in

SIMULIZI ZA VICHEKESHO: Ungekuwa Huyu Padri Ingekuwaje?

Tazama Matokeo Hapa

Download Mitihani

Nauliza tu Wajumbe, je ungekuwa Huyu Padri Ungefanyaje. Soma Simulizi za vichekesho na Simulizi Nyingine nyingi ikiwemoza Mapenzi, Mikasa ya Maisha pamoja na Hadithi za Kale Hapahapa Africona.

Kwanza tujue Padri Mwenyewe anasema…

Usisahau kuni Follow @japhary kwa Vichekesho na Mada Mbalimbali za Kuvutia. 😊

UNGEKUWA PADRI UNGEFANYAJE - CHEKA TU

SIMULIZI ZA VICHEKESHO: UNGEKUWA HUYU PADRI UNGEFANYAJE..?

Siku Moja Padri alikuwa amekaa katika Chumba cha Kuungama Dhambi, Kidhungu wanakiita (Comfession Booth). Mara kukaingia jamaa mmoja aliyekuwa anawasiwasi sana.

Baada ya kuingia hapo, akapiga magoti upande wa pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuongea na Padri. ili apate Kumuungamanisha apate kusamehewa maovu yake.

JAMAA: “Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana.”

PADRI: “Endelea…”

JAMAA: “Mapema Leo, Bosi wangu aliniita nyumbani kwake. akaniambia amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema Nisipo Zirudisha atanipeleka polisi. sasa kiukweli mm naogopa kufungwa Sana. Nilicho amua Kufanya ni Kutazama huku na huku, nikagundua tuko wawili peke yetu, nikatoa Bastola nikamuua. Yesu atanisamehe..?

PADRI: “Utasamehewa.”

JAMAA: “Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa kutazama, Loh..! Mke wa bosi, alipoona kilichotokea akasema anapiga polisi simu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu. nikamuua na yeye pia… Yesu atanisamehe hilo..?”

PADRI: “Utasamehewa, Yesu alikuja Kwaajili ya watu kama nyie.”

JAMAA: Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke. lakini mlinzi akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua. Yesu atanisamehe..?” SIMULIZI ZA VICHEKESHO

PADRI: “Ndio, Utasamehewa.”

JAMAA: “Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani. wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi. nikawaza mambo gani tena. akasema alirudi nyumbani na kukuta kilicho tokea akanionesha Diary ya baba yake. inayoonesha nilikuwa na appointment naye, tena Muda siuomrefu na kifo kutokea. Nikamuuliza nani mwingine anayejua..?

Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi. Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke yetu, nikamuua. Yesu atanisamehe na hilo..?”

PADRI: Kimyaa…

JAMAA: “Padri yesu atanisamehe..?”

PADRI: kimya…

Yule Jamaa akatazama kwenye confession booth padri hayupo. lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.

JAMAA: “Sasa Mtumishi mbona umekimbia..?” Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku nikagundua tuko wawili.”

Kweli Kifo Sio Mchezo, mpaka padri kasepa. Na Kila siku anaimba Wimbo Wa “KWETUUU PAZURIII, NIMESHA PAKUMBUKA…” Sasa sijui amesahau ukitaka Kwenda Mbinguni alipo Yesu lazima upite njia ya Kifo Kwanza.

Anyway, That was a Joke, Do not take it too Seriously.

Natumaini utakuwa umefurahi na Siku yako imepata kicheko. Sasa Hapa sio Mwisho wa Simulizi za Vichekesho kama hizi. Endelea kuperuzi Hapa Africona utapata Vituko Vingine Vingi.

Nawatakia Tabasamu lenye furaha 😊😊.

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

UJUGU NA POLISI KIMEUMANA - VICHEKESHO

UJUGU NA POLISI KIMEUMANA: Cheka Tu Uongeze Maisha

ACHENI TAMAA MABINTI - VICHEKESHO HAHAHA

VITUKO: “ACHENI TAMAA MABINTI” Mtakuja Kutumiwa Ata…