in

PENZI LA BINTI NGUVA: SUMULIZI ZA KALE NZURI

Penzi la Binti Nguva: Simulizi Nzuri ya Kale, Inayomuelezea Binti Nguva na Mikasa Aliyo pitia Katika Maisha Yake. Soma Mpaka Mwisho Utafahamu yaliy Jiri. Mtunzi: @aishamapepe

PENZI LA BINTI NGUVA SIMULIZI

SUMULIZI ZA KUSISIMUA: PENZI LA BINTI NGUVA.

wakati wana pishana kwa bahati mbaya waka pigana kikumbo cha vibega, na kisu cha fadhira kikadondoka, “samahani sana dada yangu, samahani sijuwi mawazo yangu yalikuwa wapi, yani sikukuona kabisa” alisema yule kijana huku akiinama na kuokota kile kisu mkunjo.

na kumkabidhi fadhira mkononi, wakati anamkabidhi ndipo fadhira aka mwona yule kijana akimtazama usoni, na kumshangaa kwa uzuri wake alionao, ndiyo Fadhira alijijuwa kuwa yeye mzuri, kwa mshangao ule fadhira alitegemea kusikia akitongozwa, lakini kitu cha hajabu, yule kijana aliinuka na kuondoka zake huku Fadhira akisahau kusema asante.

na mala ya pili alipishana nae akiwa na binti mmoja mdogo sana alie fanana na kijana yule aikuwa siri kuwa ni binti yake, fadira aliwaza hayo pasipo kujuwa kuwa anaye muwazia yupo nyuma yake akimfwata, wakati anawaza hayo Fadhira alikuwa amna katiza kwenye sehemu moja ya kuuzia pombe, ambayo vijana kwa wazee utumia kwa kunywa pombe,

mahali hapo uwa anapitaga kwa masimango sana,

asa muda kama huu wajioni, ambapo walevi wanakuwa wamejaa maali pale ndo maana uwa hapendi kuchelewaga kupita mahali pale, “karibu mrembo” aliongea jamaa moja kibonge cha mtu, ambae alikuwa ame kaa akinywa pombe huku chupa kazaa zikiwa chini yake, Fadhira akampuuza “unajiona mzuri sana we malaya, ebu ipeleke wakaikanyage huko” aliongea yule mlevi baada yakuona hajajibiwa kitu na Fadhira, ambae wao wanamuita dada muuza ndizi,

kauli hiyo ilimchefua sana Fadhira, ambae alitamani amfwate yule jamaa na kumchana chana kwa kisu chake mkunjo, “huna lolote, kwanza demu mwenyewe mchafutu” yani nikama yule jamaa alikuwa ame mpania Fadhira aliendelea kushusha matusi kwenda kwa binti Nguva, nakumjaza hasira, asa kutokana na walevi wengine kucheka kwa dhaarau,

lakini binti huyu alijizibiti hasira zake, nakuendelea kutembea kwa mwendo wake hule hule, ujuwe sifa ni kitu kibaya sana, kuona yule binti yupo kimya hapo yule kijana anae julikana kwa jina la kizito, aliinuka na kumfwata Fadhira ambae alisikia vishindo nya kufuatwa na yule jamaa, akakiandaa kisu chake tayari kumwaga damu ya mtu, ok! mdau unazani nini kitamtokea mlevi huyu bwana kizito?

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

African Culture

AFRICAN CULTURE: Tribes and Traditions Found in Africa

BIBI MBUYA NA WAJUKUU ZAKE

BIBI MBUYA NA WAJUKUU ZAKE: SIMULIZI NZURI SANA