in

LITAKUJA KUFA JITU: Haya Matambo Ifike Mahali Tuache

Tazama Matokeo Hapa

Download Mitihani

Litakuja Kufa jitu apa, Haya matambo Tuache jamani. maana litakuja kufa jitu kwa Presha Bure Kisa Matambo yasiyo kuwa na Maana. Soma Hadi Mwisho kisa ichi utafahamu kilicho Mkuta Huyu mjumbe.

Usisahau kuni Follow @japhary kwa Vichekesho na Mada Mbalimbali za Kuvutia. 😊

VITUKO - HAYA MATAMBO TUACHE

HAYA MATAMBO TUACHE JAMANI.

Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Huku Jijini Dar es Salaam. Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini. na kufungua Ofisi yake inayo jiusisha na Masuala ya huduma Kwa Wateja, masuala ya Kesi kesi.

Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona Mtoto Mmoja Mrembo haijapata Kutokea machoni kwake. Akiwa anakuja ofisini kwake, akajua ni mteja anamletea kesi. Ndipo akanyanyua mkonga wa simu yake ya Mezani Kutoka TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti.

Wakati mdada Huyo alipokaribia Rwegashora alimkaribisha kwa ishara maana alijifanya yupo busy na kuongea na simu kiasi Kwamba asingeweza Kuzungumza Nae.

Wakati anaongea na simu, Ghafla Jamaa akaanza Kuongea Kimombo No, No, No… Absolutely No. Wajuulishe hao lay person wa New York kua siwezi kushuhulika na kesi ambayo itanilipa chini ya 50 million Tsh.

Mimi ni professional lawyer and am crossing the border to sarve international community. Aka pose kidogo, na akanywa maji kisha akaendelea…

Naweza kuanza kukusanya primary evidence next weak but tell them watume kwanza ten million Kama Advance payment… Hahahahaha you dont know my Account Mr Roger. Ok waambie watume kwenye Account ileile walionitumia million 100 last month… Aka pose tena akameza fundo la maji na kurekebisha tai yake kisha akaendelea…

Ok usisahau kumueleza muendesha mashtaka mkuu wa marekani kua nitakuja New York mwezi ujao. maana nitapita kwanza Amsterdam kuwasilisha utetezi wa yule mteja wangu mholanzi. kisha nitaenda Tokyo kulipia ile gari yangu niloagiza.

Wakati anaongea hayo yote yule Mrembo alikua ametulia na anamuangalia Tu Bwana Rwegashora anavyojizunguusha kwenye kiti chake huku akiongea kwa Mbwembwe kwenye ile simu yake ya TTCL. Litakuja Kufa jitu apa

Baada ya kumaliza kuongea na simu Bwana Rwegashora aliweka mkono wa simu yake ya TTCL chini kisha akamgeukia mdada mrembo. Samahani sana kwa kukupotezea muda wako.

unajua tena kazi zetu zinaumiza kichwa sana kama unavyoona mwenyewe yaani niko busy sana.

Ninapokea simu sana mpaka nimechoka na simu nyingi ni za wateja wa nje ya nchi. Anyway nikusaidie nini..? Mdada akajibu mimi ni mfanyakazi wa kampuni ya TTCL nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani tangu wiki iliyopita…!!! naleo ndoNimeagizwa kuja kushuhulikia Tatizo lako uliliwasilisha Kwetu.

Unaambiwa Bwana Rwegashora Baada ya kusikia Hivyo, Alizimia. Sasa Hivi yupo Hospitali. Sijui itakua ni ile pesa yake aliyokuwa akiongelea Wamechelewesha au 🤔.

Mjumbe Kaumbuka hivihivi. Haya matambo jamani tuache, Kwani utakufa usipo Fake Maisha. Embu tuambiane Hapo Kwenye Comment. Hii Mambo imekaaje kuhusu Kufake Uhalisia wa maisha yetu.

Nijulishe Hapo Chini Kwenye Comment ungependa Vituko kama Hivi, au Kwenye Hivi Vichekesho tuongeze Kipi Tu Punguze Kipi. Nawatakia Tabasamu lenye furaha 😊😊.

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

KICHEKESHO - HII KITAALAMU TUNAITAJE

HII KITAALAMU TUNAITAJE?: Maana Nimebaki Sielewi 🤨.

HUYO TOTAL ATALIPA MWENYEWE - VICHEKESHO

TOTAL ATALIPA MWENYEWE: VICHEKESHO VUNJA MBAVU.