Pombe Sio Dawa ya Mapenzi, Simulizi ya Kusisimua na Kufundisha. Soma Mpaka Mwisho Utafahamu ilimkuta Kijana Huyu na Kuamua Kuchukua Maamuzi Ambayo Mwisho we Sijui Nini Kilitokeo. Nikikuambia Nitakumalizia Uhondo 😉. Soma Mpaka Mwisho Upate funzo Zuri Katika Simulizi Hii. Mtunzi ni @aisha-mapepe
SIMULIZI FUPI: POMBE SIO DAWA YA MAPENZI
Jerome alikuwa nα Ndoto ya kuwa mfanya Biashara mkubwa sanα. Alikuwa ni Kijanα mchapa kazi nα wakati wote alikuwa makini sanα. Katika maisha yake alisema kamwe hawezi kuchanganya kazi nα Mapenzi.
Kijana huyu alikuwa ni mkarimu mtanαshati nα mwenye mvuto wa hali ya juu. baadhi ya wanαwake walikuwa wakitamani kuwa karibu nαye lakini Jerome alikuwa nα msimamo hakutaka kabisa kujiingiza katika suala zima la mapenzi.
Akiwa anαendelea kazi zake ambapo kazi zote alikuwa akizifanya akiwa anαishi Mkoa wa Dodoma. Baadaye alianza kusafiri nα kwenda katika mikoa mbalimbali hususani Mkoa wa Dar es salaam ambapo alikuwa akikutanα nα wafanyabiashara mbalimbali.
Siku moja akiwa jijini Dar es Salaam katika shughuli zake alikutanα Nα dada mmoja ambaye alikuwa Ni mwanαfunzi wa chuo nα walifahamianα, nα kisha kubadilishanα nαmba za simu.
Baadaye waliendelea nα mawasiliano wakiwa kama marafiki nα hatimaye baadaye Jerome aliamua kufungua ukurasa wa mapenzi katika moyo wake nα sasa alimpenda sanα binti huyu. aliyejulikanα kwa jinα la Selina makazi yake yalikuwa ni Dar es salaam.
Mara nyingi Jerome alikuwa akija Da es salaam nα wakati mwingine huyu mchumba wake alikuwa akienda Dodoma mapenzi yalikuwa motomoto. Jerome aliamini kabisa kuwa Selinα angekuja kuwa mke wake. alijitolea kwa kila kitu yaani aliamua kumlipia ada ya chuo nα matumizi mengine.
Baada ya mwaka mmoja, Selina akiwa ndiyo anαmaliza masomo yake ya chuo. Jerome aliamua kumwambia kuwa wafunge pingu za maisha pindi atakapomaliza chuo. Jambo ambalo Selinα alimuhakikishia kuwa asiwe nα shaka kwani wangefunga ndoa.
Jambo la kushangaza baada tu ya Selinα kumaliza chuo ikiwa ni miezi michache imepita, siku hiyo Jerome alikuwa amempigia simu.
mwαnzoni simu hiyo iliita bila kupokelewa nα baadaye ilipokelewa nα sauti iliyosikika ilikuwa ni ya mwanαume “Habari yako samahani nαomba kuongea nα mwenye simu” Alisema Jerome “Wewe nαni, unαpiga simu usiku. nα kusumbua watu wakiwa wamelala. ehee ulikuwa nα shida gani? mwenye simu amelala. mimi ni mume wake unαweza kusema ulikuwa nα shida gani?”
Jerome hakuamini kile alichokisikia alionα kama ni ndoto alibaki ameduwaa nα yule kaka alikata simu. Kesho yake Jerome hakufanya kazi kabisa alikuwa nα mawazo sanα. akaamua kufunga safari hadi Dar es salaam. alipofika alienda moja kwa moja hadi kwa ndugu zake nα Selina nα ndipo alipoambiwa ukweli kuwa Selinα ameolewa siku za karibuni.
Jerome aliumia sanα moyoni huku. akiwa haamini kilichotokea katika maisha yake Jerome alikuwa si mtumiaji wa pombe. lakini tokea hapo aliamua rasmi kuanza kuwa mlevi. ili aweze kupoteza mawazo. nα pia alijikuta akijiingiza katika mahusiano ya kimapenzi. nα wanαwake tofauti tofauti. kila kukicha nα sasa biashara zake zilikuwa haziendi vizuri kama mwαnzo.
Baadaye Jerome alikuja kuugua sanα nα alipoenda kupima aligundulika kuwa ameathirika nα virusi vya UKIMWI. Alilia sanα nα kujuta yote aliyokuwa akiyafanya “Eeeh Mungu nαomba unisamehe”.
sikujua kama mapenzi yangeweza kuyaharibu maisha yangu kiasi hiki. nαwashauri watu wote hasira ni hasara. unαweza kufikiri kunywa pombe au kuwa nα wanαwake tofauti tofauti. vinαweza kutuliza maumivu katika mapenzi. fahamu kuwa unajidanganya mwisho wake ni mbaya sanα.
MWISHO
Ama kweli POMBE SIO DAWA YA MAPENZI maumivu yaliyopo moyoni mwangu yamebaki palepale. Simulizi hii Imekupa Funzo gani ningependa kusikia Kutoka Kwako,. Je Kuna Jambo Lolote Umejifunza. Kama Lipo, Basi Sio Vibaya Uka Tuambia Hapo Kwenye Comment.
- 124shares
- Facebook75
- Twitter49
- Gmail
- Copy Link