in

SMS ZA MAPENZI: Meseji za kuvutia kwa Mpenzi Wako

Sms za Mapenzi: Jipatie Maneno Matamu ya Kumueleza Mpenzi wako wako, Laazizi Kipenzi chako. Yaani hizi Meseji za Mapenzi ni Special kwa Kila Mtu alie kwenye Mahusiano. Soma hadi Mwisho utapata Maneno ambayo yata nyeshelea Penzi lenu. Siunajua tena Maneno yanaponya na Yanaua, Kua Mjanja wa Kuchagua – Japhary H. Pia Kama Unataka Love Quotes za Kizungu Bonyeza iyo link.

Meseji za Mapenzi

MESEJI ZA MAPENZI KWA MPENZI WAKO.

Kwanza Kabisa Kabla Hatuja endelea Mbele, Ukiona Unazo Dalili hizi apo chini. Jua Kabisa Umesha Penda yaani kuna Mtu unampenda. Hatakama Hujamuambia, Ishara hizi Humtokea kila mtu aliye Fall in Love.

  • Kila Mara Unakuwa Unasoma Meseji zake.
  • Kila unapo mfikiria, Moyo wako unaenda mbio kwa Upendo.
  • Pia pale unapo kutana nae, unakua na aibu.
  • Pale unapo sikia Sauti yake, Unaanza Kutabasamu bila sababu.
  • Unapo kuwa nae wakati mnatembea, huwa unatembea mwendo wa taratibu automatic.
  • Kila wakati anakuwa katika mawazo yako.
  • Muda mwingine unajishtukia ukitabasamu pale unapo muwaza, maranyingi hii huwakuta wanawake.
  • Ingawa Sijataja Jina la Mtu hapa, lakini wewe Kichwani kwako picha yake imekujia.
  • Unajikuta Unaanza Kusikiliza nyimbo za Taratibu.

Haya sasa Baada ya Kukupa Baadhi ya viashiria vinavyo onesha umesha PENDA. Basi tuangalie Sms za Mapenzi sasa.

SMS ZA MAPENZI KWA MTU UNAEMPENDA.

Ama baada ya salamu, mimi ni mzima wa afya njema. Mie ni ndege nipo angani na nimetafuta mti wa kutua kila pembe ya dunia lakini sijaupata bado. Je naweza nikatua kwako ?

Najua kuna vishawishi vingi sana uko ulipo, lakini nikiwa moyoni mwako, siku hii itakuwa nzuri zaidi kwetu, upendane daima lahazizi…

Uzuri wako hung’ara kuendana na matendo yako, Ushupavu, upole, ujasiri na uchambuzi wa kweli, kwa yote yajayo mbeleni mwako.

Mapenzi ni nini? Wale wasiopenda huita majukumu, wale wanaoyachezea huita mchezo, wale wasiokuwa nayo huita ndoto, na wale wanaoelewa huyaita mwisho wa safari, na mimi, mwisho wangu ni wewe.

Kulikuwa na vipepeo wawili waliokuwa wanapendana sana, siku 1 waliamua kucheza mchezo wa mahaba. Waliweka ua na walipanga kesho ambaye atakuja mapema na kukaa juu ya UA, atakuwa anampenda mwenzake zaidi. Asubuhi kipepeo dume alienda mapema sana na kukaa juu ya UA. Masikini kumbe jike alifika tangu jana kumwonesha mpenzi wake ni jinsi gani anavyompenda…!!

Jee…!! wewe, utamuonesha nini umpendaye ili aone ni kiac gani..?

Mpenzi unawafahamu maadui wa mapenzi yetu ? Ni wale rafiki zako wanaokuletea maneno ya uongo, ndugu zako wanaotugombanisha na wachawi wanotuotea mabaya, tujihadhari tusiwape ushindi. Mapenzi yetu yadumu daima.

Macho huona na moyo hurdhia,ila co kila kitu jicho lionalo moyo hurdhia.lakn pind moyo urdhiapo upendo moyon huingia.moyo huwa kpofu japo wng wa hisia.upendo ndan ya moyo haupimwi kwa mizani kwa unayemzimikia. moyo wangu umepata hisia Kwa flan licha bdo cjamjua.

Kuna Michezo Mingi hapa Duniani lakini kunawapuuzi wameamua Kuchezea Mioyo ya Wengine na Kuiumiza. Kama Ukimpenda Maanisha.

Moyo upendao kwa dhati. Haujalishi ni kababu au chapat. Ni wingi wa upendo wenye tarakimu kama somo la hisabati. kumpata akupandae kwa dhati pia hyo ni bahati. nimfikiriaye kwa sasa nahc anaupendo wa dhati. Nitashukuru anikaribishe naye nimuonyeshe upendo wa dhat. Huu ni ukaribisho wa penzi la dhati. Wenye wing wa furaha na Lenye pendo la kitanashati

Je unakubali au unakataa kwa mujibu wa sheria ya mahakama ya mapenzi kifungu cha mahaba unahukumiwa kuwa na mimi milele,unaweza kukata rufaa kama hujatendewa haki.sawa?

Naomba upokee zawadi hii ya kiwembe. Amini ndicho kilichotumika kufanyia operation kwa kupasuliwa moyo wangu, kwa sababu nimeoza kwa ajili yako, nimeambiwa ili nipone maradhi haya nipate:- (1)Ushirikiano wako (2)Furaha yako, (3)Upendo wako, (3)Tabasam lako.
Je! uko tayari kuokoa maisha yangu?

Pindi nikukumbukapo chozi langu huwa linatoka bila sababu,kasi Ya mapigo ya moyo Huongezea Pasipo Sababu,nimegundua Nakuhtaji Naomba Unikubalie.

Mpenzi wangu T tambua kuwa ulimwengu tunaoishi una mambo muhimu matatu. Jambo la kwanza ni kumpata umpendaye, la pili ni kupata atakayekupenda la tatu ambalo ni kubwa kuliko yote ni kwa jambo la kwanza na la pili kuungana pamoja. Nashukuru nimekupata wewe nikupendaye, naomba unipende na uungane name.

Mapenzi ni kitu kisichotabirika, ndio maana kila mwenye KUPENDA au KUPENDWA hana uhakika na PENZI lake kwa yule AMPENDAE, Muda wote huhisi anasalitiwa. PENZI Ni kama JENGO lililokosa NGUZO muda wowote unahisi litadondoka… Usinielewe vibaya sikukatazi KUPENDA au KUPENDWA. Ila tazama wapi UMEPENDA au UMEPENDWA.kilalakher kwa umpendae

SMS NA MESEJI YA UPENDO KWA YULE UMPENDAYE. MAHABA PRO MAX 😍😉.

Sms Za Mapenzi

Tone la mvua huonekana dogo sana, lakini kwa mwenye kiu hulisubiri kwa hamu kubwa. Sms ni kitu kidogo, lakini huonyesha mahali fulani yupo mtu ANAYEKUPENDA, ANAKUKUMBUKA, ANAKUOMBEA, ANAKUJALI na, ANAKUTAKIA mafanikio mema

Hii ni mbegu bora inaitwa UPENDO ipande kwa ndg zako,na pale utakapokuta imeota imwagilie maji ya FURAHA,iwekee kivuli cha USHIRIKIANO, ipalilie kwa jembe la KUSAMEHE, iwekee mbolea ya AMANI, ipige dawa ya NENO LA MUNGU, itakayoua wadudu wote waharibifu kama ubinafsi, chuki, wivu, dharau, unafki, kiburi, choyo, tamaa na fitna kwenye mmea huu, MMEA HUU (UPENDO) UENDELEE KUWA MCHE BORA KULIKO YOTE KTK MAISHA YAKO SIKU ZOTE

Usimpende mtu tuu kwa sababu uko mpweke, Au kwa sababu ana pesa, kwa sababu upendo Sio pesa wala siluhisho la matakwa yako.

Rafiki wa kweli hudhaminiwa kama familia. Pendo la kweli humaanisha, kupenda kweli Kumlinda, kumjali, kuvumilia na kusameana.

Nakutakia kila la kheri katika maisha yako ya ndoa,wengi watakuambia maneno kila kukicha,lakini nakuambia wapo ambao kwa hakika watakaokuwa wamelenga kutia doa ndoa yako, rafiki yangu kipenzi kwani wengi waitamani ndoa lakini hawajapata wa kuwaowa

UPENDO ni ubeti wa maneno yaliyo tamkwa mpaka sasa hajulikan nani alietunga!
PENZI ni hadithi iliyocmuliwa lakin mpaka sasa hafahamik nan muhucka, ndio maana kila mwenye KUPENDA au KUPENDWA hana uhakika muda wote huhis anasalitiwa.

PENZI Ni kama jengo lilokosa nguzo muda wowote unahic litadondoka… Ucnielewe vibaya ckukatazi KUPENDA au KUPENDWA, ila tazama wap UMEPENDA au UMEPENDWA! Je eti nikweli kumpenda asie kupenda ni sawa na kusubiri boti airport?

Mpenzi unawafahamu maadui wa mapenzi yetu ? Ni wale rafiki zako wanaokuletea maneno ya uongo, ndugu zako wanaotugombanisha na wachawi wanotuotea mabaya, tujihadhari tusiwape ushindi. Mapenzi yetu yadumu daima.

Mapenzi si pombe lkn yanalewesha, wala si kidonda lakini yanatonesha,wala si maradhi lakini yanaumiza, wala si njaa lakini yanakondesha ,mapenzi ni uvumilivu kwa unaempenda.

“Watu tumeumbwa Kupendana. Vitu Vimetengenezwa Kutumiwa. Sababu inayopelekea mambo kuwa magumu ni kwamba,watu wanapenda vitu, na kutumia watu.”

“Tumepewa Mikono Miwili, Macho Mawili, Figo Mbili, Miguu Miwili. Ila Kwanini tumepewa Moyo Mmoja..?”

Soma Simulizi za Mapenzi Zifuatazo kwa kubonyeza hiyo picha Hapo chini. Nauhakika Utajifunza Mambo mengi.Kuhusu Mahusiano.swahili Love Stories

Je Ungependa Kupata Sms za Mapenzi Nyingine kama Hizi. Meseji za Mapenzi kama hizi zitakuja. Chakufanya endelea kutembelea hapahapa kwenye tovuti hii ya Africona.

Written by Teacher Pizo

My Name is Teacher Pinael Zakaria Olais. Wengi wamezoea Kuniita Teacher Pizo. Nipo Hapa Kuwasaidia wanafunzi katika Masomo yao. Niandikie Swali lako Hapo Kwenye Comment nami Nitakujibu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

MATOKEO KIDATO CHA NNE - NECTA CSEE RESULTS 2022-2023

MATOKEO KIDATO CHA NNE: NECTA CSEE Results (2022/2023)

GEOGRAPHY PAST PAPERS FORM FIVE AND SIX

GEOGRAPHY PAST PAPERS A-LEVEL: Form Five and Six Free (PDF)