Vituko na Nusu lazima Ucheke kwa Vichekesho hivi. Soma Hadi mwisho upate kujua walicho kifanya hawa wazee. Maana hawa wazee kweli Kiboko. 🙌🏽
VITUKO NA NUSU: HAWA WAZEE KIBOKO.
Siku moja Bibi na Babu walisafiri wakielekea kwa mtoto wao. Ambaye hawaja muona Siku nyingi. Walipofika njiani wakawa wamechoka Sana. Wakaamua kutafuta Hoteli ili Wapumzike. Wakakubaliana walale kwa masaa 4. Wakalala, Walipoamka.
Muhudumu wa Hoteli akawatoza 500,000 Tsh. Wale wazee wakashangaa. hata kama ni hoteli ya kisasa lakini sio laki Tano kwa masaa 4. Babu akagoma kulipa akasema aitiwe meneja. Meneja akaja kuwasikiliza.
Babu: ” Kwanini bili ni kubwa hata kama ni hotel ya kisasa?”.
Manager: “kuna maswiming puli, ya kisasa”.
Babu: “Lakini hatukuyatumia”.
Manager: “Ah ah ah. Lakini mungeweza kama mngetaka”.
Babu: “Hata hivo bado Thamani yake Haijafikia kuwa laki Tano”.
Manager: “Pia Kuna waimbaji kutoka sauzi, Uganda , Congo”.
Babu: “Lakini sisi hatukuwasikiliza”.
Manager: “Ndiooo. Lakini mngeweza kama mngetaka”.
Babu akiwa na Huzuni aka kumwambia mkewe andika cheki uwape. Bibi akaandika akampa meneja. Meneja anaangalia anaona 50,000 Tsh. Akashangaa na kusema. “VP mbona Elfu hamsini” Bibi akajibu “450,000 Tsh ya kulala na mimi”…
Manager: “Lakini sijalala na wewe…”
Bibi : “ungeweza kama ungetaka”
Chezea Bibi wewe, Wanajikuta wajuaji kumbe Wazee walisha fanya Uhuni zamani. Kweli Hawa wazee kiboko. Nijulishe Hapo kwenye Comment Mtazamo wako kuhusu hawa wazee.
Kwa Vichekesho zaidi Shuka Hapo chini uzidi kuongeza Siku za Kuishi kwa Kucheka. “Maisha Mafupi pipi.. ukikunja kunja kunja Sura Utazeeka.” Ni Marioo ndo Amesema jamani.
- 185shares
- Facebook108
- Twitter77
- Gmail
- Copy Link