Tazama Matokeo Hapa
Download Mitihani
Hizi ndizo Sheria za Mpira Utotoni. Enzi hizo wahenga wenzangu tulikua Bado wadogo. Tena Wengi wetu tulikuwa watoto wa Uswazi, yani Mpira tunaupiga Pale Uwanja kivumbii Mpaka ufumuke 😂. Watoto wa kishua hawawezi kuelewa haya Mambo.
SHERIA ZA MPIRA UTOTONI.
- Mwenye mpira Lazima apate namba, hata kama hajui kucheza mpira.
- Dogo mnene Lazima awe golikipa.
- Mwenye mpira ataamua nani acheze na nani asicheze.
- Kama haujashiriki kufuma mpira unaweza usipate namba kabisa.
- Inaruhusiwa kujificha kama akitokea mzazi wako, tena kama hukuaga nyumbani. Akiondoka unarudi uwanjani.
- Mwenye mpira akikasirika mpira ndo umeisha, Kwahiyo kila wakati ni kumpamba kama Bibi Arusi.
- Inaruhusiwa kubadili golikipa kamaikitokea penati, na baada ya hapo ataendelea kudaka kama Kawa.
- Mechi itaisha pale giza linapoingia, Haijalishi mmeanza Saangapi.
- Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka Nje.
- Yule mtaalam wa soka huwa hakosi namba, hata siku moja.
- Akipita mtu mzima uwanjani, Mpira unasimama kwa muda mpaka afike mbali kidogo ndo ball liendelee.
Je, unakumbuka Sheria gani nyingine..? Nijulishe Hapo chini kwenye Comment Sheria za Mpira utotoni unazozikumbuka. itakuwa Poa Sana. Mimi pia na kumbuka kulikuwa Hakuna refa yaani kila mchezaji ndio refa au wale mashabiki ambao ni wachezaji walio kosa namba ndo wanatoa maamuzi.
Pia Usisahau ku share kwa Marafiki zako nao Wapate ku cheka.
- 250shares
- Facebook178
- Twitter72
- Gmail
- Copy Link