in

MWANAUME MWENYE NGUVU KULIKO WOTE

Unamfahamu Mwanaume Mwenye Nguvu Kuliko Wanaume Wote. Naongelea Mwanaume Sio Hawa Wavulana wa Dar es Salaam Wala Chips. Leo Aisha Nimeamua Kuja Kitofauti na Simulizi hii Kutoka Kwenye Bible. Najua Wengine Watashangaa Aisha Katokana Wapi na Biblia. Ndoivyo Wadau Soon Msishangae nimeokoka ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜‰.

Mwanaume Mwenye Nguvu

SIMULIZI: MWANAUME MWENYE NGUVU KULIKO WOTE

UNAJUA Jina la mwanamume mwenye nguvu kuliko wote? Ni Samsoni Mwana wa Manoa. Yehova anampa Samsoni nguvu hizo. Hata kabla ya Samsoni kuzaliwa, Yehova anamwambia mama yake hivi: โ€˜Upesi utazaa mwana. Ataongoza kuokoa Israeli kutokana na Wafilisti.โ€™

Wafilisti ni watu wabaya wanaoishi Kanaani. Wana wanajeshi wengi, na wanawaumiza Waisraeli sana. Wakati mmoja, Samsoni anapokwenda kwa Wafilisti, simba mkubwa anatokea akinguruma kukutana naye. Lakini Samsoni anamwua simba huyo kwa mikono yake tu. Pia anaua mamia ya Wafilisti wabaya.

Baadaye Samsoni anapendana na mwanamke, Delila. Viongozi Wafilisti wanaahidi kwamba kila mmoja wao atampa Delila vipande 1,100 vya fedha akiwaambia kinachompa Samsoni nguvu nyingi hivyo. Delila anataka fedha zote hizo. Yeye si rafiki wa kweli wa Samsoni, wala wa watu wa Mungu. Anazidi kumwuliza Samsoni kinachompa nguvu nyingi hivyo.

Mwishowe, Delila amshawishi Samsoni. Naye Samsoni anamwambia siri ya nguvu zake, akisema: โ€˜Mimi sijanyolewa nywele. Tangu kuzaliwa kwangu, Mungu alinichagua niwe mtumishi wake wa pekee, yaani, Mnadhiri. Nikinyolewa nywele, nitapoteza nguvu.โ€™

Delila anapojua hayo, anamlaza Samsoni katika paja lake. Kisha amwita mtu aje amnyoe nywele. Samsoni anapoamka, anakuta amepoteza nguvu. Ndipo Wafilisti wanakuja kumkamata. Wanamwondoa macho yake mawili, na kumfanya mtumwa wao.

Siku moja Wafilisti wanafanya karamu kubwa ili waabudu Dagoni mungu wao. Wanamtoa Samsoni gerezani ili wamcheke. Wakati huo, nywele za Samsoni zimekua tena. Samsoni anamwambia kijana anayemwongoza kwa mkono:

โ€˜Acha nishike nguzo za jengo hili.โ€™ Kisha Samsoni anamwomba Yehova ampe nguvu, naye anashika nguzo hizo. Anapaza sauti hivi: โ€˜Acha nife pamoja na Wafilisti.โ€™ Wafilisti wanaokula karamu ni 3,000. Samsoni anapoegemea nguzo hizo, jengo laanguka na kuua watu wote hao wabaya.
Waamuzi sura ya 13 mpaka 16.

Kwa Muendelezo wa Hadithi Nzuri za MUNGU Kama Hizi. Tembelea Biblia au Quran Kwa Hadithi Zenye Mafundisho ya Kukupa Imani.

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Architectural Drawing PAST PAPERS AND NOTES FOR DSEE

ARCHITECTURAL DRAWING PAST PAPERS DTEE: Free (PDF)

Mama Usilie Simulizi

MAMA USILIE: SIMULIZI ZA KUSISIMUA NA KUFUNDISHA