Hadithi ya joka lenye vichwa Saba. wengi wetu tukiwa wadogo tulishawahi kusimuliwa hadithi nyingi shuleni na wanafunzi wenzetu hata nyumbani na wazazi, kaka na dada zetu.
basi leo tunakwenda kusimuliwa hadithi nzuri inayo muhusu nyoka mwenye vichwa saba, na atakaye tusimulia simulizi ni Mzee Hassan Mambo Kombo.
HADITHI YA JOKA LENYE VICHWA SABA.
Hapo zamani za kale palikuwepo na visima, baadhi ya siku vilikuwa vinakauka maji kama kule Same kwa nao pafahamu, watu wanakosa maji, na kule kwenye kisima cha Uwamba hakukauki maji lakini hakwendeki kuna nyoka mkubwa, na nyoka huyo ana vichwa saba. Hakwendeki, kila mtu anaogopa.
Wanakijijiwakasema sasamaji hatuna tutafanya nini?
Kwa bahati walihamia watu, wakazaa mpaka na wao wakafa, wakabakia watoto wao wawili Makame na Miza. Lile joka likaja kumposa Miza hapo wakaulizana si ataenda kumla huyu, wakamruhusu kwanza aende, wakabakia kushauriana.
Joka lile likarudi, wakaamua bora wakubali ili wayapate yale maji, wengine walipinga kwa kuhofia kuliwa mtoto wao, hadi siku ya saba wakakubali na harusi ikapangwa. Siku ya harusi kuwadia kucha hawakulala, wakachimba shimo kubwa likajazwa kuni na juu likazibwa vizuri bila kujua kwamba pana shimo na harusi ilipangwa saa nne. Ilipotimia saa tatu ulikolezwa moto.
Karibu ya lile shimo aliwekwa bibi harusi na pale kwenye shimo pakatandikwa mikeka mizuri kwa ajili ya bwana harusi. Alipokuja tu bwana arusi akakaa na bibi harusi na bibi harusi akaanza kusema:
” Huja masikini bwana wangu hujaaa weee huja
Nipe pete yangu, moja hujaaa weee huja
Nikuoneshe mguu wako, hujaaa weee huja “
Na joka likaitikia:
“Huja weee masikini bibi yangu hujaaa weee huja Shika pete yako moja, hujaaa weee huja Unioneshe mguu wangu, hujaaa weee huja” Joka likatoa pete na yule bibi harusi akaimba tena: “Huja weee masikini huja bwana yangu hujaaa weee huja Nipe pete yangu, moja hujaaa weee huja Nikuoneshe mkono wako, hujaaa weee huja “
Na joka likaitikia:
Huja weee huja masikini bibi wangu hujaaa weee huja
Shika pete yako moja, hujaaa weee huja
Unioneshe mkono wangu, hujaaa weee huja
Hapo akafunuliwa mkono wake na akapewa pete.
Huja weee huja Masikini bibi yangu hujaaa weee huja
Nipe pete yangu, moja hujaaa weee huja
Nikuoneshe sikio lako hujaaa weee huja
Huja wee huja Masikini bibi yangu hujaaa weee huja
Shika pete yako moja, hujaaa weee huja
Unionesh, Masikini bwana wangu hujaaa weee huja
Nipe pete yangu moja, hujaaa weee hujaaa
Nikuoneshe uso e sikio langu hujaaa weee huja
Akapeleka pete ile akaoneshwa shikio. Akaendelea kuimba na bibi akaitikia:
Hujaaa weee hujaaa wako, hujaaa weee hujaaa
Tayari moto ukaanza kumpata akaanza kuomba maji ya kunywa.
Nikuoneshe uso wako hujaaa weee hujaaa
Na yeye akaitikia.
Huja weee hujaaa masikini bibi wangu hujaaa weee hujaaa
Shika pete yako moja, hujaaa weee hujaaa
Unioneshe uso wangu, hujaaa weee hujaaa
Kuomba tena maji ya kunywa. Akaendelea kuimba tena.
Hujaaa weee hujaaa, Masikini bwana wangu hujaaa weee hujaaa
Nipe pete yangu moja, hujaaa weee huja
Nikuoneshe nywele zako, hujaaa weee hujaaa
Na yeye akaitikia kwa sauti ya chini, joto lilikuwa lishampata.
Masikini bibi yangu, hujaaa weee huja
Shika pete ylako moja, hujaaa weee hujaaa
Nikuoneshe nywele zak,o hujaaa weee hujaaa
Akapeleka pete na hapo ikawa tayari amekwishachoka anatapatapa akajitumbwikiza kwenye moto.
Hapo watu wote wakakusanyika wakaanza kumfukia kwa dongo na mawe mpaka likawa halionekani. Na wakafurahi kwa mpango wao kufanikiwa na wakaanza kutumia maji bila ya hofu.
MWISHO
Na huo ndio mwisho wa Hadithi ya Joka lenye Vichwa Saba.
Dah! kiukweli nimekipenda hicho kiitikio 🎵”Hujaaa weee juja”🎵 . Navutapicha kama nimesha wahi kusikia Njimbo moja apa Bongo Chorus kama hii 😉.
Niandikie hapo chini kwenye comment, ya kwamba umejifunza nini.. pia sio vibaya kama uta share simulizi hii kwa wengine nao wapate kujifunza na kufurahi…
- 176shares
- Facebook108
- Twitter68
- Gmail
- Copy Link