Vichekesho Vunja Mbavu : Huyo Total Atalipa Mwenyewe. Soma Mpaka Mwisho utafahamu kilicho jiri. Kwani Total Mwenyewe anasemaje..?
Usisahau kuni Follow @japhary kwa Vichekesho na Mada Mbalimbali za Kuvutia. 😊
VICHEKESHO – HUYO TOTAL ATALIPA MWENYEWE.
Ilikuwa ni Jumamosi moja Katika Baa Moja Hapa Marangu. Masawe alikuwa amekuja kutembelea Marafikizake Hivyo mida ya jioni Kama Tunavyo jua Wachaga wazee wa Mbege. Basi Masawe akaenda kupata Moja Baridi Moja Moto. Ukizingatia masawe alikuwa yupo vizuri Mapene anayo Warembo Wakajichanganya. Bila Uchoyo akawazungushia kama walivyo.
Baada ya Watu kupiga vyombo Bili ikaja Kama ifuatavyo…
Mankaa = 35,000 Tsh.
Marieta = 20,000 Tsh.
Monika = 30,000 Tsh.
Gilo = 15,000 Tsh.
Tina = 10,000 Tsh.
TOTAL = 110,000/=
MASAWE akaicheki akasema “Wote nitawalipia” lakini huyo “TOTAL” Yesuu simlipii, Huyo Total atalipa Mwenyewe. Kwansa anamiliki sheli nyingi sana Hapa mjini. “Nomanya Kumonyi..!” Na amekunywa nyingi kuliko wote alipe mwenyewe…
(“Nomanya Kumonyi” = Atajua Mwenyewe.)
Kweli Wachaga mmezidi Aise. Sasa na ujanja Wote uo Masawe umeshidwa kujua (Total = Jumla). Anyway Hichi ni kichekesho Wachaga Msije mkanikaanga Kwenye Comment Kiruu..! 😁.
- 200shares
- Facebook127
- Twitter73
- Gmail
- Copy Link