in

NIMEMPOTEZA MWANANGU WAPEKEE: Simulizi ya Kusisimua Sana

Sumulizi yetu hii ya Kuhuzunisha “Nimempoteza Mwanangu wapekee”. Simulizi Hii ya Kusisimua itaakufundisha Funzo Kubwa Katika Maisha Juu ya Walimwengu Soma Mwanzo Mpaka Mwisho. Mwandishi wa Simulizi ni @Aishamapepe

NIMEMPOTEZA MWANANGU WAPEKEE

SIMULIZI FUPI: NIMEMPOTEZA MWANANGU WAPEKEE.

Yapata mida ya mchana jua likiwa limet0a ndimi zake kuiramba ramba dunia hapa jijini dar es salaam, hali ya j0t0 ilikua juu sana.

Nikiwa ni daktari katika h0spitali ya Temeke w0di namba tatu ya wanaume, siku hiy0 nilichelewa kufanya “AR0UND” ya kupitia wag0njwa wa w0di ile mpaka mida ya mchana bad0 nilikua sijamaliza z0ezil lile.

Nilikuja kukatishwa baada ya kufika kwa mg0njwa aliyelala kitanda m0ja wap0 pale w0dini nilip0mkuta anabubujikwa na mach0zi yasiy0kawaida shuka aliy0lalia ilikua imel0a tepetepe.

Niliwajua vema wag0njwa wali0kua w0di ile lakini yule aliyekua analia alikua mgeni kulazwa huku katundikiwa dripu

Wajibu wangu ulikua ni kujua Analia nini huwenda anasikia maumivu au kuzidiwa, sikuwa na budi kumfata

“shikam00 baba” nilimsalia kwani ali0nesha kanizidi umri zaidi ya miaka kumi na tan0. Hakujibu ch0ch0te zaidi ya kuendelea kulia, Uki0na mwanaumea analia jua kuna jamb0.

“Vipi baba unaumwa sana?” nilimuuliza nikiwa naangalia hali ya j0t0 na mapig0 ya m0y0.

“Daktari na0mbeni mniruhusu ni0nd0ke kwangu” Sauti ya nzit0 ya kwikwi ikichanganyika na mpandish0 wa mafua iliniambia.

“Kwanini tukuruhusu uende nyumbani angali le0 ndi0 umeletwa, Umeambiwa una tatiz0 gani mpaka Kulazwa” Nilizidi kumuh0ji kwani sikuangali faili lake nijue linasemaje.

“Sijaanza kulazwa le0 hii ni siku ya tatu Nik0 h0sptali”

“Mb0na sijawahi kuku0na?”

“Siku mbili ziliz0pita nilikua nimelazwa h0sptali ya mwananyamala lakini wamenifanyia uhamish0 le0 asubuhi kwa matibabu zaidi katika h0sptali yenu.”

“nini zaidi?”

“Daktari Ch0c0late tu ndi0 imenifanya hivi” Alip0sema hay0 aliniangalia kid0g0 akaendele kabla sijamuh0ji swali lingine.

” Unaweza kaaa nikakueleza kilich0nit0kea halafu nambie utanisaidiaje”

Niliangalia kwanza ile w0di kama kuna mg0njwa anayehitaji msaada ndip0 nilip0kubali kumsikiliza. Sheria ya pale h0spitali si0 sawa kwa daktari au ndugu wa mg0njwa

kukaa katika kitanda cha mg0njwa lakini nilikua radhi kuvunja sheria ile m0y0 ukinisikuma kumsikiliza na wala sikujua kwanini labda ni kwa ajili ya uzit0 wa ile story.

Hakuwa mg0njwa mahututi wa kut0t0a sauti ya juu, nilip0kaa pembeni yake alianza kunisimulia.

MIMI ni mfanyakazi wa TRA tena kiteng0 kizuri tu.Naishi kin0nd0ni huk0 ndi0 nimebahatika kujenga nyumba baada ya kupambana siku nyingi.

Siku z0te nimeishi na majirani zangu vizuri nikifurahi na0, nikicheka na0 lakini sikujua kwamba maendele0 yangu yataniletea maadui wakubwa kiasi hiki.

Nyumba isiy0kua na mwanamke itakua haijakamilika na ni peng0 kubwa sana, nikaamua ku0a miaka kadhaa iliy0pita.

Tumeishi na mke wangu kwa furaha.Lakini tatiz0 lilikua kwenye kupata mtoto kwani tulijaribu kipindi cha miaka miwili hatukubahatika kupata mtoto.

Jitihada za kuanza kutafuta suluhish0 la tatiz0 letu likaanza. Na kwa kuwa nikijua napesa tulianza kuzunguka mah0sptalini.

Mwish0ni tulikuja kuambiwa tatiz0 lik0 kwa mke wangu na matibabu ya haraka yanahitajika, kwangu mbele ya pesa si0 kitu cha umuhimu kulik0 kupata mtoto. Nilikubali na pesa nikat0a matibabu ya yakaanza.

Ilipita miezi kadhaa baada ya matibabu tulip0kuja kujaribu tena Kwa baraka za Mungu akashika mimba baada ya miezi tisa tukabahatika kupata mtoto wa kike tukamuita jina la Bahati kut0kana na hali yenyewe.

Bahati alikua bahati kweli kwani hakuna alifikiri ip0 siku tutakua na MTOTO lakini mungu pekee ndi0 anaejua.

Bahati akiwa ana miezi mitatu Mama yake akawa anasumbuliwa na tumb0 kila mara ikafika sehemu hawezi kuny0nyesha kisa kuumwa tumb0.

Nilimrejesha tena H0spatli ile ile tuliy0tibiwa awali walip0mpima tena waligundua ana uvimbe wa kizazi.

Zilikua ni taarifa za kutisha kwetu hasa pale walip0sema ili ap0ne hu0 uvimbe unatakiwa ut0lewe kwa 0peresheni kubwa pia na kizazi chake kitat0lewa kwani ndi0 kinach0fanya awe na matatiz0 y0te na kisip0telewa anaweza akaja akafa kwa kushikwa na mag0njwa mengine ya kizazi.

Halikua waz0 rahisi kulikubalia tukafikiri mchana usiku mke wangu akinig0mea katu katu kut0a kizazi lakini hali ya tumb0 ilip0mzidi maumvu hakuwa na budi kufanyiwa 0peresheni hiy0 akat0lewa kizazi ku0nesha hawezi zaa tena milele.

MTOTO tuliyekua nae ni mm0ja WA kipekee malezi tuliy0mpa ni zaidi ya MTOTO kwani tulijua huy0 ndi0 wa kwanza na wa mwish0.

Bahati alikua kama mmea baada ya kufikisha umri wa miezi nane alikua ashakua mkubwa mkubwa hata mimi baba yake nilikua nawezi kumtembeza.

Hela nilikua naz0 lakini sikubahatika kununua gari wala ile nyumba sikuizungushia uzi0. Nikawa na maz0ea kila ninap0t0ka kazini ji0ni namkuta mke na mtoto wangu wak0 nje nami kwa furaha w0te wawili na wabusu nakumchukua mtoto.

Kichek0 kikubwa cha bahati kilikua pale ninap0rudi kazini nakumchukua alich0kua anapenda na pia wat0t0 wengi wanapenda ni kumurusha juu kama tulivy0z0ea wanaume wengi kuwarusha wat0t0 wetu.

Yale maz0ea ya kumrusha yalimea yakazidi mpaka akiwa na umri wa mwaka mm0ja bad0 Tabia ya kut0ka kazini nikiwakuta nje namrusha bahati sikuiacha.

Nakumbuka ilikua ndi0 juzi nikiwa njiani nimet0ka kazini furaha yangu kubwa ilikua ni kufika nyumbani kujumuika na familia yangu.

Nimez0ea kusalimiana na kila mtu hakuna mtua ambaye hanijui pale Kind0ndini jap0 nina uwez0 wa kifedha sikutaka ku0nesha dharau zangu sasa sijui kwanini. wamenifanyia hivi.

Nikiwa nishapita nyumba kadhaa karibu nifike kwangu Mbele yangu nilikutana na mtoto wa makam0 kati ya miaka mitatu na nusu au minne wa kiume kashika Biskuiti mk0n0ni.

Kalinisalinia tukap0sh0na lakini kabla sijapiga hatua kadhaa nilisikia kananiita

“Baba! Baba!” nilip0geuka alini0neshea ule mk0n0 ali0beba biskuti.

“Na0mba nifungulie hii ch0kleti yangu” Nilitabasamu kid0g0 ku0na mtoto md0g0 kama yule ana0mba msaada MTU asiyemjua lakini wanasema mtoto ni malaika.

Nilirudi nikamfungulia ile biskuti aina ya ch0c0late nikataka kumkabidhia lakini alikataa kwa kichwa

“Mama alinifundisha kama mtu akinisaidia kufungua bithikuti nimpe m0ja kama shukrani yangu, Kwa hiy0 na wewe chukua m0ja” Kiukweli hakuna siku niliy0cheka kwa kumu0na mtoto mchangamfu na manen0 ya kuk0nga ny0y0 kama yule MToTo.

Sikutaka kubishana nae nikachukua ch0c0late m0ja nikamrudishia pakti lake.

Nataka ni0nd0ke tena alinishika mk0n0.

“Kula hapa hapa niku0ne” hakika alifundishwa na mama yake tabia nzuri. Ujanja ulinishinda jap0 sikuz0ea kula biskuti ya ch0kleti lakini siku hiy0 ilibidi niile mbele yake ndip0 akakubali ni0nd0kea bila kujua ile ch0kleti ndani yake ina nini.

Niliendelea na safari ya kwenda kwangu dalili y0y0te ya tuki0 baya haikuwep0.

Kama kawaida niliwakuta mke na mtoto wangu kibarazani. Nikafanya kama nilivy0z0ea kuwabusu w0te wawili nikamchukua Bahati mtoto wangu nikana kumrusha juu juu.

Nilimrusha Mara ya kwanza, ya pili huku namchekesha mama yake akifurahia kitend0 kile. Mara ya tatu na ndi0 mara ya mwish0 kumshika mwanangu Wapekee.

nilip0mrusha Mara ya Nne juu Ghafla kwa juu nilp0mrushia nika0na giza na kizunguzungu cha ghafla. Ata kabla mtoto sijamdaka nilijikuta naenda chini fahamu zikanip0tea.

Le0 hii nilip0letwa hapa H0sptali ndi0 nimepata nafuu ya kuamka, asubuhi ndugu walikuja kunitembelea. Wakaniambia habari ambaz0 zilinifanya niwe nalia t0ka mda ule mpaka sasa.

Kumbe siku ile wakati nilip0teza fahamu sikuwa ninemdaka mtoto. Kwa bahati mbaya Bahati MTOTO wangu wa kike wakipekee kwa kuk0sa mtu wakumdaka. Alid0nd0ka kwa kichwa mpaka kwenye sakafu nakupasuka kichwa.

Hapa ninvy0kwambia manen0 haya wanafanya mpang0 wa mazishi. Ndi0 maana nimeku0mba mniruhusu ni0nd0ke nyumbani hata nikaangalia mwili wa mtoto wangu kwa mara ya mwish0.

Inasemakana mwilini kwangu nikikula sumu. Sasa sumu gani ya aina ile nimekuja kukumbuka huwenda ni ile Ch0c0late ya yule MTOTO katumwa kunifanyia vile. Bila yeye au mimi kujua na huy0 mtu ina0nesha anajua fika kuhusu ninavy0rudigi na kumbeba.

Tatiz0 ni kuwa nina kumbukumbu za tuki0 lile lakini sura ya yule mtoto siikumbuki kabisa mpaka sasa.

Kinach0ni0ngezea Mimi machungu mke wangu atakua kwenye hali gani kwa sababu kizazi kashat0lewa Tutapata wapi mtoto mwingine sisi.

Alimaliza hiy0 st0ry akiwa anapiga kwikwi za kili0. Nilishangaa k0ti langu la udaktari linad0nd0kewa na maji kuja kujishika us0ni hata Mimi nilikua nalia.

Binadamu wa aina gani mwenye kumfanyia mwenzake ubaya kama hu0 tena kwa kumtuma MTOTO.?

***USIMUAMINI MWANADAMU Y0Y0TE***

MWISHO

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Unazani ni Kwanini Matatizo yanatupata Sisi Binadamu na Tena Wanaosababisha Hayo Matatizo ni binadamu Wenzetu. Kama kwenye Simulizi Hii ya  Nimempoteza Mwanangu wapekee.

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

IZABELAH Simulizi ya Kusisimua

ISABELAH: SIMULIZI YA KUSISIMUA NA KUFUNDISHA

MKEWANGU MSHAMBA LAKINI ANATHAMANI

MKE WANGU MSHAMBA LAKINI ANATHAMANI: Simulizi za Kusisimua