Swahili Love Stories: Simulizi Saba Bora za Mapenzi zilizo andikwa kwa Lugha ya Kiswahili na Mtunzi wako Mahiri @japhary . Katika Simulizi Hizi Utakwenda Kujifunza Mambo mbalimbali yaliyo wakumba wapenzi katika mahusiano yao. Ungana nami Mwanzo hadi mwisho katika hizi Love Stories nauhakika utazipenda.
LIST OF BEST SWAHILI LOVE STORIES.
- #1: SIMU YA MAUMIVU.
- #2: HERI YA KUZALIWA.
- #3: PENZI LA SIMANZI.
- #4: UPENDO WA KWELI.
- #5: NIMESHINDWA KUKUSAHAU.
- #6: LAITI NINGEJUA!
- #7: KWANINI UMENIACHA HIVI?
#1: SIMU YA MAUMIVU.
Palikuwa na Kijana pamoja na Msichana Mmoja waliokuwa marafiki sana. Walikuwa wanaweza kuzungumza Kwenye simu Kwa muda mrefu sana pasipo kuchoka.
Na pindi ambapo wakiwa wanazungumza katika Simu, ilikuwa ni kama Hamna tatizo hapo Duniani kabisa kwa mazungumzo waliyokuwa wakiongea. Kama unavyo jua Masuala ya Mahusiano yakiwa yamepamba moto.
Siku Moja, Siku moja Binti alimtumia Sms Kijana lakini Haukujibiwa na Haikuwa kawaida. Aliendelea kumtumia Message lakini Hakukuwa na Majibu yeyote. Mwishowe, Aliamua Kumpigia Simu lakini Haikupokelewa.
Siku nzima Ilipita pasipo kijana Kuwa Hewani, Binti alijaribu Kutuma SMS na Kupiga Simu pasipo Majibu. Binti alianza Kuingiwa na Uwoga na Kupata hofu kuhusu Kijana ampendaye
Usiku uliofuata, Binti alikaa macho Usiku Kucha Akimuwaza kijana ampendaye na Kuanza Kulia. Huku akiwaza kuhusu Upekwe alio kuwa nao Kwa Kutowasiliana naye kwa muda wote huo.
Hasubuhi iliyo Fuata, Binti alipigiwa Simu. Alikuwa ni Mpendwa wake! Binti Alipata Furaha Sana Baada ya kuona kijana Amepiga Simu, Kisha Akapokea…
Mvulana: Hey!
Msichana: Nimefurahi kukusikia, Nini Kilitokea?
Mvulana: Nili… Nilikuwa… busy.
[Msicha Alianza Kuona mambo hayapo sana, ila Hakuongea chochote.]
[Ukimia ukatawala Kwa Muda Fulani]
Mvulana: Unajua nini, Unaonaje tukiachana. Tusiongee tena.
Msichana: [Binti akaakimia Kidogo kisha aksema] Kwa nini? Why?
Mvulana: Sorry. Bye.
[Kijana Akakata Simu. Binti hakuamini macho yake, Alikaa Kimia. Aliona nikama Moyo wake umepigwa Shoti]
Akiwa amebakikimia Huku kumbukumbu za Mtu ampendaye zikimjia mbele ya Macho yake.
Alianza Kulia, Machozi yalianza Kutirirka Machoni taratibu kwa Huzuni.
Binti alikuwa nikama amechanganyingiwa haelewi cha Kufanya.
Alihisi Moyo wake ni kama Umevunjika, Alibaki na Huzuni akiwa Pekeyake.
Wakati huo alikuwa yupo juu ya Nyumba yao ya Ghorofa, Alitamani hata Kujirusha .
Akikumbuka ndie Kijana Pekee aliye Mpenda kwa dhati, Kwa nini amemfanyia Hivi?
“Why?!” Alipiga Kelele .
Alikaa kwa Muda Kisha akawaza lazima Ampate tena Mtu ampendaye.
[Kisha Akapiga Simu]
Msichana: Hey
Mvulana: Umenipigia Kwa Nini?
Msichana: Nahitaji Kukuambia Kitu.
Mvulana: Haya niambie.
Msichana: Nahitaji kukuambia Kitu Kimoja tu…
[binti alizungumza Kwa Hisia uku akiwaza. “Nadhani hata Ajali kuhusu Mimi,” .]
Mvulana: Sema!
Msichana: Uko Salama?
[Ukimia Ukatawala]
Machozi yalimtiririka tena Binti. Akakata Simu, na Akaamua Kuandika Ujumbe kwenye Karatasi Kisha Akatokana Kwao Akikimbia Kumfuata Kijana.
[Muda Ulipita Takribani Masaa Sita Hivi]
[Simu ikawa inalia Kwa Kijana]
Baada ya Kupokea, Alizungumza Mama yake na yue Binti. Binti yangu amogongwa na Gari wakati akija Kukuona, Hivi sasa tunavyo ongea Yupo Hospitali.
Kijana aliharakisha na Kukimbia katika Hospitali aliyo pelekwa Binti.
Baada ya Kufika Aliomba Kuzungumza nae. Kisha Akamuita na Kufungua Macho.
Mvulana: Tafadhali utakuwa Salama, Naomba Nisamehe.
Msichana: Kwa nini umefanya Hivyo?
Mvulana: Nina Ugonjwa wa Moyo kwa Muda Mrefu, Hivi Sasa Nimebakisha Siku Chache za kuishi. Na nisingependa Kukuachia Maumivu.
Baada ya Kusikia Hivyo Binti, Alifunga Macho yake. Na Hakuyafumbua Tena.
Kijana Hakuamini kwa Kilicho tokea, na yote ni kwasababu yake.
Baada ya Dakika Kumi Baadae Kijana Alipata Mshtuko wa Moyo na Kupoteza Maisha.
*MWISHO*
Katika Swahili Love Stories Hii Unazani kama ikatokea wamekutana Mbinguni wataendelea Kuwa Pamoja. Nijulishe hapo chini Kwenye Comment.
#2: HERI YA KUZALIWA.
Binti: Happy birthday baby!
Kijana: Thank you sweetheart 😊
Binti: Nitakuja Kukuwish Kwenye Saa Mbili.
Kijana: Sawa Mpenzi, Unaniahidi?
Binti: Ndio, Nitakua Hapo Haijalishi Kipi Kitatokea. I love you.
Kijana: I love you baby, Basi Ngoja Niandae Chakula Kwaajili yetu!
Binti: Sawa! Tutaonana.
[Saa mbili Usiku Ilipofika, Hapakuwa na Dalili za Mtu Kufika Kijana Akaendelea kusubiri. Lisaa Limoja Lilipita pasipo Binti kutokea. Baada ya Kufika Saa Tatu na Nusu. Binti Alifika]
Kijana: Hi babe. Nimefurahi Kukuona. Mbona umechukua Muda Mrefu kufika?
Binti: *Binti alimkumbatia Kipenzi chake na Kumuambia* Sorry sweetheart, Kulikuwa na Foleni.
Kijana: Usijali, Nimefurahi kukuona.
Walikuwa na njaa, Hivyo walizungumza Kidogo kisha Wakapata Chakula.
[Ghafla Simu ikapigwa ya Kijana, Kuangalia akaona ni Mama yake Binti]
Kijana: Shkamoo mama
Mama wa Binti: (Sauti, ya mama ikiwa kama analia.) Hujambo mwanangu, Nasikitika Kukutaarifu kwamba Trisha Hatunaye tena, Ameiaga Dunia *Mama Aliangua Kilio cha Uzuni*
Kijana: Unasema.. Sijaelewa mama?
Mama wa Binti: Mwanangu amepata Ajali… Alipo fikishwa Hospitali Akaiaga Dunia … (Mama Ameongea Kwa Uchungu na Kushindwa Kuzungumza tena)
Kijana Akamgeukia Binti… Kisha akamuona ameshika Mshumaa, (Kumbuka ni Siku ya Kuzaliwa ya Kijana)
Binti: Nilikuambia Lazima nifike. Usiogope Mpenzi, Nitakuwa na Wewe Milele.
*MWISHO*
Katika Swahili Love Stories nina Swali moja kwako, Je unazani Upendo kama Huu Upo kati ya wapendanao sikuhizi. Nijulishe hapo chini Kwenye Comment Mtazamo wako kuhusu Mapenzi ya Kweli.
#3: PENZI LA SIMANZI.
Kijana Mmoja Alikuwa Akisumbuliwa na Ugonjwa wa kansa, Muda mwingi alikuwa akiishi ndani, huku mama yake akichukua uangalifu juu yake.
Siku moja Kijana Huyo Alitamani kutoka, Ingawa mama yake alikuwa akisitasita Aliamua Kumruhusu. Alitambua Mwanawe amechoka Kukaa ndani pekeyake kwa Muda. Hivyo aliona ni vyema Kumuacha Aende akatembee tembee.
Basi Kijana akawa Ametoka, na Kuelekea kwenye Duka linalo uza CD. Kisha akaingia ndani. Baada ya Kuingia ndani alishangaa sana Baada ya Kumuona Mwanamke Mrembo sana. Moyo ulitokea Kumpenda Ghafla kwa Mara ya Kwanza tu, Alivutiwa nae sana.
Kisha akaamua Kumfuata, katika meza alikua amesimama huku akiudumia baadhi ya wateja. Ilipo fika zamu yake ya Kuhudumiwa Kijana, Yule binti alimpatia tabasamu Kisha kumuuliza. “Nikusaidie nini?” Aliongea kwa Sauti nzuri sana yenye upole na ukarimu. Kijana aliwaza ata Ampatie busu, ila aliwaza itakua ni jambo la Kijinga, Hivyo alisita, kisha akazungumza.
“Nilikuwa… nahitaji kununua CD,” Alizungumza Kijana. Kisha akachagua CD tub ila ata kuangalia kisha Akalipia.
“Ungependa nikufungie?” Binti alimuuliza, Huku akimpatia tabasamu la bashasha.
Kijana akatikisa Kichwa kuashiria amekubali.
Binti alienda Kuifunga Ile CD KIjana alienunua. Kisha akampatia Kijana na Kuondoka.
Siku iliyo Fuata Kijana alikwenda tena Kwenye lile duka, Akanunua tena CD na Kufungiwa kama Kawaida. Lakini alitamani kumuambia ya Moyoni ila moyo wake ulisita. Kijaan aliendelea Kununua CD katika Lile Duka kila Mara kwa Takribani wiki Mbili. Kila Alipo kuwa akinunua zile CD alikua akizificha Kabatini kwake.
Mama yake aligundua kuhusu swala la Kijana wake, Na kumuambia asigope azungumze naye yule Binti. Siku Hiyo alienda Kununua CD kama kawaida, Baada ya Binti kwenda kumfungia CD yake, Kijana aliandika namba yake pale Kisha akaondoka Bila Kuchukua CD.
[Siku zilipita, Siku moja Simu ikawa inaita]
Mama wa yule kijana akapokea, Alikuwa ni yule Binti. Alihitaji kuongea na yule kijana. Mama aliongea kwa masononeko, akamwambia Mwanangu amefariki wiki iliyo Pita.
Baada ya Hapo mama aliamua Kwenda kwenye Chumba cha Mwanawe, Kwa kuwa alimkumbuka.
Kisha akafungua kabati lake na Kuangalia vitu vya mwanawe. Alishangaa kuona CD nyingi ambazo hazija Funguliwa. Baada ya Kufungua CD Moja alikuata kaujumbe. Ulikuwa umeandikwa na yule Binti. “Hi, Unajua ww ni Handsome jamani, Ningependa Siku moja Tutoke Out Pamoja?”
Mama akafungua CD nyingine. Lakini Kila CD ilikuwa na Ujumbe Huo huo katika CD Zote…
*MWISHO*
Katika Swahili Love Stories Unazani ni Kwanini Kijana Huyu Hakufungua CD Alizokuwa akinunua, je, Ni kwasababu Hakuwa na Lengo la Kuzisikiliza au Hakuwa anataka Kumuumiza Mtu kwa Maana ya Kwamba Apendane na Mtu ilihali anajua Amebakusha Mda Mfupi Duniani. Nijulishe hapo chini Kwenye Comment.
#4: UPENDO WA KWELI.
Siku Moja Kuna Kijana Alikutana na Mzimu. Mzimu huo Ulikuwa ni wa Rafiki yake waliopotezana Kwa Muda Mrefu.
Kijana: Ilikuwaje Mpaka Ukafariki?
Mzimu: Niligongwa na Gari.
Kijana: Ulikua Unavuka Barabara au ilikuaje?
Mzimu: Kitu kamaicho.
Kijana: Unamaanisha nini?
Mzimu: Nilikua najaribu kumsaidia Mtu.
Kijana: Kwanini lakini?
Mzimu: Sikutaka Athurike.
Kijana: Umetoa Maisha yako sadaka kwaajili ya Mtu Unaempenda? Nadhani atakua anahudhunika sana kwa kukupoteza.
Mzimu: Hapana, Anayo furaha, Kwa Sababu niliye Msaidia ni Mpenzi wake…
*MWISHO*
Unamaoni gani Katika Swahili Love Stories Hii, je, unazani Kijana Huyu Aliye Kufa Kwaajili ya Mpenzi wa mpenzi wake amefanya jambo la Kijinga au amefanya ivyo baada ya Kuona Mpenzi wake anampenda sana Uyo jamaa na Kuona Amsaidie. Nijulishe hapo chini Kwenye Comment Maoni yako Kuhusu ichi Kisa.
#5: NIMESHINDWA KUKUSAHAU.
Wapenda nao wawili waliamua Kuachana katika Mahusiano yao. Ingawa Kijana Hakupenda Kuacha na Mpenzi wake, aliamua kukubali kishingo upande.
Baada ya Miaka Mingi Kupita, Jamaa alipata Mtu mwingine na Kuamua Kumuoa.
Baada ya harusi kupita, Ex wake na Jamaa Alimfuata. Nakuongea nae.
“Kwa nini umetumia Rangi ninayo ipenda Kwenye Harusi yako, Maua Niyapendayo kama Mapambo na Tarehe tuliyo kutana kama Siku ya Harusi yako? Kwa nini Umefanya Hivyo?”
Jamaa Alianza Kulia Hukua Akiongea Kwa Sauti ya Huzuni, “Hii ndo njia Pekee… Njia pekee ambayo ningeidanganya nafsi yangu… Yakwmba yule ninaye muoa ni wewe.”
Binti Aliondoka Akiwa Analia kwa Uchungu Huku akijutia Maamuzi yake ya Kuachana na Mtu Aliye kuwa Anampenda Kwa Dhati Mno.
#6: LAITI NINGEJUA!
Kijana MmojaAlikuwa Anamahusiano na Mwanafunzi mwenzake wa Chuo. walikuwa wakipenda Sana. Siku moja Walikuwa Wakichati.
Kjana: Mambo Mpenzi! Unaendeleaje?
Msichana: Embu Subiri Kidogo, Nipo Busy Kuna Kitu nafanya, Mtakutafuta Baadae.
Kijana: My, Unaweza Kunipa japo dakika chache? Kunajambo la Muhimu nahitaji kuongea na ww.
Msichana: Nimepewa Muda wa Kukamilisha ninacho kifanya, Hujajua kwani?
Kijana: Japo Kidogo tu my, Tafadhali? Unadhani tutachati Muda Mrefu?
Msichana: Unajua Hii kazi inaumuhimu gani kwangu? Kwanini unanisumbua? Tambua ninayo maisha yangu!!!
Kijana: Samahani kipenzi, Ntakutafuta Baadae.
[Baada ya Muda Kupita…]
Kijana: Hey darling, Siwezi Kukaa mbali na ww Muda mrefu… Kazi yako Umemaliza?
[Kimia]
Kijana: My, Muda Umeenda sasa. Kwann Haujibu? Ninapata wasiwasi!
Msichana: Kwani sijakuambia ninakazi namalizia? Ntakutafuta Nikimaliza. Sawa? Sio kama Hatuta Ongea Kesho … We lalatu my, Sawa?
Kijana: Sorry babe. Goodnight. Mungu akulinde.
[Siku iliyo Fuata]
Msichana: Samahani my, Jana Kweli nilikua Busy. Amka! Leo Umesahau ni Chuo. Nijibu Tafadhali.
[Kimia, Muda Ukapita]
Msichana: My, Mbona Hunijibu? Au Hauna Salio, Nimuda wa Chakula Sasa. Uko wapi? Mbona Sijakuona Class?
[Mara Simu Ikaita, Kuangalia ni namaba ya Mpenzi wake]
Mama wa Kijana: Patrick Hatuo nae Tena. Mwanangu hayupo tena. Tulijaribu Kumuamsha lakini hakuamka, Na Madaktari wamedhibitisha Ameiaga Dunia.
Miaka Mitatu iliyo Pita Mwanangu alikuwa anaumwa na Ugonjwa wa Moyo, Madaktari wakasema Ataishi Miaka miwili Ila Mungu Alimsaidia akaishi Mitatu Mpaka Sasa.
Nakatika Simu yake Nilikuta Ujumbe Alio kuakitaka Kuutuma Kwako ndio Maana Nimekupigia Kukupa Taarifa Hizi, Ujumbe Wenyewe Nimekutumia…
“Chukua Uangalifu Mpenzi wangu. Mimi nitakuwa na Furaha Huku niendapo. Na ninahitaji na wewe Uwe na Furaha. Naomba Unisamehe Sana, nilikuficha Kuhusu Hali yangu. Lakini Sikutaka Kuku Umiza. Najua Ulikua Busy Ukikamilisha Kazi yako ya chuo, na ninatambua Umuhimu wake. Nakupenda SanaNinajutia yakuwa hatukuweza Kuongea Leo Muda Mrefu, Ila Natambua Umuhimu wa Project uliyo kua unaifanya. 1 love you very much. Niahidi ya kwamba Utakua Jasiri Katika Wakati huu Mgumu, Pasipo kuwa na Mimi.”
*MWISHO*
Kiukweli Katika Swahili Love Stories hii wakati naiandika Mwenzenu machozi yalikuwa yanatiririka. Ila nina Swali moja Kwako Mpenzi wa Simulizi hizi, je unazani Huyu Binti anamakosa Kwa kuto jibu Message za Huyu Kijana, au Kijana Aamakosa Kwakuto mpataarifa juu ya Ugnjwa wake wa Moyo. Nijulishe hapo chini Kwenye Comment.
#7: KWANINI UMENIACHA HIVI?
Boyfriend Alikua na Girlfriend wake Usiku wakielea Nyumbani. Walikua Katika Pikipiki.
Girlfriend: Tafadhali naomba Upenguze mwendo? Naogopa.
Boyfriend: Usijali my… It’s fun!
Girlfriend: Hapana Haifurahishi Kabisa. Tafadhali nakuomba Upenguze Mwendo, Naogopa.
Boyfriend: Kama Unataka Nipunguze Mwendo niambie Unanipenda.
Girlfriend: Sawa, I love you. Punguza Sasa Tafadhali!
Boyfriend: Nikumbatie kwanza!
(Binti akamkumbatia)
Boyfriend: Tafadhali chukua Helmet yangu Kisha Uvae wewe, Mimi inaniboa.
Siku iliyo Fuata, Taarifa ya Habari Ilitangaza Habari ifuatayo:
“Watu wawili wapata ajali ya Pikipiki. Ni Baada ya Brake Kufeli. Mmoja wao Ametoka Salama, ila Mwingine Amepasuka Kichwa Vibaya.”
Kipindi ambapo Kijana Anaendesha pikipiki aligundua yakwamba Brake Hazifanyi kazi. Hivyo, Aliamua Kumpa ile Helmet ili Asidhurike Endapo Chochote kikitokea.
Hizo ndizo Simulizi Saba Nilizo Kuandalia Mpenzi wa Simulizi za Love Story, ama kwa Upande wangu naweza Kuziita Best Swahili Love Stories. Ningependa Kusoma Maoni Juu ya Simulizi Hizi, Maana Najua tu Kwa namna Moja ama Nyingine itakua Zimekugusa Moyo na Kukupatia Funzo.
- 254shares
- Facebook186
- Twitter68
- Gmail
- Copy Link