in

Simulizi za Kiswahili Mpya: “Usilolijua ni Usiku wa Giza”

Simulizi za Kiswahili Mpya: “Usilolijua ni Usiku wa Giza”. Katika kijiji cha Mtakuja kulikuwapo na wasichana watatu na wote walikuwa ni warembo kwani kwa uzuri waliokuwa nao ulitosha kabisa kuwatetemesha na kuwatoa udenda wakware wote watakao waona hao warembo wamepita mbele yao .

Simulizi za Kiswahili - Usilolijua ni Usiku wa Giza

USILOLIJUA NI USIKU WA GIZA: SIMULIZI ZA KISWAHILI MPYA

Uzuri hao mabinti walikuwa marafiki wa chanda na Pete kwani walipendana kuliko kawaida mpaka wakawashangaza watu katika kijiji hicho,kwa majina yao binti wa kwanza aliitwa Aisha ,wa pili aliitwa Manka na wa tatu aliitwa Jasmini.

Sasa katika tembea tembea zao hapo mtaani siku moja,walikutana na kijana mmoja mtanashati na mpole akiwa anapishana nao njiani, mmmmh usema ukweli yule kijana aliwapasua moyo hao mabinti kwani wote walimwangalia mno kwa hisia nzito ,waliendelea kumtazama yule kijana mpaka alipotoweka kwenye mboni za macho yao.

Yule kijana pasipo kujua kwamba anatazamwa kwa hisia nzito aliendelea na safari yake kama kawaida, Binti mmoja aliyeonekana kuwa mrembo kuliko wote ,Jasmini, ndiye aliyeonekana kutekwa zaidi na hisia za mapenzi kwa huyo kijana pasipo kujua hisia za wenzake zipoje Kuhusu huyo kijana handsome,

Jasmini alilemewa na hisia nzito sana akiwa amekaa ,amelala au anakula,alimfikiria sana huyo kijana ikafikia kipindi akaonekana kana kwamba alikuwa akiumwa,alinyong’onyea sana akatamani angarau siku moja aone hata picha ya huyo kijana moyo wake ufarijike.

*****

Siku moja hisia zilimlemea akaamua kuwatoroka wenzake bila hata kuwaaga na kwenda kumsaka yule kijana popote pale alipo,alizunguka kila sehemu pale mtaani kama chizi huku njemba zingine zikiendelea kumwangalia huku zikimmezea mate, watu wengine walianza kujiuliza,huyu siye Jasmini shogae na akina Aisha na Manka?

Mbona yuko peke yake wakati Mara nyingi tumezoea kumwona akiwa na wenzake, kipi kimemsibu huyu binti? Mbona anaonekana kama amechanganyikiwa vile mmh!! Makubwa!!. Jasmini aliwasikia yote waliyokuwa wakiyaongea lakini hakuwajali,duuh! Mapenzi bwana daah! Noma sana ,watu wanasema mwanamke akipenda amependa kweli sasa nimeelewa kupitia kwa Jasmini.

Akiwa anatembea huku akiwa amekalibia uwanja wa mpira wa miguu lahaura Jasmini akamwona yule kijana akiwa amekaa peke yake akiangalia mpira huku akiwa hajui hili wala lile,Jasmini alipomuona akaachia tabasamu la furaha la chini chini akajipiga konde na kuamua kusogea hadi sehemu aliyokuwa amekaa huyo kijana, akajisogeza na kuketi karibu nae,kijana akiwa anaangalia mpira,

Ghafla aliamua kuangalia pembeni yake mh! Hakuamini macho yake kama amekaa na binti mrembo kiasi hicho,Alijikaza kimya kimya na kujifanya na yeye kama anaangalia mpira huku akiibia ibia kumwangalia Jasmini, mood ya huyo kijana kuendelea kuangalia mpira iliyeyuka mara moja kutokana na uwepo wa Jasmini pembeni yake, Simulizi za Kiswahili

*****

Jasmini na yeye kimya kimya aliendelea kumwangalia huyo kijana kwa kuibia.Wakiwa wanaendelea kutizamana kwa kuibiana mmh! si ghafla wakakutanisha macho yao, Jasmini akawa wa kwanza kuyakwepesha macho yake kwa aibu.

Kijana akaamua kutumia uanaume wake kuvunja ukimya akaanza kama hivi; samahani Dada ninaweza kukufahamu? Jasmini akaitikia bila samahani ,kwa jina Mimi naitwa Jasmini nakaa mtaa wa pili kutoka hapa,alijibu huku akiachia tabasamu nono lililozidi kumchanganya huyo kijana, kijana nae akaamua kujitambulisha,

Mimi naitwa Kelvin au kwa kifupi unaweza niita Kelv,nakaa mtaa wa kwanza kutoka hapa,Jasmini akamjibu unajina zurii nimelipenda sana sana,akaendelea; kama hutojali Kelv ningependa tupeane mawasiliano hehehee!! Alijichekesha huku akijaribu kujiinamisha kwa Kelvin, haina shida Jasmini, baada ya hapo wakapeana mawasiliano na kuagana kila mmoja baada ya kumaliza kuangalia mpira.

*****

Jasmini alirudi nyumbani kwao huku akiwa na furaha ya ushindi katika jambo lililokuwa likimnyima usingizi siku baada ya siku.Usiku wa siku hiyo Jasmini hakuweza kupata usingizi kabisa, hivyo akaamua kuchukua simu yake na kumpigia Kelvin usiku huo huo na mazungumzo yakawa hivi;

Jasmini: Haloo! Darling? Uko poa!

Kelvin: Niko fresh kabisa Jasmini!, nambie.

Jasmini: Nimekumis!! Sana Kelvin ama hakika wewe ni mwanaume pekee niliyetokea kukupenda katika maisha yangu na siwezi kuishi bila wewe Kelvin, wewe ndiye chaguo sahihi la moyo wangu Leo nimeamua kukukabidhi moyo wangu usiniumize mwenzio nitakufa .

Kelvin kusikia hivyo alihisi kama yuko paradiso maana hata ile sauti tu ya Jasmini ilitosha kabisa kumtoa nyoka pangoni,ilikuwa ni sauti nyororo na laini .Kelvin akamjibu Jasmini hata Mimi nakupenda sana Jasmini tokea tuonane kule uwanjani nimetokea kukupenda, Waooo!! Umenifurahisha sana Kelvin wangu nitakupenda daima, ukifa na Mimi nakufa.Waliongea mengi sana mwishowe wakatakiana usiku mwema .

Asubuhi na mapema Jasmini aliamka na kwenda kuwaeleza mashoga zake Kuhusu ujio wa mpenzi wake,nao bila kinyongo wakamkubalia huku wakiwa na hamu kubwa ya kumuona shemela wao mtarajiwa.*Laiti kama angejua kuwa huyo anayemwita mpenzie anawindwa pia na shoga zake hao asingedhubutu hata kuwaambia*. Simulizi za Kiswahili

*****

Baada ya masaa mawili Kelvin alifika hapo nyumbani alipokuwa ameelekezwa na Jasmini na kuwakuta Jasmini pamoja na shoga zake wawili, Waooo!! Baby ,Jasmini alimkimbilia Kelvin na kumkumbatia huku akimmiminia busu za nguvu, mashavuni na mdomoni.

Wakati hayo yakiendelea Aisha na Manka hawakuamini macho yao wakabaki wameshangaa huku wakiwa wamepigwa na butwaa maana walimkumbuka vilivyo huyo kijana handsome. Jasmini pamoja na Kelvin waliendelea kubaki wamekumbatiana wakiwa hawajui hili wala lile.

Mapenzi kati ya Jasmini na Kelvin yaliendelea kuchanua siku hadi siku huku wivu wa mashoga zake Aisha na Manka ukizidi kuongezeka siku baada ya siku .Siku moja Jasmini akiwa kwa Kelvin yaani sehemu walipoamua kuyaanzia maisha yao mara baada ya kuwa pamoja,Aisha na Manka walipanga kitu kibaya cha kumkomesha Jasmini kwa usaliti wake zidi yao.

Siku zikapita Jasmini na Kelvin wakiishi kwa furaha kama mke na mume .Siku moja Aisha pamoja na Manka waliamua kuwatembelea Jasmini pamoja na Kelvin kwa lengo la kuwasalimia.

Walipofika nyumbani kwao bahati mbaya au nzuri walimkuta Kelvin peke yake akiwa amejipumzisha sebuleni huku pembeni yake akiwa ameweka kinywaji chake kwenye bilauri na kinywaji hicho kilikuwa ni maji ,

*****

Wakati huo Jasmini yeye alikuwa ametoka kidogo kwenda kidogo kwenda kufanya mahemezi ya hapa na pale sokoni ,Basi Aisha pamoja na Manka wakafika pale…. Manka akachungulia dirishani akamuona Kelvin amelala peke yake sebuleni huku pembeni yake kukiwa kuwewekwa bilauri ya maji iliyokuwa juu ya meza maana yeye alikuwa amejilaza juu ya sofa .

Manka bila kupoteza muda alinyata mpaka kwenye bilauri hiyo alipoifikia akatoa kijikaratasi kimoja haraka haraka akachukua dawa kutoka kwenye hicho kijimfuko yenye rangi nyeupe mithili ya glucose akaiweka kwenye hayo maji ya Kelvin kisha akatikisa pole pole alipomaliza akaondoka,

Punde si punde Kelvin akashtuka usingizini na kuhisi kama ana kiu,maskini wa Mungu ! Kelvin akachukua bilauri ya maji akaamua kunywa pasipo kujua kama kuna adui aliingia na kuweka sumu kwenye maji hayo ,alipomaliza tu kunywa ghafla akahisi maumivu ya tumbo kama vile kuna kisu tumboni kinakata ,,

*****

Kelvin alianguka chini na kugaa gaa kisha akatulia kimya.Jasmini alirudi akiwa mwenye furaha ya kwenda kumpikia mumewe chakula kile akipendacho ,Mume wangu Leo utakipenda chakula nitakacho kupitia, Jasmini aliongea bila kujua nini kimempata mmewe Ghafla alipoingia sebuleni na kumkuta mpenzi wake amedondoka chini alimkimbilia na kwenda kumwangalia huku akiwa analia,

Mme wangu, Mme wanguuuu!! My husband, amkaa uone nilicho hemea, amkaa! Umekufa Mme wangu, amka babaaaaa!! Usiniache peke yangu amkaaa!! My Darling!!, Jasmini hakuwa na chochote cha kufanya au kusaidia maana Kelvin tayari alikuwa ameaga dunia. Alilia sana mwishowe na yeye akaamua kujiua.

FUNZO:

Usimwamini kila umdhaniye kuwa ni rafiki yako wa dhati maana hujui uadui alio nao moyoni mwake akikuona umefanikiwa.

MWISHO

Kwa Simulizi za Kiswahili Mpya kama Hizi Bonyeza Hapa.Simulizi yetu ya Usilolijua ni usiku wa Giza Haina la Ziada Mpaka Hapa. Kama Unamaoni au Ushauri Tuandikie Hapo chini kwenye Comment

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Mitihani ya Kiswahili Secondary

Kiswahili Past Papers Form Four and Three: Secondary Free (PDF)

Civics Past Papers Secondary

Civics Past Papers Secondary: Form Three and Four (PDF)