in

IMANI INAYOWEZA KUFUFUA: SIMULIZI ZA MAISHA

Imani Inayoweza Kufufua ni Simulizi ya Maisha inayo Fundisha Masuala Mbalimbali yatakayo Kusaidia Katika Kukabiliana na Changamoto za Kila Siku Kwenye Maisha Yetu. Soma Mpaka Mwisho Simulizi ya Imani Inayoweza Kufufua Kufahamu Yaliyo Jiri.

Imani Inayoweza Kufufua

SIMULIZI ZA MAISHA: IMANI INAYOWEZA KUFUFUA

Baba mmoja alikuwa akila chakula kwa furaha na mke wake ambaye alikuwa siku za mwisho akijitazamia kabla ya kujifungua mtoto wao wa kwanza. Mara mama akaanza kulalalamika maumivu ya kichwa na baba akaita gari na wakiwa njiani kuelekea hospitali yule mama akafariki.

Walipofika hospitali baba akaomba mama afanyiwe upasuaji wa haraka ili waone kama mtoto aliyekuwa tumboni angeweza kupona.

Baada ya upasuaji wa haraka mtoto alitoka akiwa mzima na madaktari wakiwa wanashangaa baba aliendelea kuomba kwa Mungu akisema;

“Eeh Mungu kama umeweza kumwokoa mtoto huyu naamini pia waweza kuurejesha uzima wa mama yake kwani kimekuwa ni kifo cha ghafla nisichokielewa.
Ikiwa ni mapenzi yako naomba mke wangu kipenzi apone na kumshuhudia mwanae aliyemgojea kwa siku nyingi na hamu tele.
Ninaomba nikiamini kuwa wewe ni Mungu wa miujiza na mwenye huruma kwa sisi watoto wako

“AMEN”

Jopo la madaktari waliokuwa wakimsaidia yule mama wakaanza kushangaa kwa mbali mama mapigo ya moyo yakaanza kurudi na baada ya jitihada mama alipona na kila mtu mule ndani aliushangaa ule muujiza huku wakiwa na mshtuko wa kamshukuru Mungu.
Sasa naomba nawe usikie maneno haya kwa makini:

*Mungu akupe wepesi, amani na furaha kwa kila tatizo litakaloyasibu maisha yako

  • Kamwe usichoke kumwomba Mungu hata kwa jambo unaloliona machoni mwako haliwezekani, kwani kwa Mungu hakuna linaloshindikana
  • Kuanzia leo katika kila jambo uliloliona kuwa gumu kwako litakuja kuwa rahisi na liwezekanalo
  • Kwa kila jambo lililokuwa likichelewa katika maisha yako kuanzia sasa litaanza kwenda haraka nawe utashangaa ukuu wa Mungu.
  • Utafurahia mafanikio ya kila jambo na ukishuhudia miujiza katika maisha tyako.

MWISHO.

Na Huo Ndio Mwisho Wasimulizi yetu ya Imani Inayoweza Kufufua, Natumaini Umejifunza Jambo Kubwa Katika Simulizi Hii. Niandikie Maoni yako Hapo Chini Kwenye Comment Nami nitakujibu.

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Malipo ni Hapahapa Duniani

MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI: SIMULIZI MPYA

Usimtukane Mamba Kabla Hujavuka Mto

USIMTUKANE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO