Kwenye Hadithi yetu hii ya Tusiwadharau wadogo, tutakwenda kujifunza mambo mengi ya msingi na ya muhimu kama ilivyo kawaida ya simulizi zetu huwa zinafundisha na kufurahisha. utafahamu ni kwa nini kinyonga anabadilisha rangi.
HADITHI ZA KALE: TUSIWADHARAU WADOGO.
Hapo zamani za kale alikuwepo Mfalme ambaye alioa na kupata mtoto, wa kike. Alikuwa mzuri na akasifiwa na kila mtu katika kijiji chake. Siku moja walijitokeza marafiki wawili, Ng’ombe na Kinyonga na wakaanza kumsifu yule mtoto kwa ajili ya kutaka kumuoa. Kati ya wale marafiki kila mmoja alitaka kumuoa yule binti.
Kati ya wale marafiki kila mmoja alitoka kisiri siri na kwenda kwao kumposa bila ya mwenziwe kujua.
Mfalme aliposikia vile aliamua kupigisha mbiu kwa ajili ya kuitisha mkutano.
Mfalme aliwajuilisha lengo la kuwekwa mkutano ni posa ya mwanawe na kuoneshwa waposaji hao,
Ng‘ombe na Kinyonga. Waposaji hao walikuwa wote ni marafiki. Kila mmoja alistaajabu kuona wanagombania mtu mmoja. Mfalme alitoa siku na alisisitiza na kusema ataefi ka mwanzo ndie ataeowa. Kuona vile ng’ombe alimcheka kinyonga na kumdharau, kwa kumuona kinyonga ni mdogo sana na kumuona hana mwendo.
Siku ilipofi ka ng’ombe alijiandaa na kinyonga alijiuliza, nitafanya nini mimi nifi ke mapema nipate niwahi na mimi mwendo wangu mdogo mdogo? Lilimjia wazo zuri na kuanza kupanga, kinyonga alipanga kama hivi: Atatoka kwake mapema kabla siku ya shughuli na kukaa kwenye tawi la mti. Siku ilipowadia
Ng’ombe alikamilisha ahadi yake, alianza kutoka mbio kwake alipofi ka tu kwenye mti kinyonga aliurukia mkia wa ng’ombe bila ya yeye mwenyewe kujua kama Kinyonga kakaa kwenye mkia wake.
Ng’ombe alipofi ka kwenye shughuli aliwakuta watu wengi wamefi ka, lakini kumuangalia kinyonga hakumuona na alianza kufurahi akajua kwamba hajafi ka kwa hiyo alihisi yeye ndie atakaekuwa mshindi.
Alipotaka kukaa tu alisikia sauti ya kinyonga na kumuuliza; „Mbona unataka kunikalia.“
Ng’ombe aliposikia ile sauti ya kinyonga alilia sana na kuhuzunika huku akisema; „Dunia imeniandama! Dvnia imeniandama! Dunia imeniandama! Dvnia imeniandama! Dunia imeniandama! Dvnia imeniandama!“
Aliona kwamba mke kamkosa kwa kuchelewa kufika. Hapo alisimama mfalme na akachaguliwa kinyonga kwa kufika mapema na kuozeshwa mtoto wa mfalme. Nakuona vile Kinyonga alifurahi sana kwa kuona amemshinda mshindani wake kwa kupata mke ambae walikuwa wanamgombania. Hapo Kinyonga akaanza kubadili nguo za kila aina hadi leo.
MWISHO
Kwenye Hadithi hii ya tusiwadharau wadogo umejifunza kitu gani? ningependa kusikia kutoka kwako ya kwamba kunafunzo lolote umelipata hapa…
Niandikie hapo chini kwenye comment, nami nitakujibu. pia sio vibaya kama uta share simulizi hii kwa wengine nao wapate kujifunza na kufurahi…
- 167shares
- Facebook77
- Twitter90
- Gmail
- Copy Link