in

MAMA USILIE: SIMULIZI ZA KUSISIMUA NA KUFUNDISHA

Mama Usilie ni Simulizi ya Kufundisha na Pia ina Burudisha Sana. Soma Mpaka Mwisho Kufahamu Sababu ya Msemo Neno Hili “Mama Usilie“. Mwandishi Wako ni Yule yule Aisha Mapepe.

Mama Usilie Simulizi

SIMULIZI FUPI: MAMA USILIE.

Alisimama mbele ya kioo chenye urefu sawa na urefu wake. Urefu wa futi tano na pointi nane, akijitazama kwa tabasamu dhoofu.

“Ondoka kwangu malaya mkubwa wewe”

Ikawa ni sauti iliyomjia kichwani mwake kama mawimbi, ghafla. Aliubandua uso wake kwenye kioo alichokuwa akikitazama, akaupeleka kwenye tumbo lake lililoumuka.
Bado urembo haukupotea.

Upande wa kushoto ukatuna ghafla kuonesha mtoto anacheza. Kidogo akaonesha tabasamu, sauti ile mbaya ikajirudia tena kichwani mwake, lakini kwa maneno mengine mabaya zaidi

“Toka bwana na kitambi chako. Mpelekee hawara uliyelala naye wakati mimi sipo nyumbani”
‘Hawara gani? Ina maana mimi nimekuwa mpumbavu kulala njaa nikimsubiri alipokuwa akisafiri na gari zake hata miezi mingi huku akiwa ameniachia fedha isiyotosha hata wiki?

Nimekuwa mpumbavu nilipokuwa nikiwakataa rafikize kulinda heshima yake?

Leo mvulana aliyeujua usichana wangu akanifanya nimdharau mama yangu, nisimsikilize baba yangu akanipachika ujauzito ulionifanya nifukuzwe shule; leo kaniita mimi malaya?

N’na hawara? Yupi basi, Festo mpenzi nieleze’ Alipohisi kama kuna kitu kimemkaba, aliweka kituo na kumeza donge la mate kwa uchungu. Akatazama uso wake kwenye kioo uliomtazama yeye. Machozi yalitosha kudhihirisha uchungu aliokuwa nao moyoni.

Teke lingine likapigwa katika tumbo lake na kitu mithiri ya goti la mtoto mdogo, likajitokeza wazi tumboni mwake. Nancy akakisugua kichuguu kile, huku tabasamu lililoporomosha machozi likiwa limedhihaki maana halisi ya furaha.

Ilionekana mtoto alitaka kutoka. Nancy akakunja sura. Akakunja midomo kwa kuiuma na meno. Mkono wa kulia ukiwa unasugua tumbo lake lililovimba wa kushoto ukawa unafinya mito ukafinya mashuka akajipiga mapajani mwisho akapiga yowe hafifu.
“Anhaa!!”
Uchungu.

Maji mazito yakamtoka katikati ya mapaja yake na kumwagikia sakafuni.

Ni hapo Nancy alipofahamu kuwa muda wa kujifungua umefika. Msichana aliyemsaidia kumpa hifadhi ndani ya nyumba yao, alikuwa nyuma ya mlango wa chumba alichokuwako Nancy, akishusha kitasa. Baada ya kufungua kitasa na kujitoma ndani, hali haikuridhisha.

Mapaja ya Nancy yalikwisha tapakaa damu na maji mazito ambayo wazazi husema “chupa imepasuka”.
Immaculata binti wa mzee John Mdobe mwenye umri wa miaka 28, miaka 15 zaidi ya Nancy aliyekuwa akiugulia maumivu ya uzazi sakafuni.

Alihaha akimpigia dereva wao kuleta gari karibu na mlango. Kisha akambeba Nancy aliyelegea wala asiweze kujisogeza japo kwa hatua moja.
“Jikaze Nancy, Jikaze mdogo wangu” Wakafika ndani ya gari na dereva alikuwa mzuri katika kukimbiza gari, huku akipuliza selo za uhakika. Gurudumu za gari hiyo, zikalalama gari likayumba, wala sauti ya Immaculata haikufua dafu.

“Juma punguza mwendo bwana!!!”

Alibwata, lakini juma alipachika gia hii akaichomeka ile na ile ilipokubali gari likayoyoma mpaka hospitali ya taifa muhimbili. Machela zikaletwa mbio mbio baada ya gari hilo aina ya landcruser kuonekana likija mbio. Wauguzi wakasaidiana kum’beba Nancy na kumpandisha kwenye machela ile.

Huku wakiwa ndio kwanza wameupita mlango na kuingia kwenye korido la vyumba vya hospitali Nancy akasikika akilalama. “Siwezi! Siwezi tena” Uchafu fulani ukatoka katikati ya mapaja yake, kisha kikafuata kichwa kilichokikaribisha mabega.

Wauguzi wakapigiana kelele.
“Anajifungua! Anajifungua jamani”
Nancy alikuwa amevaa gauni pana jepesi bila nguo nyingine yeyote ndani ikawa rahisi kwake kujifungua.

Wauguzi wakisaidiwa na daktari maalumu wa shughuli hizo, wakamsaidia Nancy kujifungua. Nancy akapata mtoto wa kiume, baada ya kujifungua akazimia. Dripu tatu za maji zilizoteremshwa katika mishipa yake, zikampa nguvu tena ya kuamka kama aliyewehuka.

“Yuko wapi mwanangu!? Namtaka mwanangu”
Pembeni yake alikuwako Immaculata aliyesimama zaidi ya masaa matatu akimsubiri kuamka.

Alionesha furaha alipomuona Nancy ameamka.

Dokta naye alikuja alipoambiwa kuwa mgonjwa ameamka. Akampima visivyoeleweka kisha Nancy akaruhusiwa kupewa mtoto wake.
“Mpeni mtoto wake amnyonyeshe” Nancy akafurahi kumshika mikononi mwake.

Mtoto aliyefanana riyali ya kwanza kwa ya pili na Festo. Chozi likamtoka tena.
“Nancy ina maana hujamfurahia hata mtoto wako pia mdogo wangu?”
“Hapana si hivyo dada, ni huyu mtoto amefanana kabisa na Festo baba yake! Wanaume hawa jamani?” “Basi usilie Nancy”

Alipomaliza kumnyonyesha, Immaculata alirudi nyumbani kuchukua mtori ambao Juma alipewa maelekezo ya kutengeneza kwa ajili ya mzazi. Immaculata aliporudi Nancy akaunywa kwa bakuli mbili na kuridhika.

Siku ya pili wakaruhusiwa kutoka baada ya Nancy kutoonesha matatizo yoyote ya kuendelea kumuweka hospitalini hapo. Wakiwa wanatoka katika geti la hospitali ya muhimbili, Juma akiwa anaendesha Immaculata alishuka kabla hawajaingia barabarani.

“Naenda kununua vocha”

Ilimbidi kuvuka barabara na kuelekea upande wa pili wa maduka. Akanunua vocha aliyohitaji na kuanza kuikwangua huku akitembea taratibu. Nancy akiwa na mtoto wake aliyekuwa akilialia ndani ya gari, Juma akichezea funguo yake ya gheto; sauti ya kishindo kikubwa cha gari lililoserereka kwa mida mrefu na kukumbana na kitu kilicholeta taharuki hiyo kikawashitua.

Juma alikuwa wa kwanza kuona mwili wa mtu aliyedondoka chini mbele ya gari ndogo lililobonyea kidogo kwa mbele huku yule mtu akitokwa na damu nyingi sehemu ya kichwa. Ajali hiyo ilitokea mita chache kutoka pale walipo. Mtu yule aliyeikumbatia sakafu ni yule waliyekuwa naye ndani ya gari mnuda mchache.

“Kuna nini kaka Juma!?” Nancy akauliza kwa hofu huku kilio cha mtoto yule kikizidi ndani ya gari. “Immaculata”
Juma aliweza kukisema kitu hicho pekee huku macho ya hofu na uoga yakimtoka pima sanjari na mapigo ya moyo yaliyokuwa yakimuenda mbio.

Immaculata akawa amefariki pale pale barabarani kwa kupasuka kichwa baada ya kichwa chake kujipigiza kwenye barabara.

Zikaja siku mbaya kwa Nancy. Mzee John hakujali miezi mitatu ya mtoto wa Nancy aliyeitwa jina la Moshi, bali yeye alimtaka Nancy.

Alimtaka kutembea naye kwa kisingizio mke wake amekwishafariki miaka mingi iliyopita. Hakujali kuwa Nancy hakuwa na tofauti yoyote na Immaculata binti yake. Kuna wakati mpaka mwanaume yule asiye na haya akamtisha kumuua kwa panga kama akiendelea kusimamia msimamo wake wa kumkataa.

“Nitakuua wewe na kifaranga chako kama unashindwa kunifadhili kwa wema wangu”
Hakuona aibu hata chembe. Nancy hakuhadaika akaendelea kusimamia msimamo wake.

Kuna siku ikambidi yeye Nancy na Moshi kulala ndani ya pipa baada ya kuonekana John kuwa na lengo la kutaka kutimiza alilomuahidi Nancy kuwa atamuua kwa panga.

Nancy akaona sehemu hiyo haifai. Moshi alipotimiza mwaka mmoja na miezi michache, akaondoka nyumbani kwa John, sinza vatican asijue aelekeako.

Maisha ya Nancy yakawa mabovu kupita kiasi.

Hakuwa na pa kulala wala chakula. Alihifadhi mbavu zake zisipigwe na baridi kwa maboksi huku akiwa amezilaza juu ya zege kavu ndani ya pegare moja lililotelekezwa.

Nancy aliweza kumudu gharama mbalimbali za maisha na kuhusu chakula kwa kuuza mwili wake kwa bei nafuu. Hakuhitaji kumpeleka Moshi mbali pale ambapo mtoto huyo alikuwa bado hajalala. Hakuwa na wa kumwachia pale aingiapo katika biashara yake ya Ngono.

Kuna wakati alikuwa akilia wakati akimuhudumia mteja akamnyakua Moshi na kimnyonesha. Alijua yalikuwa ni mateso aliyompa mtoto wake, lakini hakuwa na pesa za kumuwezesha kuchukua chumba kwenye vyumba vya kulala wageni na hakupenda kumtupa Moshi.

“Nitakulea kwa nguvu zangu zote kwa kuwa nakupenda sana mwanangu”

Nancy hakuacha kulia. Uzuri wake ukafifia kadri siku zilivyozidi kwenda. Alitamani ajiue lakini kila alipomfikiria Moshi, aliifungua kamna aliyoifunga juu ya mchikichi alioaka kujitundika.

Hakuwa tena mwanamke aliyetamanisha. Maziwa yake yakalala kama lapa bovu na kuchakaa huku marapurapu aliyoyaona kama nguo yakaficha uzuri aliobarikiwa na rabuka. Uso ulionawiri hapo mwanzo ukafifia kwa makunyanzi na mawazo ya jinsi ya kumlea mtoto wake.

Baada ya kuona soko lake likianza kupukutika, akajiuliza nini sababu. Mmoja siku moja akaja na jibu. “Nataka nyuma, mbele sisikii raha. Ntakupatia sh’ng efu tano badala ya efu moja” Nancy akajisikia raha sana kwa kiwango kikubwa kama hicho cha fedha alichotajiwa.

Akakubali bila hajizi bila kujua mwanaume yule alikuwa mwizi. “Pesa yangu iko wapi?” “Toka zako ina maana wewe huna stafu? Basi nikopeshe” Akaondoka bila kumsikiliza kama Nancy amekubali au lah! Moshi akawa mkubwa akawa miongoni mwa machokoraa waliotafuta vyupa jalalani na kuuza kwa wahindi.

Huko ndipo aliweza kusikia mengi ambayo alikuwa hayajui kuhusu mama yake.

Huenda hata kama alikuwa akijua, hayakumuumiza kama alivyokuwa akiambiwa na rafiki zake. Akarudi nyumbani alipokuwa akiishi na mama yake tofauti na kawaida yake. Nyumba haikuwa nyumba, ilikuwa danghuro.

Uzuri siki hiyo Nancy hakuwa akihudumia mteja yeyote. Moshi hakuwa akijua chochote kwa kuwa mama yake alimdanganya wale ni rafiki zake. Lakini kwa bahati mbaya alimkuta mama yake akiwa hoi kitandani.

Pembeni alikuwa na kopo lililojaa mchanga na lenye mate mengi tofauti na makohozi. Moshi hakujali kumuangalia mama yake aliye hoi kitandani akachukua nguo zake na kutaka kutoka nje, Nancy akamuita. “Moshi!?” “Unasemaje we malaya?” Neno alilotamka Moshi likamchoma sana Nancy.

Nancy akapiga moyo konde akajikaza na kujiinua kwa maumivu makali.

“Nilijua ipo siku utanitukana matusi yote unayoyajua hapa duniani lakini mwanangu nilikupenda ndio maana niliamua kufanya kazi hii ili usife njaa na uishi maisha ya afadhali” Nancy akaanza kulia.

Alipoona Moshi akiwa anamtazama asielewe nini alikuwa anaambiwa, akamdadavulia kwa kumuelezea kisa kizima kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Nancy akaendelea kulia kwa uchungu huku Moshi naye akiwa analia zaidi kumpita.

“Mama usilie, nakupenda sana mama yangu. Nisamehe mama yangu sikujua kama unakufa kwa ajili yangu pole sana mama. Usilie maam yangu” Kukawa na maombolezo yaliyowafanya kila mmoja kushindwa kum’bembeleza mwenzake bali kumzidishia kilio. Miezi miwili baadaye, Nancy akaaga dunia kwa ugonjwa wa ukimwi huku uti wake wa mgongo ukiwa umejaa maji kwa mapenzi ya kinyume na maumbile.

Nancy alikufa kwa ajili ya UKIMWI akiwa na miaka 23 pekee. Uzuri wake ukapotelea kwenye kazi haramu za kuuza mwili wake kwa sababu ya kumpatia Moshi maisha bora. Nani kama mama? Nani kama mwanamke aliyekuleta duniani?

MWISHO

Ni wangapi wameaharibu uzuri wao kwa sababu ya watoto wao? Wapo wengi walio jinyima maisha kwa sababu ya watoto wao. Kila mmoja ampende na kumuheshimu sana mama yake.

Na Huo ndio Mwisho wa Simulizi yetu Hii Nzuri ya Kusisimua na Kufundisha Sana. Jamani Aisha Sio Kila Wakati nina andikaga Maupuuzi Kuna Wakati naelimisha Kama Ukiwa Mjanja Kwenye Simulizi Zangu Utagundua Kuna Somo natoa. Niandikie Maoni yako Hapo Chini Kwenye Comment.

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Mwanaume Mwenye Nguvu

MWANAUME MWENYE NGUVU KULIKO WOTE

History Past Papers Secondary

History Past Papers Secondary: Form Three and Four (PDF)