Tazama Matokeo Hapa
Download Mitihani
Wajumbe nawakumbusha Tamaa Mbaya. Tazama Kilicho Mkuta Shemeji yetu Hapa hatakuja Kusahau. kwani Kimemkuta Kipi..? Soma Mpaka mwisho utafahamu.
Usisahau kuni Follow @japhary kwa Vichekesho na Mada Mbalimbali za Kuvutia. 😊
WAJUMBE TAMAA MBAYA – VICHEKESHO.
Siku moja Jamaa kaenda kwa mke wa rafiki yake kwa lengo la Kutaka Ustaarabu, Wajumbe Mmesha nielewa ni Ustaarabu upi:
JAMAA: Shem Nimekuelewa kinoma, Yaani nakupenda.
MKE: Hebu toka hapa..! Je rafiki yako akijua..? tena koma.
JAMAA: Ntakupa milioni Moja. (Shem kusikia Pesa mate yakamtoka)
MKE: Basi njoo kesho mchana mume wangu akiwa kazini..!
Kesho yake Jamaa kaja na milioni Moja. wakamalizana na mke wa rafki yake, jioni ilipofika Mume akarudi Nyumbani na kumuuliza Mkewe… “Rafki yangu SAM kaleta hela yangu milioni moja..?”
MKE: akajibu kwa unyonge, “Ndio..!”
MUME: Yes! Ndio maana nampenda SAM kanikopa asubuhi jioni karejesha..!
Mke hoi…
Hivi ndivyo Vichekesho Vunja mbavu, Tuacheni tamaa Wajumbe Hili funzo mlikamate. Tamaa Mbaya ata 20% aliimba “Chunga tamaa Mbaya.” Shem katoa Kitumbua Bure, alizani amejipatia Milioo kirahisi ndani ya Siku moja.
Nijulishe Hapo Chini Kwenye Comment ungependa Vituko kama Hivi, au Kwenye Hivi Vichekesho tuongeze Kipi Tu Punguze Kipi. Nawatakia Tabasamu lenye furaha 😊😊.
- 212shares
- Facebook147
- Twitter65
- Gmail
- Copy Link