in

VICHEKESHO VUNJA MBAVU: Huyu Afande Kweli Anachekesha

Vichekesho Vunja mbavu, Huyu Afande Kweli Anachekesha. Tizama kilicho tokea hapa, uniambia kitaalamu Hii tunaitaje 😂😂.

Kwa Sms za Vichekesho, Mada za Vichekesho, kauli za Kuchekesha na Vichekesho vingine Vingi vya Ku vunja Mbavu. Wewe ni Follow @japhary

HUYU AFANDE KWELI ANACHEKESHA - CHEKA TU

VICHEKESHO VUNJA MBAVU: HUYU AFANDE KWELI ANACHEKESHA.

Siku moja Askari Walikuwa wametumwa Kwenye nyumba iliyokuwa kuna ugomvi. Walipo Fika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya simu juu ya walichokikuta.

 • AFANDE: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe na Msukumio wa Chapati wa kichwa na kumuumiza vibaya sanaa.
 • ASKARI: Kha! kisa na mkasa mpaka akafanya Hilo tukio.
 • AFANDE: Mama mwenye nyumba alikua anapiga deki mumewe akaingia ndani viatu kabla sakafu haijakauka.
 • ASKARI: Sasa Mmefanikiwa kumkamata huyo mwanamke.
 • AFANDE: Bado mkuu.
 • ASKARI: Kha! sasa mnangoja nini.
 • AFANDE: Mkuu tunangoja sakafu ikauke.

BONUS JOKES.

Nani haelewi kati ya hawa?

 • Chalii: Bro naomba nitumie hela.
 • Braza: Tumia tu mpaka uchoke.
 • Chalii: Hujanielewa,nitumie hela.
 • Braza: We ndo hunielewi, nimesema tumia tu…!!!

Jamani Kuangalia Mpira Na Wanawake Ni Stresi Sana, Haya Ndiyo yaliyo mkuta huyu Husband Material.

 • MKE: Baby, yule ni nani? Ni Chris Brown..? au.
 • MUME: Yule ni Theo Walcott.
 • MKE: ile Yellow Card ni ya nini..?
 • MUME: ile ni ya Onyo, na Red Card inamaanisha mchezaji awache kucheza na atoke inje ya uwanja.
 • MKE: Oooooh! Inakaa kama traffic light! Yellow- Ilani na Red – Simama.
 • MUME: Yeah yeah, sweety..! Ndiyo hivyo.
 • MKE: je Green Card..?
 • MUME: Aaaah! Hakuna kitu kama hicho.
 • MKE: Nataka Arsenal ishinde world cup.
 • MUME: (kimya).
 • MKE: Ni nani yule mzee anakaa kama Mr. Bean..?
 • MUME: Yes sweety, yule ni kocha wa Arsenal, anaitwa Arsenal Wenger.
 • MKE: Oooooh! inamaanisha yule kocha mwengine ni Chelsea Wenger??
 • MUME: (Kabadilisha channel)

Hivi ndivyo Vichekesho Vunja mbavu, Huyu Afande Kweli Anachekesha. kwa Vituko vingine. Shuka Chini utavipata.

Nijulishe Hapo Chini Kwenye Comment ungependa Vituko kama Hivi, au Kwenye Hivi Vichekesho tuongeze Kipi Tu Punguze Kipi. Ntafurahi kusikia kutoka kwako.

Written by Admin

Space is for everybody. It’s not just for a few people in science or math or a select group of astronauts. That’s our new frontier out there, and it’s everybody’s business to know about space.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

VITUKO NA NUSU - HAWA WAZEE KIBOKO

VITUKO NA NUSU Lazima Ucheke: Hawa Wazee Kiboko

UJUGU NA POLISI KIMEUMANA - VICHEKESHO

UJUGU NA POLISI KIMEUMANA: Cheka Tu Uongeze Maisha