I Will be Back: Sehemu Ya Tatu (3)
Nilimuuiza yule mzungu ambapo baada ya kumuuliza tu aligeuka nyuma na kumuangalia mpenzi wake kama bado alikua amelala kisha akatazama kila upande wa mule ndani kwenye ndege kwaajili ya kuhakikisha kama abiria wengine nao walikua wamelala na mara baada ya kuridhika ndipo akavuta pumzi zake kwa nguvu kisha akazishusha na kuanza kuniambia.
Ilikua ni majira ya saa 10 za afrajili wakati ambapo bwana Joel alianza kuniambia ile siri nzito ambayo hakutaka mtu yoyote tofauti na mimi aifahamu.
“It’s a long story nigger but I have to tell you cz I hope you can help me to finish this mission”
(ni story ndefu niga lakini lazima nikuambie kwa sababu nadhani umaweza kunisaidia kuimaliza hii kazi)))(mission kazi ambayo lazima uifanye kwa ajili ya kutimiza lengo Fulani kama kulipiza kisasi,kuiba,kumkomboa mtu n.k) yule mzungu aliniambia
“ok go on”
(sawa endelea) nilimwambia yule mzungu ili aanze kunisimulia hiyo siri yake
Yule mzungu bila kuchelewa alianza kuniambia
“Two years ago my father was move from London to Afica, he moved Congo and he was start running his business with the rich guy from Congo …
Ilikua ni siri kubwa sana halafu nzito, siri iliyotutoa machozi mimi pamoja na yule Joel kijana wa kizungu ambaye alikua amemdanganya mpenzi wake kuwa walikua wakienda nchini Tanzania kutalii kumbe nyuma ya pazia Joel alikua na kazi kubwa sana ya kuifanya kwa ajili ya kutimiza maagizo aliyokua ameachiwa na marehemu mama yake.
Lakini licha ya siri ile kututoa machozi lakini ilionekana kufanana baadhi ya matukio kiasi cha kufanya na mimi nione kuwa nilikuwa nikihusika katika ile mission ya Joel kwa ajili ya kuyaekeleza maagizo aliyokua ameachiwa na marehemu mama yake.
Joel Poesmark hakua akija nchini Tanzania kwa lengo la kutalii kama alivyo mdanganya mpenzi wake ambaye muda wote ule alikua hajielewi kwa sababu ya kupitiwa na uisngizi mzito uliozichukua fahamu zake kama ilivyokua kwa abiria wengine.
Joel alikua anakuja nchini Tanzania kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa kijana wa kikongo aliyekimbilia nchini Tanzania kutokea katika nchi ya Kongo mara baada ya kumuua baba yake Mr.Poesmark aliyetoka nchiniUingereza miaka miwili iliyopita na kwenda nchini Kongo ambapo alifungua biashara kubwa ya kuuza magari yaliyotumika kutoka nchini Japani na kuyasambaza katika nchi za Kongo pamoja na Angola.
Biashara ile ilionekana kumlipa sana Mr.poesmark na kumpatia utajiri mwingi sana uliomtoa udenda kijana yule wa kikongo ambaye aliamua kumuua Mr.poesmark na kuiba mali zake zote karibu dola million 2 za kimarekani ambazo ni sawa na shilingi bilioni tatu na milioni mia 2 za Tanzania.
Kitendo cha Joel kuniambia kuwa alikua anakuja nchini Tanzania kumtafuta yule raia wa Kongo aliyekua amemuua baba yake na kuiba mali zake kilinishtua sana na kufanya niyakumbuke yale maneno ya bwana James kaka yake na yule mzungu mdogo Slyvester niliekua nikisafiri nae ndani ya ndege moja ambapo yeye alikua anakwenda nchini Kenya.
“All of you’re companies are selled to a guy from Congo who called Motemapembe”
(makampuni yako yote yameuzwa kwa mtu mmoja kutoka Kongo aitwaye Motemapembe)
Yalikua ni maneno ya rafiki yangu kipenzi James siku nilipoongea nae baada ya kukutana nae pale Nanning airport usiku muda mfupi kabla sijaianza safari yangu ya kurejea nyumbani.
Akili zangu zilishtuka sana licha ya kutomwambia Joel lakini akilini kwangu ilianza kunijia picha kuwa huenda yale makampuni yangu yote mawili ya usafirishaji alikua ameyanunua huyo mkongo kutoka kwa mke wanguTressy aliyeamua kuyaharibu maisha yangu kwa kuniacha bila sababu na kuamua kuyatia umaskini maisha yangu kwa kuziuza mali zangu zote nilizokua nikizitegemea sana katika kuniingizia kipato.
“I think I know this bastard who you talking about”
(nadhani ninamfahamu uyu mwanaharamu unaemuongelea)
Nilimwambia Joel na kumfanya aghutuke sana , nilimwambia huku nikifuta machozi yaliyonitoka hasa baada ya akili zangu kuanza kuamini kuwa huenda ikawa huyo mkongo aliyenunua makampuni yangu yote mawili ya usafirishaji kutoka kwa Tressy.
“Are you sure?”
(Una uhakika) Joel aliniambia mara tu baada ya mimi kumwambia kuwa huenda ninamfahamu huyo mwanaharamu aliyekua akimuongelea.
“Im not sure yet but as I told you, my wife betrayed and sells all of my companies and according to Mr James told me all this, that the buyer of my companies is a guy from Congo”
(sina uhakika sana lakini kama nilivyokwambia mke wangu amenisaliti kwa kuyauza makampuni yangu yote na kwa mujibu wa Mr James aliyeniambia haya yote mnunuzi wa makampuni yangu ni mtu kutoka Kongo)
Nilimwambia Joel ambaye alikua ametulia huku akinisikiliza kwa makini sana
“Is it possible?”
(inawezekana?) Joel aliniuliza baada ya mimi kumaliza kuongea kabla hata sijameza fundo la mate.
“Yeah it possible because as you told me that your father was the cars seller and supplier and my companies were dealings with transportation don’t you think there is something match here”
(Yeah inaweza kuja kama ulivyoniambia kuwa baba yako alikua muuzaji na msambazaji wa magari halafu mimi nilikua namiliki kampuni za usafirishaji huoni kama kunakitu kinataka kufanana)
“May be your right but I remember let me show you the picture of that guy which my mother gave to me before he die”
(unaweza kuwa sahihi lakini nimekumbuka ngoja nikuonyeshe picha ya huyo mtu ambayo mama yangu aliniachia kabla hajafariki)
Joel aliniambia huku akikagua mifuko ya koti lake zito alilokua amelivaa kutokana na baridi iliyosababishwa na hali ya hewa ya pale jijini Beijing.
Ilikua ni saa 11 karibu na nusu, Joel alikua bize kuikagua mifuko ya koti lake, kuitafuta picha ya huyo mkongo aliyesadikika kumuua baba yake kutokana na maelezo ya marehemu mama yake na Joel.
Ghafla!! Akiwa katika kuikagua mifuko yake sauti ya kike ilisikika kutoka upande wa pili wa viti tulipokua tumekaa.
“Baby you are not sleep?”
(mpenzi haujalala) ilikua ni sauti ya mpenzi wake na Joel aliyeuamka usingizini muda mchache uliopita.
Kitendo cha mpenzi wa Joel kuamka kiliashiria kuwa huo ndio ulikua mwisho wa maongezi yangu na Joel na baada ya yeye kuamka mimi nilijidai kukoroma kana kwamba nilikua katika usingizi mzito sana nilifanya hivi ili kumzuga kua hakuna kitu chochote kilichokua kinaendelea kati yangu na Joel
ZzZzZz ZzZzZ!! KROWH KROWH nilikoroma kana kwamba nilikua usingizini kumbe nilikua nikimzuga huyo mpenzi wake na Joel aliyetoka kushtuka kutoka usingizini muda mfupi uliopita.
“Baby plz just try to sleep even one hour otherwise youn will tired”
(mpenzi basi jaribu kulala hata saa moja lasivyo utachoka sana)
Sauti laini ya huyo mpenzi wa Joel ilimsihi Joel ajaribu kulala kwa baada ya kufumwa na mpenzi wake akiwaa macho anatafuta picha ya yule mwanaharamu kutoka Kongo kwa ajili ya kunionyesha.
Nilikua mzugaji mzuri, niliongeza tena sauti yangu ya kukoroma kwa makusudi ili kuharibu maongezi yao mara baada ya kumpiga Joel kajicho upande na kumuona kua alikua ameshaanza kuchoka na maongezi ya mpenzi wake ambaye sikua nikimfahamu jina lake
Nilifanya hivi kwa lengo la kupata tena nafasi ya kuongea na Joel, nilikua na hamu kubwa sana ya kumuona huyo mkongo ambaye tulikua tukimuongelea, lakini pia niliingiwa na wivu, mapenzi yao yalinikumbusha Tressy wangu ambae alikua amenipiga changa la macho, kunisaliti na kuuza mali zangu zote.
“why this guy sound like the frog”
(kwanini huyu anakoroma kama chura)
Yule mpenzi mtoto wa kike alimuuliza mpenziwe Joel, kelele zangu zilimkera.
“may be he tired”
(labda amechoka)
Joel alimwambia mpenzi wake huku akijua wazi kua tulikua tukimchezea huyo mtoto wa kike picha la kihindi.
Na wakati hayo yote yanaendelea mimi nilikua nikitabasamu kimoyomoyo kwani mission yangu ndogo ya kumuokoa Joel ilikua imeshafanikiwa na kuwafanya bwana Joel na mpenzi wake waache mazungumzo yao.
Kitendo cha kuzuga kua nilikua nimelala kilimuokoa Joel dhidi ya mpenzi wake ambae hakugundua kama tulikua na ajenda ya siri. Dakika 40 nilizozitumia katika uzugaji huo zilitosha kuwaamsha baadhi ya abiria waliokua wamelala kweli. Ilikua imefika saa 12 asubuhi.
“Good morning guys” niliwasalimia.
Tuliongea kidogo, niliwapa udambwi dambwi juu ya Mlima kilimanjaro ambao ndio ulikua kivutio kikubwa masikioni mwa mpenzi wake na Joel. Aliporidhika niliwaacha waendelee na maongezi yao kisha nikaanza kusikiliza mziki kutoka kwenye ile ipad yangu ya pink.
Safari ilikua ndefu kupita maelezo. Saa 5 na nusu asubuhi tulitua Adisi ababa Ethiopia kubadilisha ndege na kisha kuendelea na safari.
Tulitoka Ethiopia, tulitumia masaa matatu tukaenda kutua jijini Nairobi, baadhi ya abiria waliteremka. Slyvester mdogo wake na yule rafiki yangu kipenzi Mr.James niliyekutana nae kule airport ya Nanning nchini China alikua miongoni mwao, alishuka nairobi, kutokana na muda tuliagana kwa kupungiana mikono.
Safari ya kuelekea nyumbani Tanzania ikaanza, hofu kubwa ilianza kutanda, mawazo mfululizo yalipokezana kuingia na kutoka kichwani mwangu. Nilimuomba Mungu nisikutane na matatizo mengine tofauti na yale ya mke wangu Tressy.
Ilikua ni saa 8 na robo kwa masaa ya nchi za Afrika mashariki, tulipopaa tena na kuiacha ardhi ya Kenya kuelekea Tanzania. Masaa machache sana yalibaki, tulitumia masa manne na nusu kutua ndani ya uwanja wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es salaam.
Ilikua ni hamu kubwa sana kwa abiria wasiokua wazawa, kama ilivyokua kwa Joel na mpenzi wake ambao walikua wanafika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza.
Ndege ilitua, abiria wote tulishuka, kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne niliikanyaga ardhi ya nchi yangu pendwa, iliyojaliwa amani na utulivu wa kutosha.
“Thank you friend for everything” ( Asante rafiki kwa kila kitu ) Joel na mpenzi wake waliniaga huku tukipeana mikono. Kabla sijatengana nao Joel aliniita pembeni kidogo, alichukua mawasiliano yangu na kuahidi kunitafuta siku chache zijazo.
Uwanja wa ndege sikuona ndugu wala wazazi wangu wakija kunipokea, kitendo hicho kilinishtua kidogo lakini sikujali sana. Nabii hakubaliki nyumbani lakini hapotei. Sikuepi Tanzania miaka minne lakini nilikumbuka kila mtaa, japo mabadiliko makubwa yalikuwepo, lakini nitaanzaje kupotea wakati nilizaliwa na kukulia jijini Dar es salaam.
Nilichukua usafiri wa tax, dereva alifuata maelekezo yangu, alinipeleka nyumbani kwangu nilipokua nkikishi na mke wangu Tressy kabla ya kwenda masomoni
Uwanja wa ndege hadi kwangu ilikua safari fupi kuliko ile ya kutoka China mpaka Tanzania. Ufupi huo uliongeza wasiwasi mkubwa lakini sikua na jinsi ilikua ni lazima nikajionee kwa macho yale niliyoyasikia.
Uwingi wa magari jijini Dar es salaam na ukubwa ulitukawiza kidogo, tulitumia muda wa saa moja na robo mpaka kufika nyumbani kwangu.
Mungu wangu! Nilichosikia kwa watu ndicho nilichokikuta, kiukweli sikuamini nilichokua nimekiona mara baada ya kufika nyumbani kwangu. Kama nilivyotegemea nilikuta nyumba yangu imeuzwa pamoja na magari yangu mawili, nilihisi kuchanganyikiwa sana.
Ghafla bila kujielewa machozi yalianza kujitokea machoni kwangu, kilio cha sauti kuu kiliuvamia mdomo wangu, nililia kama mtoto. Ilikua ngumu kuamini kama kweli Tressy mwanamke niliyempenda kuliko wote ukiacha mama yangu mzazi juu ya uso wa dunia hii, alikua amedhamiria kuyaharibu maisha yangu kiasi hicho kwani kunisaliti aliona haitoshi akaamua kuuza na mali zangu.
Niliomba iwe ni ndoto lakini bahati mbaya haikua, mwanzo sikuamini lakini kitendo cha mlinzi getini, kunizuia kuingia ndani tena kwa kutumia silaha kiliipa nguvu akili yangu kuamini kilichotokea.
Umbea wa dereva tax ulinisaidia, kwani hakua ameondoka, alishuhudia kutoka mwazo hadi mwisho wa kile kilichotokea. Ghafla huruma ilimuingia, aliamua kunisaidia, alinitendea wema mkubwa sana.
Kama ndugu yake alibeba mizigo yangu na kunirudisha kwenye gari lake.
“Usijali kaka ndiyo ukubwa huo pole sana” aliniambia kunitia moyo.
Niliukubali wema wake, kabla sijaingia kwenye gari niliomba nafasi nikaongee na mmoja wa majirani zangu wakati nilipokua nikiishi hapo. Yule Dereva tax alikubali, bila kuchelewa nyumbani kwa Mzee Ambrosi, jirani yangu mkubwa ambaye nikizoeana nae kupitia mpira wa mguu, tulikua watani wa jadi, mimi nilikua yanga na yeye alikua simba ama mkia fc kama nilivozoea kumtania.
Kwa ufupi Mzee Ambrosi aliniambia kila kitu kuhusu Tressy kuwa alikua ameuza kila kitu changu, nyumba zangu zote 5 magari yangu yote manne pamoja na habari za kusadikika kua alikua amekuchukua pesa zangu zote za benki, bila kusahau kampuni yangu, ambako nako alikua ameuza hisa zote 95% nilizokua nazimiliki. Pia aliniambia kua Tressy alikua anatembea na pedeshee maarufu kuliko wote jijini Dar es salaam papaa Motema pembe muzee ya kutumbua mapesa, na si muda mrefu wangefunga ndoa.
Maneno ya yule jirani yangu yalinimaliza nguvu, nilijuta kwa nini nilienda kumuuliza, yani kama isingekua yule dereva tax kuniwahi nahisi ningeanguka chini na kuukumbatia mchanga.
Hata ungekua wewe ungelia, yule dereva tax machozi yalimtoka, Mzee Ambrosi nae aliuweka upinzani wetu wa jadi kando na kunipa pole. Niliumia sana, jamani mapenzi yanauma acheni masihara, labda yalizidiwa na maumivu ya uchungu wa uzazi tu, tofauti na hapo sioni kitu kinachoweza kuzidi maumivu ya mapenzi.
Niligeuka kua kifurushi cha mahindi, kwa mara nyingine yule dereva tax alisaidiana na Mzee Ambrosi kunipeleka kwenye gari.
Sikua na muda wa kuongea wala kuangalia wapi tulipokua tunaenda, muda wote niliuwaza umasikini kichwani kwangu, toka utoto wangu hakuna kitu nilikichukia kama umasikini, umasikini ni utumwa kuliko hata ule wa kizungu, umasikini utakufanya uwafulie watu wazima mpaka nguo zao za ndani, umasikini utakufanya uwalambe watu miguu, kama haitoshi utakufanya udharaurike, wapo watakao kuona muhuni, wapo watakao kuona bwege, fala, mjinga, jamani ndugu zangu umasikini ni mbaya mno, naombe tuuchukie, umasikini unaleta aibu na kujipendekeza, mademu wote wakali utaishia kuwala kwa macho, vyakula vyote vitamu utaishia kunusa harufu zake kwa majirani.
Nilijihurumia sana, hasa nilipowafikiria wazazi pamoja na ndugu zangu ambao mimi ndiye nilikua tegemeo lao kwa kila kitu.
Kama yule dereva tax angetaka kunifanyia kitu chochote kibaya, kuniibia au kuniua angefanikiwa kiurahisi. Muda wote huo akili ilikua haifanyi kazi yani hata mtu angeniuliza moja kujumlisha moja ni ngapi ningekosa jibu.
Mawazo mfululizo yalikishambulia kichwa changu, kama feni mzunguko wangu wa damu ulizunguka haraka, mapigo ya moyo yaliongezeka, presha nayo ikaamua kula ujana mwilini mwangu.
Ghafla macho yangu yaliacha kuiona picha kubwa ya umasikini iliyokua ikikatiza mbele yangu, ukungu mzito uliyaelemea kiasi kwamba nikashindwa hata kusoma saa ya gari kwenye dash board.
Sauti ya kifo ilinukia puani mwangu, kwa mbali sana nilisikia ni kama israel mtoa roho akiliita jina langu lakini kwa bahati nzuri au mbaya sikuitika, midomo yangu haikua na nguvu kwa sababu ya kulia.
Nilikua kama zumbukuku asiyekua na akili, mwanzo sikujua wapi tunaelekea lakini safari hii sikujua tena ni kitu gani kimetokea kwani matukio ya ajabu yalifululiza, kwanza nilianza kuona giza zito ghafla, pili mwili ukaisha nguvu tokea hapo sikujua nini kiliendelea.
Nilikuja kushtuka saa nne kasoro asubuhi. Nilijikuta ndani ya chumba kidogo kilichopakwa rangi nyeupe na bluu ambayo haijakolea sana. Kitanda nilichokua nimelalia na mashuka niliyokua nimejifunika vilinisaidia kupata majibu, sikuhitaji kuuliza kama pale palikua ni hospitali.
Niliangaza macho yangu pande zote, japo yalikua mazito lakini safari hii ukungu ulipungua na niliweza kuona kwa kiasi fulani. Dereva tax ndiye alikua mtu wa kwanza kumuona, alikua amekaa karibu na dirisha huku pembeni yake alikuepo Mzee Ambrosi yule jirani yangu wa muda mrefu.
“Kwanini nipo hapa nini kimetokea?” dishi langu liliyumba. Niliuliza huku nikijaribu kuzirudisha kumbukumbu nyuma.
Ni rahisi kuvumilia matatizo lakini sio kuyasahau, nilitumia muda mchache kuvuta kumbukumbu na nilikumbuka kila kitu. Kila kilichotokea jana kilijirudia kama picha ya kutisha machoni kwangu. Nilikumbuka nilivyotua uwanja wa ndege mpaka nilivyokwenda nyumbani kwangu na kupokelewa na yale matatizo. Nilikumbuka vilivyobebwa mpaka kwenye gari, kumbukumbu zikakoma hadi nilipoamka hapo na kujikuta hospitali.
Kumbukumbu hizo na kitendo cha kutowaona ndugu wala wazazi wngu vilitosha kunitoa tena machozi, dereva tax na Mzee Ambrosi walisogelea, walinipa pole, walinituliza walipoona sielekei kutulia daktari aliitwa, bila hata salamu alichanganya sindano ya nusu kaputi kwenye dripu niliyokua nimetundikiwa, ghalfa usingizi mzito ukanichukua.
Nilikuja kuzinduka tena majira ya saa 7 mchana. Dereva tax pamoja na Mzee Ambrosi bado walikuwepo. Simanzi na huzuni nyingi viliwatesa. Walinipa chakula nilikula kiasi tena kwa kujilazimisha, matunda waliyonipatia yalitenda wema mkubwa yalipa nguvu ya kuweza hata kuinuka kitandani na kwenda msalani.
Baada ya kula, kupumzika na kila kitu daktari alikuja, kitendo cha kuweza kuinuka na kutembea bila kushikiliwa kilimuingiza king, alinipa ruhusa yakutoka.
“Hana ugonjwa ni mshtuko tu aliopata” alituambia huku akinichomolea sindano ya dripi mkoni.
“Jitahidi kula vizuri na kufanya mazoezi” alimalizia.
Baada ya kutoka hospitali, tuliongozana hadi nyumbani kwa Mzee Ambrosi. Dereva tax alinikabidhi mizigo yangu akaniambia nikiwa na shida nisisite kumtafuta, nilimlipa pesa zake lakini alikataa kuzipokea, nilimshukuru sana kwa ukarimu wake.
Kwa Mzee Ambrosi palikua kama nyumbani kwangu, niliifahamu nyumba nzima pia nilikua huru kufanya kila kitu. Baada tu ya Dereva tax kuondoka nilienda bafuni kuoga, nilibadilisha nguo na kwenda kupumzika katika chumba nilichopewa.
Chumbani nilianza kuikagua simu yangu, nilikutana na meseji na simu kadhaa ambazo sikua nimezipokea. Katika list ya simu niliona namba mpya ikiwa imenipigia zaidi ya mara tatu. Sikupoteza muda niliipiga na kuweka simu sikioni, bahati nzuri iliita.
“Hellow Davis” sauti ilisikika baada tu ya kupokelewa.
Alikua ni Joel, niliyekaa nae siti moja pamoja na mpenzi wake kwenye safari yangu ya kutoka nchini China hadi Tanzania.
“Hi Joel where are you?” nilimuuliza.
“Sun set Hotel, Masaki” alinijibu.
Sikupoteza muda nilikata simu, nilikua na hasira, ilikua ni lazima nikamuone Joel yeye ndiye mtu pekee ambaye angenisaidia kumuadhibu Motemapembe. Nilitumia gari la Mzee Ambrosi kwenda hotelini, japo alinikatalia mwanzo kuhofia usalama wangu lakini mwisho wa siku alikubali kunipa funguo.
Nilifika mpaka Sun set hotel, nilimpigia simu Joel, mzungu ni mzungu tu hata dakika moja haikupita tayari Joel alikua mbele yangu.
“Your welcome Bro” alinikaribisha.
Tulisalimiana kisha tukaenda mpaka sehemu ilipokuwepo bar tulivu ndani ya hoteli hiyo. Ilikua ajenda ya siri hakutaka mtu yoyote mbali na mimi asikie wala afahamu kile tulichokua tukienda kukijadili, hata pua ya mpenzi wake haikutakiwa kujua hata kidogo.
Yalikua maongezi mazito kama mtu angetusikia basi angepiga simu polisi au kutufungulia mashitaka ya kigaidi.
Niliongea sana na Joel. Joel alikua amekuja nchini Tanzania kwa ajili ya kumtafuta na kumuua raia mmoja wa kikongo aishie nchini Tanzania. Kutokana na maelezo yake raia huyo alikua amemuua baba yake mzazi na Joel marehemu Joackim Poesmark, ambapo baada ya kumuua mkongo huyo mkongo huyo aliuchukua utajiri wote wa baba yake, mali pamoja na pesa taslimu sh.bilioni 3 na million 200 na kisha kukimbilia kula maisha nchini Tanzania.
Baada ya maongezi Joel alinionyesha ile picha ambayo awali alitaka kunionyesha wakati tukiwa ndani ya ndege lakini kitendo cha mpenzi wake kuamka usingizini kilimzuia asinionyeshe.
“This is fucking bastard who kill my father” aliniambia huku akinikabidhi picha.
“Oh shit I know this bastard”
Nilimwambia Joel baada ya kuipokea na kuitazama ile picha.
Ilikua ni kama mchezo wa kuigiza, huwezi amini mwanaume niliyemuona kwenye ile picha ndiye yuleyule mwanaume niliyemuona akiwa amekumbatiana na mke wangu Tressy pamoja na yule mtoto niliyemucha kipindi kile nikienda masomoni nchini China, ambaye mpaka muda huo sikua na imani tena kama alikua mwanangu.
“I know this motherfucker” nilirudia tena kumwambia Joel, safari hii sauti ilikua kubwa tofauti na awali.
Niliona ni kama Joel anachelewa kuniamini nilichukua laptop yangu kwenye begi, niliiwasha nikaiunganisha na mtandao kisha nikafungua ukurasa wa facebook, nilienda moja kwa moja kwenye profile la mke wangu na kuanza kumuonyesha zile picha alizo upload mke wangu Tressy akiwa na mwanaume huyo.
Alikua mtu mmoja, haikuhitaji hata akili za chekechea kuligundua hilo.
“How do you know him? and who is that woman?” Joel aliniuliza.
“Huyu mshenzi anaitwa Motemapembe ndiye niliyekuambia habari zake. Ndiye aliyeyanunua makampuni yangu yote kutoka kwa mke wangu na huyu mwanamke ndiye mke wangu aliyeyauza makampuni hayo kwa huyu mshenzi lakini sikua nikijua kama walikua na uhusiano wa kimapenzi na mke wangu mpaka siku ile kwenye ndege nilipoanza kuhisi kuwa huenda mimi na wewe tukawa kwenye mission ya kumtafuta mtu mmoja.
Nilizidi kumwambia Joel ambaye muda wote huo alikua akinisikiliza huku akitingisha kichwa kuashiria kuwa alikua amenielewa yote niliyokua nimemwambia.
“I get you Mr. Davis so where can we find this son of bitch?”
Joel aliniuliza huku akinitegemea sana mimi kwa sababu ya ugeni wake nchini Tanzania kwani hakua amewahi kuja hapo awali.
“Kuna mtu ninadhani anaweza kutusiaidia kwa asilimia 100 jinsi ya kumpata huyu mwanaharamu” nilimwambia Joel, bila kusema neno alisimama.
“Why you waste time stand up and let’s go to that person” aliniambia huku akitamani kuniinua.
Nilikua na hamu ya kumtia Motemapembe mikononi mwangu nimchape vibao vya ndala kabla kufikiria adhabu ya kumpa, lakini kitendo cha Joel kuinuka mapema kilionyesha hamu na kiu yake kubwa ya kumkata huyo mwanaharamu kuliko yangu.
Kama mlinzi anavyoisubiria asubuhi kwa hamu, ndivyo Joel alivyokua na hamu ya kumtia mikononi Motemapembe. Kitendo cha wazungu kujali muda kilifanya Joel aniharakishe kwenda kwa yule mtu niliyemuambia huenda angetusaidia kupata mahala pa kuanzia kumsaka huyo mshenzi Motemapembe.
“What about your girl” (Vipi kuhusu msichana wako) nilimuuliza.
“My late father is more important than her” (Marehemu baba yangu ni muhimu kuliko yeye) alinijibu.
Sikua na swali tena wala pingamizi lolote. Bila kupoteza muda tulitoka pamoja ndani ya ile bar na kuelekea sehemu yalipokuwepo maegesho ya magari. Tulitumia lile lile gari nililoenda nalo, niliungurumisha injini nikaingiza gia kisha safari ya kuelekea kwa yule mtu niliedhani angeweza kutusaidia mimi na Joel kupata mahala pa kuanzia kumtafuta yule mwanaharamu kutoka Kongo .
Ilikua kama muvi ya kutisha, ndani ya gari hakuna aliyemuongelesha mwenzake, Joel alikua bize kuichunguza Dar es salaam na mimi nilikua bize kuendesha chombo, mikono ilicheza na gia na usukani wakati miguu ilicheza na breki na mafuta.
Speed niliyoondoka haikua ya kawaidia, ilikua kama picha la kutisha kama ungetuona ungesema hollywood imehamia bongo maana mwendo ulikua mkali kama majambazi waliopora bank na kuanza kufukuzana na ma askari.
Tulikua tunarudi nilipotoka, mbezi beach kwa Mzee Ambrosi yule jirani yangu mkubwa aliyekuepo karibu kabisa na ile nyumba yangu ya kifahari ambayo Tressy alikua ameiuza.
Sehemu ya Nne (4) I Will be Back
- 97shares
- Facebook43
- Twitter54
- Gmail
- Copy Link