in

SIRI YA FURAHA – Simulizi za Kufundisha na Kukufariji Katika Maisha.

Tazama Matokeo Hapa

Download Mitihani

Siri ya Furaha ni Simulizi ambayo inaelezea Kisa Cha Kweli Kilichotokea Katoka Semina Moja Hapa jijini Dar es Salaam. Soma Mpaka Mwisho Kisha Uniambie Umejifunza nini Katika Hii Simulizi.

Siri ya furaha

 

SIMULIZI FUPI: SIRI YA FURAHA

Siku moja kundi la watu 60 walikuwa Wame Hudhuria semina moja. Ghafla mwezeshaji wa Semina Hiyo akaacha kufundisha na kutoa zoezi, ambalo walitakiwa kulifanya kwenye makundi. Kisha Akawagawa Wale Waudhuriaji wa Semina Katika Makundi.

Baada ya hapo akampa kila mtu puto na kumwambia alipulize lijae hewa na kuliandika jina lake kisha wakayakusanya na kuyaweka kwenye chumba kimoja.

Walipoyaweka kwenye kile chumba akawapa zoezi la pili kuwa kwa pamoja watumie dakika Tano ambapo kila mtu awe amefanikiwa kulitafuta puto lenye jina lake.

Waliingia mle ndani kila mtu akawa busy akijaribu kulitafuta puto lake lakini hakuna aliyefanikiwa na dakika tano zaikaisha huku kila mtu akiwa hana puto mkononi.

Mwezeshaji akasema tena haya sasa kila mtu aingie na alichukue puto lolote na kumpa mwenye jina lake.

Wakaingia na haikufika hata dakika ya nne kila mtu akawa ameshapata puto na kukaa kwenye kiti chake.

Mwenzeshaji akawaambia hongereni sana, na huu mfano unaendana sana na maisha yetu ya kila siku. ambapo watu Wengi wako busy kuitafuta furaha katika maisha yao, bila kujua furaha hiyo ipo wapi au wataipata wapi.

Furaha zetu zipo katika furaha za watu wenigne, wape furaha yao nawe utapata Furaha yako. Hii ndio Siri ya Furaha ya Kweli.

Kiukweli Sikuamini Kama Jambo Dogo kama Hili Lingeweza Kunifundisha Kitu Kikubwa kama Hiki Katika Maisha. Je, Katika Simulizi Hii niliyo Kusimulia Umepata Funzo Gani au Kitugani Tofauti na Furaha. Kama Unalo Jibu Ningependa Kusikia. Niandikie Hapo Chini Kwenye Comment.

Hili ndilo kusudio na hitaji kuu la kila binadamu

Wewe unatafuta nini katika maisha?

Furaha inatakiwa sehemu zote: Nyumbani, kazini, mtaani, shuleni na kila sehemu katika maisha yetu

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WATOTO WASIKU HIZI WANA MAMBO - VITUKO

WATOTO WA SIKU HIZI WANA MAMBO KWELI: SOMA HAPA.

swahili Love Stories

SWAHILI LOVE STORIES: Simulizi za Kusisimua na Kuelimisha