in

ASHURA SIMULIZI: Kweli Ashula Sio Mtu Mzuri

Simulizi ya Ashura, Huyu ni Dada Ambaye Amefanya Tukio la Namna yake kwa Jamaa Mmoja. Soma Mpaka Mwisho Mkasa Huu Kujua Yaliyo Jiri. Mtunzi wako ni Mimi @aisha-mapepe

Ashura Sio Mtu Mzuri

SIMULIZI YA ASHURA: ASHULA SIO MTU MZURI

Kijana mmoja alitokea kumpenda sana dada mmoja Aitwaye Ashura. ijapokuwa dada huyo alikuwa akimtolea nje mara kwa mara lakini kijana hakukata tamaa. akiendelea kurusha ndoano huku akiamini siku moja atafanikiwa. Siku moja dada huyo akiwa yupo nyumbani aliamua kumpigia simu huyu kaka na kumtaka aje nyumbani kwake. yule kijana alifurahi na kuhisi sasa ombi lake limekubaliwa.

Akiwa nyumbani kwake dada huyo (Ashura), alikuwa amevalia kanga moja laini. kutokana na hali ya hewa ya jiji la Dar es salaam. Kwa upande wa yule kijana alikuwa amefurahi sana na haraka alijiandaa na kuanza safari kuelekea kwa huyu dada.

Njia ni kaka huyu alikuwa akijiuliza maswali mengi. huku akiwa haamini kama yule dada amemuita nyumbani kwake. Alipofika, alibisha hodi na yuel dada akafungua mlango huku akionyesha tabasamu pana katika paji la uso wake.

Kaka huyu aliingia ndani huku kijasho kikimteremka mithili ya mtu aliyekuwa anakimbia. Dada huyu alimkaribisha vizuri. yule kaka aliomba maji ya kunywa huku muda wote akimtizama kwa umakini dada huyu mrembo. Aliyeumbika kila idara na ile kanga nyepesi aliyovaa ilikuwa ikionyesha umbo zuri la Ashura ambaye waswahili huwa wanasema. mtoto kajaaliwa (mashalaah).

*********

Kaka alikuwa akivuta pumzi kwa haraka haraka, na kusema. “Nimefurahi sana, umenikaribisha nyumbani kwako ni pazuri sana”. Ashura alitabasamu na kusema “Asante sana, nimefurahi pia umeitikia wito wangu, samahani kwa usumbufu wangu”.

Yule kaka alitabasamu huku akijisogeza sogeza “Hakuna tatizo, usijali kabisa, mimi nipo kwa ajili yako, naimani sasa nina….” Kabla hajamilizia kuongea Ashura alimshika mikono yake miwili huku akimtizama machoni, kwa macho yake malegevu, mithili ya mtu aliyekula kungu

“Samahani kaka. mimi nimekuita hapa kuna jambo nataka unishauri, nataka kujua ni zawadi gani nzuri unaweza kumpatia mwanaume unayempenda”. Kaka yule alikuwa akitetemeka na kusema “Chochote tu, zawadi ni zawadi. alimradi kuwe na Mapenzi ya Kweli

Ashura alitabasamu na kusema “Ni kweli, mapenzi ya kweli ndiyo jambo la msingi. nitampenda maisha yangu yote”. Kaka yule akauliza “Utampenda? Nani huyo”

Yule dada alitabasamu tena na kusema “Samahani, rafiki nilikuwa sijakuambia. wiki ijayo nafunga ndoa na mpenzi wangu wa muda mrefu ambaye nampenda sana, na pia nilikuita ili nikupe kadi ya harusi, nitafurahi kukuona, kwani wewe ni rafiki yangu pia”

Yule kaka alibaki amepigwa na butwaa. “Ati, nini unaolewa, daaah, jamani, kwahiyo.” Alinyanyuka na kuondoka bila ya kuaga. huku akimuacha yule dada anamuita ili ampatie kadi bila ya mafanikio

MWISHO

Kumbuka Sio Kila Unalo liwaza litatokea Hivyo Hivyo. Haya Maisha Kunawatu Tofauti Tofauti, Wengine Kama Ashura. Hivyo Kaa Kijanja 😉.

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sarafina Simulizi

SARAFINA: MOJA KATI YA SIMULUIZI PENDWA MNO

Asiyesikia la Wakuu Huvunjika Miguu

ASIYE SIKIA LA WAKUU: HUVUNJIKA MIGUU 😎