in

SIMULIZI ZA MAISHA: Kila Jambo Lina Sababu

Aisha Mapepe is Back Again na Kithungu cha Mchongo, Leo Nimekuja na Simulizi za Maisha nimeenda Likizo Kwenye Simulizi za Mapenzi kidogo. Simulizi Hii inakwenda Kwa Jina la “Kila Jambo lina Sababu”. Kwenye Maisha Kila Jambo Hutokea kwa Sababu Maalum ingawa Mwanzo wakati Jambo Hilo Linatokea Sio Rahisi Kusema Hivi. Okay Ungana Nami Mpaka Mwisho wa Simulizi Hii Kufahamu Yaliyo Jiri.

Simulizi za Maisha - Kila Jambo Lina Sababu

KILA JAMBO LINA SABABU: SIMULIZI ZA MAISHA.

Rubani mmoja wa ndege alipata majanga akiwa angani baada ya ndege yake kuanza kushika moto, yeye pamoja na abiria wake wakawa hawana jinsi zaidi kutumia parachitu ili waweze kujiokoa .
Parachuti ile ilimpeleka rubani yule baharini na baada ya siku nzima ya kuogelea kwa bahati nzuri baharia yule akiwa peke yake alijikuta katika kakisiwa kadogo ambako watu hawaishi huko .

Maajabu ya kisiwa kile kilikuwa na kabonde kadogo alikoweza kupata maji ya baridi (yasiyo na chumvi). Baharia Yule ilimbidi atumie majani ya minazi mitano aliyoikuta pale ili aweze tengeneza sehemu ya kujisitiri usiku pamoja na kuwasha moto (kwa njia ya kupekecha). Atakao utumia kuchomea samaki ili ale pamoja na kujilinda dhidi ya viumbe hatari waishio majini.

Kwa uzoefu wake wa miaka mingi katika masuala ya anga na baharini alijua kuwa eneo. Lile kamwe asingeweza kupata msaada wowote. Kwani hakuna meli wala boti ambayo ingeweza kufika pale na pia kwa kuwa kale kakisiwa kako katikati ya bahari ni dhairi. Eneo lile hakuna meli ambayo ingeweza tia nanga hivyo meli na boti hupita kando ya kisiwa kile tena mabli sana. Simulizi za Maisha

*****

Rubani yule aliishi pale kwa zaidi ya wiki bila ya mafanikio na kuanza kujiona kama mtu aliyetupwa kwenye dunia yake isiyokuwa na msada wa aina yoyote ile. Kazi yake kubwa ilikuwa ni kuvua samaki, na kuja kuwachoma na. Kwa kuwa kuni zilikuwa zaenda kuishia hivyo alijitahidi kuufumbika moto na kuutumia usiku tu.

Siku moja akiwa bondeni anajitafutia samaki na maji ya kunywa ghafla akahisi kama kuna. Harufu ya moshi ikambidi arudi kwenye kiota chake mara moja. Kufika pale akashangaa kuona upepo ulipuliza ulemotona kuunguza kuni zake na. Kibanda chake kwa hiyo hata weza kula wala kuwa na moto tena.

Kwa uchungu mwingi rubani Yule alijitupa chini na kulia huku akiwaza kuwa sasa Maisha yatakuwaje bila ya chakula, moto na hata kula samaki wa kuchoma tena?

Basi Baada ya kuwaza na kulia kwa muda mrefu akapitiwa na usingizi mzito na kulala zaidi ya masaa matano.

Baada ya kuamka akiwa na uchovu na njaa akashangaa kuona kwa mbali kuna meli inakuja. Na baada ya kukaribia ikatia nanga wakashuka watu na na baada ya kuwauliza walijuaje. Kuna mtu pale jamaa wakasema tukiwa kwa mbali tuliona kuna moshi. Unafuka hapa tukajua kuwa kuna watu wanaishi hapa hivyo tukaamua tuje tutafute maji ya kunywa kwani tuliishiwa kwenye meli yetu.
Baada ya hapo jamaa akapata lifti na kurudi kwao

MWISHO

Funzo

  • Kila jambo katika maisha yetu hutokea kwa sababu maalumu na mwisho wa siku lazima jibu litokee.
  • Mungu wetu ni mwema na hujibu maombi kwa muda muafaka na wala hachelewi

Kwa Simulizi za Maisha Kama Hizi Endelea Kutembelea Website Hii ya Africona. Na Mtunzi wako ni mimi Aisha Mapepe. Peace…

Written by Aisha Mapepe

Aisha Mapepe ni Mwandishi wa Simulizi Mbalimbali za Mapenzi, Maisha na za Kuelimisha. Lengo ni Kuburudisha Jamii na Kuondoa Stress za Maisha zinazo tukabili Baadhi Yetu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Story za Maisha - Wifi Nimekuchoka Kwa kweli

Story za Maisha: Wifi Nimekuchoka Kwa kweli

Hadithi za Maisha - Sijapoteza Furaha Yangu

HADITHI ZA MAISHA: Sijapoteza Furaha Yangu, Kikulacho ?