kile chumba vizuri kama kilivyokua mwanzo na mara baada ya ya kumaliza kukipanga nilichukua simu yangu nikajaribu kumpigia tena Tressy.

Nilipiga simu zaidi ya mara tatu mfululizo lakini hali ilikua kama jana Tressy hakupokea simu yangu kiukweli kitendo hicho kiliniumiza sana lakini niliamua kuachana nae nikachukua leso yangu nikajifuta machozi yaliyokua yakilenga lenga kwa huzuni.

Nilivyoona Tressy hapokei simu yangu niliamua kuwapigia rafiki zangu wapenzi nilosoma nao chuo kule Chang chun niliongea nao kwa muda kisha nikawaaga huku nikiwakaribisha sana nchini mwetu Tanzania.

Baada ya kuwaaga rafiki zangu na kukabidhi funguo za hoteli niliibeba mizigo yangu mpaka Nanning pale airport baada ya kufika pale airport nilipokelewa na umati wa zaidi ya watu 250 ambao wote tulikua tukisubiri kukaguliwa mizigo yetu na kisha kuingia ndani ya ndege.

Wakati mimi pamoja na wale abiria wengine tulipokua tukisubiri kukaguliwa ili tuingie kwenye ndege ghaflaa!! Kuna mtu alinipiga juu ya bega la kulia na kufanya nigeuke kumtazama
Mungu wangu nilisema mara tu ya kugeuka na kumtazama yule mtu aliyekua amenipiga bega langu ka kulia sikua nimeamini kama kweli alikua ni

Ilikua ni majira ya saa sita usiku wakati mawingu mazito yalipoonekana kuufunika mwezi na kufanya nyota zionekane kukosa ushirikiano kiasi cha kufanya giza kubwa liutawale mtaa wa Nanning mahali ilipokuwepo airport maarufu ya jiji la Beijing.

Lakini wakati mawingu mazito yanapoonekana kuufunika mwezi na giza kubwa kuutawala mtaa wa Nanning hali ilionekana kuwa tofauti kidogo katika maeneo ulipokuwepo uwanja wa ndege katika mtaa huo.

kwani taa nyingi kubwa zilionekana kutoa mwanga mkubwa bila uchoyo wowote na kuusaidia umati mkubwa wa watu zaidi ya 250 waliokua wakisubiria kukaguliwa mizigo yao kwa ajili ya kuianza safari yao ndefu ya kutoka katika bara lililokua likiaminika kuwa bara kubwa kuliko bara lolote duniani.

Wakati taa hizo kubwa zikionekana kuutendea mema ule umati wa watu zaidi ya 250 mimi pia nilionekana kuwepo miongoni mwa ule umati wa watu ulioonekana kutendewa wema na zile taa kubwa zilizokua zimelizunguka karibu eneo zima la uwanaja wa ndege wa pale jijini Beijing.

Wakati umati huo ukionena kuusubiri kwa hamu kubwa sana muda wa kukaguliwa mizigo kwa ajili ya kuinza safari ndefu ya kutoka katika bara la Asia mpaka bara la Afrika

Kwangu hali ilionekana kua tofauti kabisa kwa sababu ya matatizo yaliyokua yamenitokea siku moja kabla ya kuianza safari yangu na kufanya niichukie safari hiyo ya kurudi nyumbani
Nchini Tanzania

Kiukweli kitendo cha mke wangu Tressy kuniacha pasipo ya mimi kumtendea kosa lolote kiliniumiza sana kiasi cha cha kufanya niichukie safari yangu hiyo ya kurudi nyumbani huku nikiamini kua kila mtu alikua akiniona mjinga kwa sababu ya kitendo changu cha kumuamini mke wangu Tressy na kumuachia mali zangu zote mikononi mwake zikiwemo akaunti zangu zote za benk, magari nyumba pamoja na kampuni zangu mbili za usafirishaji.

Wakati nikiwa mawazoni huku nikionekana kutousuburia muda huo wa kukaguliwa mizigo kwa hamu kama ilivyokua kwa watu wengine ghaflaa!!! nilihisi kuguswa na mtu katika bega langu la kulia na kufanya nigeuke nyuma na kumtazama mtu yule aliyekua amenigusa bega langu.

Mungu wangu!!! Nilisema mara tu baada ya kugeuka nyuma na kumtazama yule mtu aliyekua amenigusa bega langu la kulia na kufanya nigeuke nyuma kwa uwoga na kumtazama kwa sababu ya kutofahamiana na mtu yoyote pale Nanning.

Alikua ni bwana James Scoutland mvulana wa kizungu aliyeonekana kuwa na umri wa kati ya miaka 22 hadi 24 ambaye alikua ni miongoni mwa wateja wangu wa kwanza wa kampuni yangu ya usafirishaji kabla sijaja masomoni nchini China.

“Hey mr.James I never thought if I will see you here”
(Hey bw.James sikudhani kama ningekuona hapa)

Nilimwambia bwana James huku nikitengeneza tabasamu bandia usoni mwangu kwa ajili ya kuyaficha matatizo yaliyonikuta siku moja kabla ya safari yangu na kumkumbatia kwa furaha.

“Me too mr.Davis but how are you and what about youre family are they safe?”

Bonyeza Hapo Chini Kuendelea na Seimulizi

Sehemu ya Pili (2) I Will be Back

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

List of Best Night Clubs and Casino in Tanzania 2022.

Malaika Wangu - Simulizi za Imani na Mafundisho

MALAIKA WANGU: Simulizi za Imani na Mafundisho