I Will be Back: Sehemu Ya Pili (2)
(mimi pia bw,Davis lakini vipi hali yako na hali ya familia yako vipi ipo salama)
Bwana James aliniuliza huku akiifungua mikoni yake kwa ajili ya kulipokea kumbatio langu.
Nadhani James aliniuliza bila ya kujua kuwa swali lake liliuumiza sana moyo wangu kiukweli alipouliza kuhusu familia yangu nilijikuta nikiumia sana moyo kwani bila shaka alikua anaulizia hali ya mtoto ambae mpaka kwa wakati huo hakuonekana kua damu yangu pamoja na Tressy ambae mpaka wakati huo niliokua nikiongea na bwana James hakua mke wangu tena.
Lakini licha ya swali lake kuumiza sana moyo wangu lakini nilijikaza kiume nikamjibu kuwa wapo salama na muda si mrefu Mungu akipenda nitakwenda kuonana nayo nilimjibu huku bwana James huku nikiyazuia machozi yaliyokua yakitaka yaanze kunitoka na sikua na jinsi zaidi ya kufanya hivyo ili kuyaficha matatizo yaliyokua yamenikuta
Basi mara baada ya kusalimiana na bwana James tuliongea nae mambo mengi sana ya kibihashara huku tukipiga stori mbili tatu za hapa na pale kisha akanitambulisha kwa mdogo wake aitwaye Slyvester ambaye nae alikua akisafiri usiku ule katika ileile ndege ya shirika la Ethiopia na safari yake ilikua ikiishia nchini Kenya.
Basi baada ya kunitambulisha kwa mdogo wake Slyvester maongezi yetu yaliendelea kwa muda wa kama nusu saa zaidi wakati ambapo watu walianza kuingia kwenye chumba cha kukaguliwa mizigo yao kwa ajili ya kuinza safari.
Kitendo cha watu watu kuanz kukaguliwa mizigo kilifanya niagane na bwana James ambaye yeye aliniambia kuwa atakua pale chini China kwa muda wa miezi mitatu zaidi kwa sababu ya shughulu zake za kibiashara.
“Goodbye mr James if God wishes 1 day we will meet again at any time in any country ”
(kwaheri bw.James kama Mungu akipenda siku moja tutaonana tena katika muda wowote na katika nchi yoyote)
Nilimwambia bwana James huku nikijiandaa kubeba mizigo yangu kwa ajili ya kuingia katika chumba cha kukagulia mizigo
“Goodbye too mr Davis and thank you so much for what youre company did to me some few years ago”
(kwaheri pia bw Davis na nashukuru sana kwa jinsi kampuni yako ilivyonifanyia miaka michache iliyopita)
“thanks you and goodbye once again mr James”
(nashukuru na kwa heri kwa mara nyinigine bwana James)
Nilimwambia James huku nikimpa mkono wa kwa heri
“thanks mr Davis but I wonder why you were dicided to sell all of youre company”
(Asante sana bw Davis lakini nashangaa kwa nini uliamua kuyauza makampuni yako)
Kiukweli kauili ile kutoka katika kinywa cha bw James ilinishtua sana kiasi cha kufanya niutoe mkono wagu uliokua mikononi mwake.
“what do you say mr James?” nilimuuliza kwa mshangao mara baada ya kuoamini ile kauli yake niliyoisikia
“Davis are you serious? Last four months when I was in Tanzania I came to youre company inorder to make a busness but I met all of youre company selled to some one who called Motemapembe a guy from Congo.
(Davis upo siriasi ? miezi minne iliyopita nilipokua Tanzania nilikuja katika makampuni yako kwa ajili ya kufanya biashara lakini nikakuta yote yameuzwa kwa mtu mmoja aitwaye Motemapenbe kutoka Kongo)
Bwana James aliniambia kwa msisitizo huku akionekana kutoamini kama kweli sikua nimeyauza makampuni yangu .
kiukweli sikutaka kabisa kuyaamini maneno ya bwana James nilijikuta nikianza kulia huku nikishangaa kwa nini Tressy aliamua kunifanyia hivi yaani kaamua kuniacha bila ya mimi kuwa na makosa yoyote lakini kama haitoshi kaamua kuuza mali zangu
hali yangunilianza kubadilika ghaflaa na kua kama ya jana usiku pale hotelini Guangzhou
“Sorry mr Davis I don’t think if I will pain you like this very very sorry but whats wrong”
(samahani bw Davis sikudhani kama ningekuumiza kiasi hichi samahani sana laikni ni nini tatizo)
Bwana James aliniuliza huku akionekana kushangaa sana kwa jinsi nilivyokua nikilia
“my wife has betraying me”
(Mke wangu amenisaliti ) nilimjibu bw James huku nikilia safari hii nililia kwa nguvu zaidi mpaka baadhi ya watu waliokua bado hawajaingia kwenye chumba cha kukagulia mizigo walinishangaa .
“So why you lied to me that they safe”
(sasa kwanini ulinidanganya kuwa hawajambo) bw James aliniuliza
Sikumjibu kitu chochote zaidi ya kumuangalia na kuchukua mizigo yangu kisha nikaanza kupiga hatua kuelekea katika chumba cha kukagulia mizigo.
Lakini kabla sijapiga hata hatua mbili mbele bwana James aliniita tena niligeuka nyuma na kumtazama bila ya kumsemesha neno lolote
“Please mr Davis take care of my young brother”
(samahani mr Davis naomba umuangalie mdogo waangu)
Bw James aliniambia na kufanya nisimame na kumsubiri huyo mdogo wake Slyvester ambaye tulikua tukisafiri nae kwa ndege moja nay eye alikua akiishia nchini Kenya.
“Ok all of you fly well”
(sawa safirini salama) bwana James aliniambia mara tu baada ya mdogo wake kufika pale mahali nilipokua nimesimama hatua chache kutoka kwa mr James
Basi baada ya Slyvester kunifikia niliongozana nae mpaka chumba cha kukagulia mizigo huku mabegi yetu pamoja na simu na kifaa chochote cha chuma kikikaguliwa kwa mashine maaulum zilizokua zimeunganishwa na kompyuta kubwa sana za kisasa
Baada ya kukaguliwa na kukuta hatuna matatizo yoyote tulienda moja kwa moja mpaka sehemu ilipokua imesimama ndege hiyo
Ilikua ni mwendo wa kama dakika 5 ndipo tulipoifikia ndege ile ndege ya Ethiopia na baada ya kuifikia tuliingia ndani mimi nilikaa siti za mbele tofauti na Slyvester ambaye alikaa siti za nyuma kidogo
Nilikaa siti moja pamoja na wazungu wawili mmoja alikua wa kike na mwingine wa kiume ambao niliwakuta wameketi niliwasalimia kisha nikaketi huku tukisubiri abiria wengine waingie na ndipo tuianze safari yetu.
Ilikua ni majira ya saa 7 na nusu usiku wakati sauti za vishindo na minong’ono zilionekana kusikika kwa mbali na kuuvunja ule ukimya uliokua umetawala katika eneo la uwanja wa ndege wa Nanning jijini Beijing nchini China.
Vilikua ni vishindo na minong’ono ya baadhi ya watu waliokua wakimalizia kuuingia ndani ya ndege iliyokua mali ya shirika la ndege la serikali ya Ethiopia .
Wakati watu hao wakionekana kumalizika kuingia ndani ya ndege hiyo mimi pamoja na Slyvester mdogo wake na yule rafiki yangu wa kizungu Mr.James tulikua tumeshaingia ndani ya ndege na hivyo tulikua tukiwasubiria abiria wengine wamalizike kuingia ndipo safari yetu ndefu ya kutoka katika bara la Asia na kwenda katika bara la Afrika ianze.
Rafiki yangu kipenzi Mr.James alikua amenikabidhi mdogo wake huyo Sylvester ambaye kwa mara ya kwanza ndio alikua anakwenda kuikanyaga ardhi ya bara la Afrika ili nimtazame na kuhakikisha anafika salama mpaka mwisho wa safari yake iliyokua inaishia nchini Kenya.
Lakini licha ya rafiki yangu Mr.James kuniomba na kunikabidhi jukumu hilo la kumtazama mdogo wake Slyvester aliyekua na umri wa kati ya miaka 18 hadi 20 ambaye kwa mara ya kwanza ndiyo alikua anaenda kuikanyaga ardhi ya bara la Afrika hali ilionekana kuwa tofauti kidogo kwani mara tu baada ya kuingia ndani ya ndege tulitengana na Slyvester
Ambaye yeye alikwenda kukaa katika siti yake iliyokua upande wa nyuma kabisa ya ndege na mimi nikaenda kukaa katika siti yangu iliyokua upande wa mbele kabisa ya ndege karibu na ulipokuwepo mlango wa kuingilia katika chumba cha marubani na hivyo kufanya jukumu hilo la kumtazama Slyvester ilishindikane na kuonekana kua gumu.
Nilikaa siti ya mbele pamoja na wazungu wawili walioonekana kuwa wapenzi huku mzungu wa kiume akionekana kuwa mkubwa na mrefu kidogo kuliko yule mzungu wa kike.
Basi mara baada ya kukaa niliyakatisha maongezi yao kwa kuwasalimia kiukweli walionekana kuwa watu wakarimu sana kwani waliijibu salamu yangu kwa uchangamfu mkubwa sana huku wakiniuliza sehemu niliyokua ninakwenda, niliwajibu kua ninarudi nyumbani nchini Tanzania
Mara baada ya kuwepo nchini China kimasomo kwa takribani miaka minne.
walifurahi sana kusikia ninaaenda nchini Tanzania kwani nao walikua wakija hukohuko Tanzania kwa lengo la kwenda kutalii katika mbuga mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenda kuupanda mlima kirimanjaro ambao habari zake zilionekana kuwavutia sana wazungu hao wawili walioonekana kua mtu na mpenzi wake.
Wakati maongezi yangu na wazungu hao yakiendelea msururu wa watu waliokua wakiingia ndani ya ndege ulikua umekwisha malizika na kufanya viti vyote vijae watu pasipo hata kiti kimoja kuonekana kubaki wazi.
Baada ya msururu ule kumalizika mlango wa ndege ulifungwana wakati yote hayo yakiendelea mimi pamoja na wale wazungu walioonekana kuwa na hamu kubwa ya kuifahamu Tanzania hatukua tukijua lolote linaloendelea kwa sababu ya utamu wa maongezi yetu yalyofanya nisahau hata matatizo yangu yaliyokua yamenitokea siku chache zilizopita.
Ghalfa!! Nikiwa katikati ya maongezi na wale wazungu wawili sauti laini ya kike yenye lafudhi ya kizungu ilisikika kutoka katika spika nzuri za plastiki zilizokua zimefungwa usawa wa katikati ya kila siti upande wa juu ya paa la ndege hiyo iliyoonekana kupendeza sana kuanzia muonekano mpaka mpangilio wake ambao haukuonekana kutofautiana sana na lile treni nililopanda wakati nikitoka katika mji wa Chang chun kuja jijini Beijing.
“Attention!! We are going to fly very soon, every one make sure you wear the crib well take it down of the seat”
(Angalizo tunakwenda kupaa muda si mrefu kila mtu ahakikishe amefunga mkanda vizuri upo chini siti)
Sauti ile ilirudia mara kusikika mara tatu kisha ikanyamaza
Ilikua ni sauti ya mhudumu wa ndege ikiwatahadgarisha abiria wote kufunga nikanda kwa ajili ya kuepusha migongano wakati wa ndege kupaa
Sauti ile ya muhudumu ilionekana kutiliwa mkazo kwani mara tu ya kuacha kusikika sauti nyingine za vibanio vya kufungia mikanda ilianza kusikika kwa mbali huku kila mtuu akionekana kuinama na kufunga mkanda kwa ajili ya usalama wake binafsi.
Ilichukua kama dakika 5 ambapo mikanda yote ya mule ndani ya ndege ilionekana kupita katika bega la kila abiria kutoka kwenye ungio la kwanza hadi kwenye kibanio cha pili cha mkanda huo kilichokua upande wa pili wa siti.
Baada ya zoezi hili kuonekana kukamilika sauti ile laini kutoka kwa muhudumu wa kike ambaye hakua akionekana kwa wakati huo ilisikika tena kutoka katika zilezile spika za mwanzo
“Its our hopes that every one have already wear the crib properly”
(ni matumaini yetu kwamba kila mtu amekwisha funga mkanda ipasavyo)
Sauti hile ya mhudumu wa kike ilisikika huku ikizidi kuongea tena
“we are going to fly now and for those who have health problems there are plastic pocket behind of each seat its special for vomiting”
(tunakwenda kuruka sasa hivi na kwa wale wenye matatizo ya afya kuna mifuko ya plastic nyuma ya kila siti maalumu kwa ajili ya kutapikia)
Sauti ilizidi kusikika huku ikionekana kusababisha ukimya mkubwa mule ndani ya ndege.
“we wish you all nice journey and enoj our service”
(Tunawatakia wote safari njema na furahieni huduma zetu)
Sauti ile ilimalizia kusikika kisha ikatulia na ghafla mara tu baada ya ile sauti ya muhudumu kutulia ukimya ulionekana kutawala mule ndani ya ndege ulianza kupotea polepole kwa sababu ya sauti za kukoroma kutoka kwa baadhi ya abiria waliokua wameanza kusinzia.
Ilikua ni saa 8 kamili usiku kwa saa za nchini China wakati ambapo injini zote mbili za ile ndege zilionekana kuwashwa na kuanza kuunguruma huku sauti ya miungurumo hio mikubwa ikianza kusikika mpaka ndani ya ndege na kuonekana kuziunga mkono zile sauti za kukoroma na kufanya ukimya wote uliokua umetawala ndani ya ile ndege upotee.
Injini zilionekana kuunguruma kwa karibu dakika 5 nzima kisha ndege ikaanza kukimbia kutoka mwendo mdogo mpaka kufikia mwendo mkali kiasi cha kufanya zile taa kubwa zilizotutendea wema zionekane kupitia madirishani zikikimbia kurudi nyuma harakaharaka sana.
Na wakati taa zile kubwa zikionekana kurudi nyuma kwa kasi sana sauti ya matairi ya ndege hiyo zilianza kusikika kwa mbali kuashiria kua zilikua zimeanza kuicha ardhi ya Beijing China kiasi cha ndege kuinuka mbele kuashiria kuwa tayari tulikua tumeanza kupaa.
Kwa heri China hakika hatutakusahau hivyo ndivyo nafsi za watu wengi zilionekana kuongea kwani kitendo cha watu kuchungulia madirishani na kuona jinsi ndege ile ilivyokua ikiiacha ardhi ya China kilionekana kueleza wazi kabisa hisia zilizokuwepo moyoni mwa watu wengi.
Basi kadri ndege ilivyozidi kulifaidi anga la nchi ya China muda nao ulionekana kutokua nyuma katika kuisogelea afrajili ya usiku huo wakati yote haya yakiendelea ukimya nao ulionekana kutawala tena kwani ilikua nni karibu saa 9 na robo usiku wakati zaidi ya nusu ya abiria wote walionekana kusinzia wakati sauti za kukoroma zikionekana kusikika kwa mbali sana
Huku sauti pamoja na zile ngurumo za injini zikionekana kumezwa na mawingu mazito yalionekana kutoshiba wala kushiba mara baada ya kuumeza mwezi pamoja na nyota hapo awali na kulisababhisha zlile giza zito lilionekana kuzielemea taa za mtaa wa Nanning masaa machache yaliyopita.
Wakati asilimia kubwa ya abiria wakionekana kulala huku wengine wakoinekana kujilazimisha na kuutafuta usingizi kwa lazima mimi bado nilikua nikiongea na yule mzungu wa kiume ambae tulionekana kuzoeana ghafla mara baada ya kujua kuwa safari yetu ilkua ni moja.
Tuliongea mambo mengi sana huku nikimuelezea kuhusu wasifu wa watanzania mila pamoja na tamaduni zao bila kuisahau amani ya nchi yao iliyoonekana kuchukua nafasi kubwa katika mioyo ya watanzania wengi.
Wakati maongezi yetu kati yangu mimi na yule mzungu wa kiume yakiendelea yule mzungu wa kike aliyeonekana kuwa mpenzi wake alionekana kulala huku akiwa amekiegemeza kichwa chake katika kiti cha ndege io kilichotengenezwa kwa ustadi mkubwa na kushindiliwa na pamba laini kwa ndani zilizofanya kiti icho kiwe laini na kisiumize pindi mtu aegamiapo.
Kile kitendo cha yule mzungu wa kike kulala kilionekana kumfurahisha sana yule mzungu wa kiume ambaye tangu tuzoeane sikua nimemfahamua hata jina lake.
Sikujua kwa nini alifurahia sana kitendo cha mpenzi wake kulala lakini ghafla nikiwa katika hali ya kumshangaa aliuchukua mkono wake wa kushoto na kuupepesa juu ya uso wa mpenzi wake na aliporidhika kuwa mpenzi wake huyo amelala alinisogelea tena mpaka pale nilipokua nimekaa akamnishika bega
Huku akianza kuongea kwa uoga sana na hofu ya kusikiwa na yule mpenzi wake aleyekua amelala.
Alianza kuniambia mambo ambayo yalionekana kuniogopesha na kunitisha sana kiasi cha kufanya niyakumbuke matatizo yangu yaliyonitokea siku chache zilizopita
Alikua akiongea kwa hofu sana huku akitazama nyuma mara mbilimbili ili kuhakikisha kama yule mpenzi wake bado alikua amelala.
I’m Joe Posmerk” yule mzungu wa kiume alizidi kuniambia huku safari hii akionekana kunong’ona sana kwa ajili ya kuogopa kusikiwa na mtu mwingine yoyote tofauti na mimi.
“I think I trust you and that why I want to tell you my secret which I kept for a long time and I hope you will help me”
(Nadhani ninakuamini na ndio maana ninataka nikueleze siri yangu ambayo nimeitunza kwa muda mrefu sana na ninatumaini utanisaidia)
Kiukweli yale maneno ya yule mzungu niliyekua nimekaa nae na kuongea nae tangu mwanzo wa safari na kujitambulisha kwangu kwa jina la Joe yalionekana kuzidi kunitisha sana huku yakionena kufungua mlango na kuyaruhusu maswali yasiyo na majibu yapokezane kuingia na kutoka kichwani mwangu nilijikuta nikianza kuogopa zaidi
Kwasababu nilijiuliza ni siri gani anayotaka kuniambia halafu nimsaidie na nitawezaje kumsaidia wakati mimi mwenyewe nilikua na matatizo yangu binafsi yaliyoonekana kuuzidi uzito ufahamu wangu.
Ilikua ni majira ya saa 9 usiku wakati ndege ya shirika la serikali la Ethiopia inapoonekana kuchepuka katikati ya mawingu mazito ya anga la China.
Mawingu hayo mazito yanaonekana kupambwa na giza zito giza linalopelekea na kusababisha karibu kila abiria aliyekua ndani ya ndege hiyo inayomilikiwa na serikali ya Ethiopia aonekana kusinzia.
Ukimya mkubwa unaonekana kuendelea kuitawala ndege hiyo huku sauti za kukoroma kutoka kwa watu waliosinzia zikionekana kusikika kwa mbali na kuzipita zile sauti za miungurumo ya injini za ndege hiyo zilizoonekana kumezwa na uzito wa mawingu yaliyokua yamelizunguka lile anga la nchi ya China kiasi cha kufanya mwezi pamoja na nyota zionekane kukosa ushirikiano na kusabanisha giza zito lionekane kula ujana katika maeneo mengi ya nchi hiyo.
Wakati ndege ikionekana kuzidi kuchepuka na kulifaidi anga la nchi ya China huku abiria walio wengi nao wakionekana kusinzia hali ilikua tofauti kidogo kwa upande wangu kwani badala ya mimi kulala kama ilivyokua kwa abiria wengine ndio kwanza nilikua katikati ya maongezi mazito maongezi yaliyoonekana kuutia hofu moyo wangu kiasi cha kufanya maswali yenye vihelehele yasiyokua na majibu yaanze kupokezana kuingia na kutoka ndani ya kichwa changu.
Yalikua ni maongezi mazito sana kati yangu mimi na yule mzungu aliyekua amejitambulisha kwangu kwa jina la Joel Posmerk ambaye ndio kwa mara ya kwanza tulikua tumekutana mle ndani ya ile ndege inayomilikiwa na serikali ya Ethiopia.
kitendo cha yule cha yule mzungu kuongea na mimi kwa tahadhari kubwa huku akionekana kuogopa kusikiwa na mtu yoyote tofauti na mimi kilionekana kunishtua sana kiasi cha kufanya hofu nzito ionekane kuuvaa mwili wangu na kuingia katika mzunguko wangu wa damu.
“Its a big secret I hope you will help”
(Ni siri kubwa nadhani utanisaidia)
Yalikua ni maneno ya yule mzungu bwana Joel ambayo yalizidi kunichanganya sana kiasi cha kufanya hofu nzito itawale mbele yangu kwani kitendo cha mtu asiyekufahamu wala wewe kumfahamu kukuomba msaada ambao hakutaka watu wengine wausikie kiilionekana kua cha hatari sana katika upeo wa macho yangu.
“How can I help you? While I have my own problems which I supposed to solve”
(Nitawezaje kukusaidia wakati mimi mwenyewe nina matatizo yangu nniniayotakiwa kuyatatua)
Nilijikuta niliongea kwa sauti kidogo kwa ajili ya kuonyesha msisitizo ambao nilidhani ungemkatisha tama mzungu huyo ambae sikua nikifahamiana nae kiundani zaidi.
“Shshshshshsh!! Please don’t speak loud you will wake up my fiancé”
(shshshshshsh!! Tafadhali usizungumze kwa sauti utamwamsha mpenzi wangu)
ule mzumgu aliniambia huku akionyesha kwa ishara kwa kukisogeza kidole cha nne katika mdomo wake
kukweli nilionekana kuchanganyikiwa kwani kitendo cha mzungu huyo kuonekana kubeba jambo zito ambalo hakutaka hata mpenzi wake alifahamu ndicho kilichozidi kunitia na kufanya nianze kumuuliza maswali mazito lakini kabla hata sijaanza kumuuliza yule mzungu aliendelea kuniambia tena.
“As I told you early I’m Joel Posmerk I am a british but I live here China for six month because I was learning Kung FU at Shaw leen university after being finished my sniper studies at Burma Thailand with Veitnam souldiers”
(Kama nilivyokwambia mwanzo naitwa Joel Posmerk mimi ni muingereza lakini nimekaa hapa China kwa miezi 6 kwa sababu nilikua najifunza Kung FU katika chuo cha Mashaurini mara baada ya kuitimu mafunzo yangu ya usniper katika jeshi la Veitnam huko Burma Thailand.
Yule mzungu aliniambia huku akiongea kwa saauti ya chini sana kwa kuhofia kusikika na mtu awaye yeyote tofauti na mimi niliyekua nikiongea nae.
“why you decide to learn all those dangerous studies are you a terrorist?”
(kwanini umeamua kujifunza masomo yote hay ya hatari, wewe ni gaidi)
Nilijikuta nikimuuliza tena Joel huku nikitokwa na jasho jembamba mara baada ya fahamu zangu kugundua kuwa nilikua nimekwishaanza kumuogopa
“Im not a terrorist am just a normal citizen”
(mimi sio gaidi ni raia wa kawaida) Joel alinijibu huku akiangalia saa yake ya mkononi kuashiria kwamba alitakiwa awahi kuniambia ile siri yake nzito kabla abiria wengine pamoja na mpenzi wake hawajaamka.
“So if you’re not a terrorist why you did all of this”
(kama wewe sio gaidi kwanini umefanya hivyo)
Niliendelea kumuuliza
“I did all of this because before my mother die she gave a mission of revange”
(nimeyafanya haya yote kwasababu kabla mama yangu hajafa aliniachia kazi ya kulipiza kisasi)
Joel alizidi kuniambia na kufanya nizidi kupata maswali mengi ya kumuuliza.
“which revange? And why you don’t want to tell this to youre girlfriend”
(kisasi kipi na kwanini hautaki kumshirikisha mpenzi wako)
Nlizidi kumuuliza huku majibu yake yakoonekana kukata usingizi uliokua ukinielemea na kufanya nizidi kupata hamu ya kumsikiliza zaidi.
“I don’t trust her that why I hide this secret to her because I hate if she will know this secret one day she can betray me and put my life in danger”
(Simuamini ndio maana nimemficha hii siri kwasababu kama akiifahamu siku moja anaweza akanisaliti na kuyaweka maisha yangu hatarini.
Yule mzungu aliniambia huku akigeuka nyuma kumtazama mpenzi wake mara kwa mara kama bado alikua amelala kwa ajili ya kuogopa asiyasikie maongezi yetu.
“so if you fail to trust youre lover why you trust me very faster while we never knowing each other before”
(sasa kama umeshindwa kumuamini mpenzi wako mbona umeniamini mimi haraka wakati tulikua hatufahamiani kabla)
Niliendelea kumuuliza tena
“I think I trust you very faster because I heard that you were owning two compamy of transportation in Tanzania
(Nadhani nimekuamini haraka kwa sababu nimesikia ulikua unamiliki kampuni za usafirishji Tanzania)
Yule mzungu aliniambia na kufanya nishtuke sana kiasi cha kumuona kama alikua akinifuatilia
“where did you heard it ?”
(wewe umesikia wapi) nilimuuliza kwa mshangao mkubwa sana huku hofu niliyokua nayo mwanzo ikionekana kuongezeka zaidi
“I heard when you were talking with Mr.James few time before we enter in inspection room”
(nilisikia wakati ukiongea nab w.James muda mchache kabla hatujaingia katika chumba cha ukaguzi)
Yule mzungu aliniambia na kufanya nizidi kushtuka zaidi na kugundua kua wakati wote niliokua nikiongea na Mr James kaka yake na yule mzungu mdogo Slyvester ambae nilikua nasafiri nae ndani ya ndege moja yeye Joel alikua ananisikia.
“so how can I help you because my all companys have selled by my wife after betraying me”
(Kwahiyo nikusaidiaje kwa sababu makampuni yangu yote yameuzwa na mke wangu mara baada ya kunisaliti)
Nilimjibu yule mzungu bw,Joel hukunnikisuburi jibu lake kwa hamu kubwa
“Yes that why I told you I never trust my girlfriend because many women have a weakness hearts”
(ndio maana nimekwambia simuamini mpenzi wangu kwa sababu wanawake wengi wana mioyo midhaifu )
Yule mzungu aliniambia
“I got you so what can I help you”
(nimekuelewa kwahiyo nikusaidie nini?)
Sehemu ya Tatu (3) I Will be Back
- 97shares
- Facebook43
- Twitter54
- Gmail
- Copy Link