in

SMS ZA VICHEKESHO Vunja Mbavu: Maneno ya Kuchekesha 😂.

SMS ZA VICHEKESHO VUNJA MBAVU - MANENO YA KUCHEKESHA

SMS za Vichekesho Vunja Mbavu, Maneno ya kuchesha mpaka Mbavu ziume. SMS Hizi pia unaweza Kumtumia Rafiki yako au mtu yeyote Umpendaye. Na yeye aanzeku cheka tu Maisha ndo Hayahaya. Haipendezi Kununa. Pia Kama Unahitaji Sms za Mapenzi Bonyeza Hiyo Link.

Enjoy na SMS za Vichekesho Vunja Mbavu.

SMS ZA VICHEKESHO NA MANENO YA KUCHEKESHA 😂.

“Wa Tanzania ivi Kale katabia umeme ukikatika mpaka Utoke nje Kuchungulia kama wamekata Pote. Mlikatoa Wapi..?”

“Kiporo Kinaitwaje kwa kiingereza..?”

“Tumefikia Umri ambao Hujui umpe Mtu Salamu gani MAMBO, SHKAMOO, AU ZA SAIZI… yaani Tabu tupu.”

“PENZI LIKIWA JIPYA

Demu: Baby Sipati Usingizi.
Jamaa: kuna Tatizo Gan My Wang.
Demu: Ni Mbu my.
Jamaa: Wapo wangapi Hao bby?
Demu: Wanne.
Jamaa: Paa, Paa, Paa, Paaa.
Demu: asante Bby, Uko Romantic 🥰.

“Leo nimejiangalia Kwenye Kwenye kioo Weeeh! Chamuhimu niko na Roho Safi.”

“ME: Mama nikifika Umrigani ndio nikakua narudi Nyumbani mda ninao Utaka..?
MAMA: Hata Baba yako Huo Umri Bado Hajafikisha.”

“Upo Single kwa Sababu ukitokaga Kanisani unaondoka Mbio Mbio. Acha ufala, Zubaa Zubaa uki Salimia Watu. Utanishukuru Baadae 😎.”

“Hatukatai Upo Chuo, ila Ndo uje na Laptop Msibani Kweli…”

“Unasura Mbaya alafu unataka ICE CREAM, na UJI anywe nani Sasa.”

“Upo kwenye kundi gani la Utajiri Mpaka Sasa Hivi..?”

Trillionea.
Billionea.
Millionea.
Lakionea.
Elfuonea.
Mnanionea.

I LOVE YOU CHOLOCATE”. Rudia kusoma mbwa wewe, ndo Maana Ulifeligi Shule hivi Hivi.”

“Unashangaa nikikuambia Sina Hela, Kwani Wewe unazo Sasa.”

“MIMI: Baby Wanasema Hujui kuongea English.
HER: Who speaked Those Said.”

“Nimeweka zangu Vocha, Kwa Bahati Mbaya nikasahau kuunga Kifurushi. Sinikawasha Data, ile nimewasha Tu nika kumbuka Sijajiunga Nikazima Chap. Mara SMS ikaingia Kutoka Voda “Unabahati Matako Wewe!”.”

“Wanaume Tukizubaa Hatazile 50%. Tuta bakishiwa 20% tu.”

“Ivi Kwanini 3 ina Herufi Nne, na 4 iko na Herufi tatu..? Mwenye Jibu atuandikie hapo kwenye Comment Chini ya Website Hii.”

“Shida ya Kula Sikuku kwa watu, hata Mtoto akichua Nyama Kwenye Sahani yako wewe kazi ni Kucheka Cheka Tu.”

“Hakuna Hesabu ngumu kama Kumtoa Pisi kwenye kiti, Mpaka kitandani.”

“KOIKUAKOUKOIKUOKOKO.” Una Soma nini Sasa Mbwa wewe.”

“Inauma Sana umalize kugombana na Mtu. alafu ukumbuke Matusi Mengine Very important.”

“Hivi Wale Mlio Semaga Mwaka 2022 ni Mwaka wenu. Mnaendeleaje na Mwaka wenu.”

“Siku Moja Utajikuna Matak0 Kupitia Fungua Za gari yako. Sema AMEN🙏🏽.”

“Kama PUNDE SI PUNDE. PUNDE ni nini Sasa..?”

“Mimi mara yangu ya Kwanza kufika Zanzibar.

WENYEJI: Kaka Sisi Twala Karibu tule.
MIMI: Nyie Tuleni tu mimi nilisha TWALA.”

“Hii Kauli 👉“Maisha ndo HayaHaya”. Imenimalizia Pesa Sana.”

“Unaunga Meseji (SMS) za mwezi za nini na Upo Single. Au unataka kuchat na Mashetani..?”

“Rafiki yangu wa kishua amesikia Tumbo langu linanguruma. ananiuliza Unafanyaje io embu nifundishe na Mimi.”

“Usiibiwe tena Mchele Ukienda Dukani 1Kg ya Mchele ina Punje 168,369. (Rafiki yangu wa kipare Kanitumia Leo.)”

“Tafuta Hela Wewe ili Jumamosi na Jumapili ziwe siku za Weekend. Sio siku za Kufua.”

“Mliokuwa mnasoma Topics za Mbele kabla Mwalimu Hajafundisha. tuambieni Basi 2025 nani Atashinda.”

“Hatakuolewa Hujaolewa Ushaanza Kuota unagombana na Mume wako.”

“Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.”

“Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.”

“Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?”

“Ukichanganya (wali + choroko = Mseto), lakini hautibu malaria.”

“Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.”

“Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.”

“Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.”

“Hatakama ni Maisha yako, Ndo unywe Pombe na Vitumbua Kweli..?”

“Wanaume tulipewa laana Moja tu “Tuta kula kwa jasho”, Hii nyingine ya kula kwa macho tunajitakia Wenyewe.”

“Utajiri Hautakagi Kelele ndo maana Ukienda Bank Huwezikuta zile Tv Zao zina Sauti.”

“Lipa Nauli ya Dar to Mwanza. Upite Dodoma, Morogoro, Singida na Tabora Bure.”

“Unaturingia Una mguu wa Bia na Ukija Baa unataka Tukununulie Bia. Siunywe Mguu wako sasa.”

“Kumpenda mtu anaekupenda Raha Asikuambie mtu. Ila mimi Mwenyewe nasikiaga tu.”

“Kama Tukiendelea kuvaa Barakoa Miaka Mitano Baadae, Watoto watakao Kuja Kuzaliwa watajuaga Pua na Mdomo ni Sehemu za Siri.”

“Bongo Bhana Unabisha Hodi kwa Mtu anakuuliza “Nani Wewe..?”, Unasikia “Ni mimi””

“Tangu Asubuhi kwenye simu yako SMS (0) Missed Call (0). Ndugu wewe Sio Single, Wewe ni Singular.”

“Huwa najiulizaga Wale Wanafunzi waliokuwa Wakimkimbilia Mwalimu na Kumpokea akiwa anaingia Darasani. Sasa Hivi wako wapi..?”

“Usikute Hata Msaga Sumu Hana Mashine alikuwa animba Tu..”

“Hatukatai wewe ni Mzuri ila Unavyo kigawa Sasa utazani kofia za Kampeni.”

“Nimesha Chagua Nyimbo za Kusikiliza Kwenye Gari yangu… Sasa bado kununua Gari Lenyewe.”

“Kuwa Single nako ni kazi aisee, Ukiwashwa Mgongoni Kuna Mawili… 1. ujikune na Chanuo la nywele. 2. au UjiBuruze Ukutani kama Mbuzi.”

“Huna Hela, Huna Nguvu za kiume. Una nini Bro..?”

“Eti kwavile nilikuambia Jisikie Upo nyumbani, ndo ukaange Mayai Nane. Uliyataga Wewe…”

“Acha Kutamani Boyfriend Wa wenzako, Mwambie Boyfriend wako awe anaoga Vizuri, Anapiga Mswaki, Anavaa Vizuri pia Awe anakula Vizuri na Aaache Kuvuta Bangi..”

“Kizungu zungu Kwa kiingereza Kinaitwaje..?”

SMS ZA VICHEKESHO VUNJA MBAVU CHEKA TU.

“Wajumbe nawakumbusha tu..

Ukiwa na Mwanamke PESA Hazikai.
Ukiwa Hauna PESA wanawake Hawakai.”

“Sawa atakama ni Msukuma, Sasa ndio uchore Tatoo ya SATO Jamani.”

“Ugali kabichi Tunakula Tusife Jamani, Hamna Kitu pale. Tuwe wa kweli.”

“Kama mimi Nilishaitwa Mstarini nikaambiwa niache kujikojolea Kitandani. Unadhani ukiniambia Mbele za watu “You are not my Type.” Nitaumia.”

“Pisi Kali zote Namba za Viatu Mwisho ni 38. Kama unavaa kuanzia 39 na kuendelea wewe ni AFANDE SELE.”

“Vile Mimi nilivyo na Heshima. Nikipanda gari nikaona kuna Mama Mja mzito au wazee (awe Bibi au babu). Mimi naweka Earphone na Pia na Fumba Macho, wajue nimelala.”

“Relationship Za Sikuhizi kama Kufanya Kazi kwa wahindi. Kosa Kidogo Tu, unambiwa kesho Usirudi Tena.”

“Hii mitandao ya Kijamii imeharibu Sana Akili za Watu. Yaani kunajamaa Kakutana na Pisi Kali Kapendeza aka mwambia “Wow Nice Photo”.”

“Usikate Tamaa kisa amesema Ana Mtu wake. Kumbuka Watu wanakufa 😁.”

“Nawaza hapa Kama Yona angekuwa Mpare. Pale alipo medhwa na Thamaki angempigia Simu Mkewe amuambie. “Andaa Ugali Mke wangu nipo ndani ya Mboga.”

Yaani kumtest Speed huyu Kuku 🐓 wa Jirani imekuwa Tabu. Washaanza Kuniita Mwizi.

Sio Kwamba Unapenda Sana Miguu ya Kuku. Sema Tu huna hela, Hakuna Mtu Anaweza kuacha Kidari na Paja akala miguu ya kuku.

Jana Nimeota Nimefunga Ndoa. Acha Leo nilale Mapema niende HONEYMOON.

TUANDIKIE WAZA LAKO LA LEO HAPO KWENYE COMMENT

Wazo la Leo - MSM na Picha Za Vichekesho 2022

Comment ujumbe mwingine uliowahi kuuona kwenye daladala

Je, ni SMS za Vichekesho kati ya Hizi ime kuchekesha mpaka Mbavu zikauma ukahisi kama Mbavu zinataka kuvunjika 😂😂. Nijulishe Hapo chini Kwenye Comment SMS za Vichekesho ziliyo Ku Vunja Mbavu, itakua Poa Sana. Mimi binafsi ile ya “Lipa Nauli ya Dar to Mwanza. Upite Dodoma, Morogoro, Singida na Tabora Bure.

Pia Kama Ungependa Ziongezwe SMS Nyingine za Vichekesho nijulishe Hapo Ci.hin

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

 1. Hii ni Baadhi ya Misemo Niliyo Kutana Nayo Kwenye dala dala za Hapa Arusha

  “MCHAWI MTU, PAKA KATUMWA”
  “Toa zaka , hujarogwa!”
  “Tafuta hela upunguze kujieleza”
  “Punguza maua kwenye harusi ongeza kuku”
  “Tafuta hela maharage kwenye gesi yanaiva”
  “Tafuta Hela wanawake wote wapo singo”
  “Chafya ya mpishi ni kiungo kwa walaji”
  “Mkanye mkeo gari sio yangu”
  “Punguza wema binaadamu hawana kumbukumbu”
  “Kunenepa wakati na kudai ni dalili ya zarau.”
  “Utajir hauambukizwi kwa njia ya ngono, piga kazi acha kudanga😂😂😂😂”
  “Tafuta pesa usilaumu ndugu”

How to Make Money Online in Tanzania (2022)

How to Make Money Online in Tanzania: $100+ Monthly (2023)

MATOKEO KIDATO CHA PILI - NECTA FTNA 2022-2023

MATOKEO KIDATO CHA PILI: NECTA FTNA Results (2022/2023)