Simulizi Mpya Mwezi Huu September: “Watoto 100”. Huu ni Mkasa Ambao Nimesimuliwa Na Mzee Mmoja Utamfahamu Mbele kadri Simulizi Inavyo Kwenda. Mwandishi wa Simulizi ni Jerald Maswa. Leo Aisha Mapepe nimetumika Kama Daraja tu Hapa Kuwa Fikishia Hii Story.
“We mzee unatania!” Yαlikuwa ni maneno yαngu yα kwanza baada yα kumsikiliza mzee Izadin.
“Mimi nilipokuwa kijana niliwahi kumuomba Mungu kuwa nitakapokuja kuoa basi anijaalie watoto 100.” Ndiyo sentensi aliyokuwa ameitamka mwanzoni kwenye maongezi yεtu.
“Utawaleaje?” nilijikuta nikimuuliza.
Mzee Izadin, dereva wa bosi wetu hapa kazini, alinijibu, “Kwani mimi ndo nawalisha mdogo wangu Mentor? Mimi ni njia tu yα kupitishia riziki yαo, ila mtoa riziki ni Mungu pekee”
2007, Desemba 22 Jumamosi
Victor, akiwa na miaka 36, alikuwa akifunga ndoa. Ilikuwa ni siku yα sherehe hoi hoi nderemo na vifijo kwani Wεngi wetu tulikuwa tumeshahisi kuwa kaka Victor hatooa Tεna. Kila siku alikuwa akituambia kuwa anajipanga na maisha,
anawaandalia watoto wake maisha mazuri. Tulibaki tukijiuliza hao watoto wako wapi maana hatuoni hata dalili za yeye kuwa na ukaribu na mabinti hata wa jirani.
Kaka Victor – kwa jina lingine Mchungaji – ni katika wale wakaka ambao wakati tunakua walikuwa ndio wakaka wa kutolewa mifano majumbani mwenu (role models). Yαani ukifanyα jambo bayα/kosa unaambiwa, “Muangalieni kaka yenu, kwa nini msimuige hata robo tu yα tabia zake?”
Kuna kipindi rafiki yαke aliwahi kuniambia, “Yαni siku nikimkuta mchungaji na mwanamke chumbani na wote wako uchi na mchungaji akaniambia, ‘sijamfanyα chochote’, nitamuamini.” Hivyo ndivyo jinsi kaka Victor alikuwa amejijengea sifa katika jamii.
Zaidi yα yote, kaka Victor alikuwa mfano wa kuigwa hata kimasomo kwani baada yα kumaliza shahada yαke yα kwanza katika masomo yα uchumi na kufaulu vyema, alibahatika kupata ufadhili wa kwenda kusoma masomo yα shahada yα uzamili katika chuo kikuu cha Havard huko Massachussets, nchini Marekani.
Alikuwa na akili yα peke yαke na mtu wa kujituma. Kwani alipomaliza chuo yeye kabla hata chuo kikuu cha Dar es salaam hawajamuita kuwa mkufunzi msaidizi alikuwa ameshajiajiri kwenye kampuni yαke ndogo yα BIMA.
Ngoja nikurudishe nyuma kidogo; wakati yuko mwaka wa pili chuoni yeye pamoja na mwenzake waliandika proposal ambayo ilishinda na walipewa kila mtu fedha taslimu shilingi milioni tano.
Katika vitu alivyovifanyα ilikuwa kununua kiwanja huko Kigamboni jijini Dar es salaam, eneo kubwa huko ambako kwa sasa kuna kijiji kiitwacho Avic town. Fedha nyingine alianzisha ‘agency’ yαke yα mambo yα BIMA. Ni wakati anajiandaa kwenda kusoma nje alipofuatwa na wawekezaji waliojenga hiyo Avic town ili wanunue eneo lake kwani lilikuwa limepakana sana na eneo lao.
Kwa fedha zile aliwekeza zaidi kwenye ‘agency’ yαke na kuongeza mtaji hadi kufanikiwa kuwa ‘brokerage’.
Pamoja na yote hayo alikuwa na vibiashara vyα hapa na pale ambavyo vilifanyα maisha yαke mjini hapa kuwa mazuri na alizidi kutufanyα wadogo zake sisi tuonekane bado sana.
Kaka Victor alikuwa mcheshi na mchangamfu na kama kawaida wadada Wεngi walijisogeza kwake lakini nahisi katika mambo yαliyokuwa mwishoni mwa mawazo yαke ni hilo la wanawake.
Kila alipokuwa akiulizwa suala la mahusiano alijibu, Tεna kwa kizungu, “I worry about things that I have to struggle for, not those that are provided by nature” akimaanisha yeye anahofia juu yα mambo ambayo inabidi kuyαpigania kuyαpata na sio yαle ambayo yαpo tu. Kwamba siku mtu akitaka kuoa ataoa tu lakini huwezi kutaka kuwa na mali na ukawa nazo, lazima uweke bidii kuzipata.
Akiulizwa na watu wazima zaidi kuhusu ndoa alikuwa akijibu, “najipanga na kuwaandalia maisha wanangu” Siku zote hakukosa jibu la kwa nini hakutaka kuoa na kwa hilo alifanikiwa kwani alifanikiwa kuwa na biashara ambazo zilikuwa zinaenda vizuri, nyumba yα kuishi na nyingine za kupangisha Tεna si kwa hela zetu za madafu, uwezo wa kubadili magari japo si kwa kila siku n.k.
Siku kaka Victor anatuambia anataka kuoa hakuna aliyeamini, hata alipomleta binti ambaye kwa hali yα kawaida Wεngi tungemkataa basi ilibidi tutafute justifications (vihalalishi) za kuonesha kuwa anaweza kuwa wa tofauti.
Na siku hii yα Jumamosi, Desemba 22, 2007 kaka Victor alifunga pingu za maisha huku akiwa kwa hakika amejiandaa na kujipanga vyema kwa ajili yα wanae ambao sasa tuliona wanaweza kupatikana.
Kuanzia Januari 2009
Mafanikio yαlizidi kumiminika kwa kaka Victor ambapo wakati huu Mungu alikuwa amewabariki na mtoto mmoja, James. Ni wakati huu pia alipopata ufadhili kwenda nchini Ufaransa kwa ajili yα shahada yαke yα uzamivu. Aliondoka akiwa na amani kabisa akijua kuwa kila kitu amekiacha kikiwa katika mikono salama.
Hadi wakati kaka anasafiri hatukuwa na ukaribu sana na shemeji yεtu – mke wake – kwani hakupenda sana kututembelea na wala hakuwa akipenda tukienda kwake. Hata hivyo tulimheshimu kwani kaka alikuwa akimpenda sana na kumuamini.
Mwεzi wa tano kaka alinipigia simu kuwa amepata safari kwenda jijini Rio de Janeiro kwa ajili yα mkutano. Nilimtakia kila la kheri na hata alipofika alinieleza jiji hilo lilivyo zuri na kunitumia baadhi yα picha kupitia barua pepe.
1 Juni, 2009
Nilipata habari kuwa ndege yα Air France iliyokuwa ikitokea Rio de Janeiro kuelekea jijini Paris imepata ajali na abiria wote 216 waliokuwamo wamefariki. Kwanza haikuniingia akilini hadi nilipokumbuka kuwa hiyo ndiyo siku ambayo kaka alikuwa asafiri kurudi chuoni kwake huko Ufaransa. Nilijikuta nikisali kumuomba Mungu kaka asiwepo kwenye ndege hiyo. Nilijaribu kutumia njia mbalimbali kuhakiki kama alikuwepo bila mafanikio yoyote. Ni hadi walipotangaza orodha yα abiria waliokuwa wamepanda ndege ile ndipo tulipofahamu kuwa kaka Victor hatunaye Tεna duniani.
Mipango yα mazishi ilifanyika na kwa kuwa miili yαo haikupatikana – kwani ndege iliangukia baharini – tulifanyα tu ibada na kila mtu kutawanyika. Tulimuuliza shemeji kama aliacha wosia wowote na kama ilivyo ada hakuwa ameandika chochote isipokuwa tu kwa kutumia fomu alizokuwa akijaza kazini na kwingineko alikuwa akimuandika mkewe kama mrithi pekee wa mali zake endapo kifo kitamkuta.
Hivyo sisi kwa kuamini walikuwa wanapendana hatukuona shida na tulimsaidia kupata vibali vyote vyα kuhakikisha mirathi na stahiki zote za mumewe anazipata yeye. Tulimuonea sana huruma shemeji yεtu kwani bado alikuwa binti mdogo.
Januari 6, 2016
Mpαka naandika hapa, shemeji yεtu, aliyekuwa mke wa kaka yαngu Victor, amehamia nchini Uganda ambako ameolewa na mwanaume aliyekuwa akifanyα kazi ubalozi wa Tanzania nchini Uganda. Miezi michache tu baada yα kaka kufariki, shemeji alitokomea kusikojulikana na kumuacha James mwanaye kwa mama yεtu. Tulipojaribu kufuatilia mali za mumewe alizoziacha tulikuta zote zimeshabadilishwa umiliki na hata kampuni ndogo ile yα BIMA aliiuza kwa mchaga mmoja bila taarifa kwetu.
Hakurudi kumuangalia mtoto na hata alipokutana na ndugu yεtu mwingine alisema yeye ni mdogo mno kukaa peke yαke na huyo mtoto anamnyima fursa hivyo hatomrudia.
Ni jana tu ndiyo nilitoka kumlipia ada James ili aweze kuanza darasa la kwanza mwaka huu.
Hua najiuliza ni aina gani yα Mke kaka Victor alipata, yote aliyokuwa akituambia kuwa anatafuta pesa kwa ajili yα mwanae ndio yαmeishia hivi kwa sisi kumtunzia Mwanae. Juhudi na maarifa yαke yote imekuwa bure kabisa. Mwanae hatafaidi jasho lake hata kidogo.
2016, Januari 5 Jumatano
“Tεna mdogo wangu asikudanganye mtu, wewe kula yαko yα kesho huijui, ni riziki yα Mwenyezi Mungu. Akiamua ule utakula, akiamua ukose, utakosa tu!”
Alinishitua kutoka katika lindi la mawazo na kujikuta naendelea kumsikiliza.
“Sasa hivi nina watoto 12 na watoto wa ndugu zangu 6 hivyo jumla 18, lakini kwa mshahara wangu huu huu wote wamesoma na wameishi kwangu, wamekula na kulala.”
Nilimtania kama bado ana ndoto hiyo yα Watoto 100 akanijibu, “unadhani! mke wangu hapa analea mtoto ana miezi nane. Hivyo bado ninaendelea mdogo wangu. Na hapa nina miaka karibia 50 ila ninapiga shughuli kushinda nyie vijana…”
Nilimuacha mzee Izadin akiendelea kujisifu huku nikitafakari…sijui na mimi niombe watoto 100 ?!.
MWISHO
Simulizi Mpya Mwezi Huu September: “Watoto 100”. Kwa Simulizi Nyingine Kama Hizi Bonyeza Hapo Chini.
- 107shares
- Facebook42
- Twitter65
- Gmail
- Copy Link