in

KISA CHA MWANAHARAKATI NA MFUGAJI: LAZIMA UTA CHEKA TU.

Kisa cha Mwanaharakati na Mfugaji, Lazima uta Cheka tu. Kwani Mwanaharakati Mwenyewe anasemaje..? Embu soma mpaka Mwisho utajua alicho kisema 😊.

Usisahau kuni Follow @japhary kwa Vichekesho na Mada Mbalimbali za Kuvutia. 😊

LAZIMA UCHEKE - MWANA HARAKATI NA MFUGAJI

KISA CHA MWANAHARAKATI NA MFUGAJI: LAZIMA UTA CHEKA TU.

Siku moja Kulikuwa na Mwanaharakati anatembelea Wafugaji wa Mifugo Mbalimbali. Anapitakila Nyumba Kuangalia kama Wanyama Wanaishi katika Mazingira Rafiki. Akiwa katika pitapita Zake Akakutana na Mfugaji Mmoja aliye kuwa akifuga kitifire (Nguruwe). Na Mazungumzo yao Yalikuwa Kama Hivi.

KIREFU CHA MANENO:
MH = MWANAHARAKATI.
MF = MFUGAJI.

MH: Hawa nguruwe unawalishanini..?
MF: Nawalisha mabaki ya chakula toka migahawa mbalimbali.
MH: Hayo ni makosa unawatesawanyama kwa kuwalisha chakula kichafu. Akapigwa faini…
Baada ya siku chache wakaja wanaharakati toka Umoja wa Mataifa .

MH: Hawa nguruwe unawalisha nini? .
MF: Huwa nawaanzia siku na uji wa ulezi, halafu mikate, mchana ugali kwa kabeji na usiku viazi.
MH: Loh watu wanakufa kwa njaa wewe unalisha nguruwe, akapigwa faini.
siku chache baadae wakaja wanaharakati wa Mazingira Kwa yule Mfugaji.

MH: Hawa nguruwe unawalisha nini? .
MF: (Kwanza akasita kidogo) Hawa huwa nawapa shilingi alfu tano kila mmoja kila siku. halafu wao wenyewe wanaenda kununua chakula wanachokitaka.

Baada ya kusikia hivyo, nimewaacha wanakubaliana na Yule Mwanaharakat, Kwamba Kuna uwezekano na Yeye akawa Mfugo wake. Kila Siku apate Hiyo Pesa.. Nijulishe apo chini kwenye Comment Ingekua wewe ni mwanaharakati Ungechukua hatua Gani.

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

CHEZEA MCHEPUKO WEWE - VITUKO NA NUSU

CHEZEA MICHEPUKO WEWE: Soma Maombi ya Wanandoa.