in

MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI: SIMULIZI MPYA

Malipo ni Hapahapa Duniani, Simulizi Mpya Kutoka Africona na Mtunzi Wako ni Mimi Aisha Mapepe. Soma Mpaka Mwisho Simulizi Hii Kufahamu ni Kipi Kilicho Jiri Ndani ya Simulizi Hii Mpya na Nzuri.

Malipo ni Hapahapa Duniani

SIMULIZI MPYA FUPI: MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI

Katika Mji wa Arusha Mtaa wa Kaloleni ni eneo ambalo wakazi mbalimbali walipendelea sana kuishi kutokana na mazingira yake kuwa tulivu na yenye mandhari nzuri. Katika mtaa huo aliishi mzee mmoja aiitwaye Magesa. Mzee huyo alikuwa na mke na watoto watatu, watoto wawili wakiume ambao waliitwa Joseph na Peter na mtoto mmoja wa kike aliyeitwa Julieth.

Mzee Magesa hakuwa na uwezo mkubwa sana kifedha. Maisha ya Mzee huyo na famila yake yalitegemea sana kipato kidogo kilichotokana na biashara ya kuuza mboga sokoni ambayo alikuwa anaifanya siku zote za maisha yake hadi akapewa jina la ‘Muuza mboga’. Mke wake alikuwa ni mama wa nyumbani akijishughulisha na kupika chapati na kuuza ili kuongeza kipato kwa ajili ya mahitaji ya pale nyumbani.

Maisha yalikuwa magumu sana lakini familia ilikuwa na furaha na upendo kwani waliishi kwa kupendana na kuheshimiana. Mzee Magesa aliwapenda sana watoto wake, kwani mara nyingi alikuwa akiwafundisha mambo mbalimbali kuhusu maisha ikiwa ni pamoja na kuwasisitiza kusoma. Julieth alikuwa Darasa la Tano na mdogo wake Joseph alikuwa Darasa la Pili, Peter yeye alikuwa hajaanza shule.

Siku moja yapata saa mbili usiku Mzee Magesa akiwa amekaa kwenye sebule karibu na chumba chake cha kulala alimwita Julieth kwa ajili ya mazungumzo.
“Julieth!” Mzee Magesa aliita kwa nguvu. “Abee baba!” Aliitikia Julieth aliyekuwa anaosha vyombo huku akimwendea baba yake.

****** Malipo ni Hapahapa Duniani

“Unafanya nini saa hizi?” Mzee Magesa aliuliza kwa sauti ya upole.
“Naosha vyombo baba.” Alijibu Julieth kwa adabu.
“Umemaliza?” Aliuliza tena Mzee Magesa.
“Hapana baba, bado sufuria mbili.” Alijibu Julieth.
“Acha utamalizia kesho kaa hapo nina maongezi na wewe.” Aliongea Mzee
Magesa huku akinyoosha kidole kwenye kiti cha miguu mitatu.
“Nimekuita ili kukwambia maneno machache kuhusu hali ya maisha yetu
hapa nyumbani.” Mzee Magesa alianza kueleza sababu ya wito huku
Julieth akimwangalia na kumsikiliza baba yake kwa makini.

“Kama unavyoona hali yetu ya maisha tunayoishi ni ngumu sana. Na hii
inatokana na kipato chetu kuwa kidogo. Namna pekee ya kujikwamua na
hali hii ni wewe mtoto wetu mkubwa kusoma kwa bidii ili uje utusaidie
sisi wazazi wako pamoja na wadogo zako. Na pia …” Mzee Magesa
alikatisha ghafla huku akiwa kama amekumbuka kitu fulani muhimu.

“Mama yako yuko wapi?”

Malipo ni Hapahapa Duniani Sehemu Inayofuata, Bonyeza Iyo Button iliyo andikwa Next Kusoma Kipande Kinacho Fuata.

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

DAWA YAKE NDOGO SANA: SIMULIZI FUPI

Imani Inayoweza Kufufua

IMANI INAYOWEZA KUFUFUA: SIMULIZI ZA MAISHA